RAMANI YA UBAYA IMEKOMESHWA

Na Askofu Mkuu Josephat Gwajima


Unapoona mtu anataka kujenga nyumba lazima wazo la kujenga linaze, anampa wazo mchora ramani kwamba nataka nyumba yangu iwe na jiko, stoo, sehemu ya kufulia, shemu ya sebule iwe hivi n.k, halafu mchora ramani atakwenda sehemu ya itakapojengwa nyumba atapaangalia jua linachomozaje na linazamaze, baadaye anachora ramani na baada ya ile ramani kupitishwa inapelekwa kwa mhandisi anatoa mawazo yake kwamba sehemu hii iwekwe nondo za cm kadhaa , halafu inapelekwa kwa mjenzi ambaye anaanza kujenga sawasawa na ramani aliyochorewa akiwa pamoja na consultant anayesimamia ujenzi ili vipimo na vifaa vilivyopangwa kutumika vinatumika kama ilivyokusudiwa na baadaye nyumba inatimia.

RAMANI YA UBAYA

Kwenye ramani ya Ubaya inaanza kwa mfano huu huu, bahati nzuri huwa nafundisha maisha niliyofundisha, kwahiyo ubaya unapochorwa baadaye ubaya huu unazaa matunda.

Kwenye Biblia zamani alikuwepo Mfalme anaitwa Ahabu ambaye alioa mke wake aitwaye Yezabeli ambaye hakuwa mtu mzuri, wakati ule siku moja mfalme alipita kwenye njia karibu na nyumbani kwake akaona shamba zuri limestawi linapaliliwa vizuri na lina mbolea ambalo ni la mtumishi wa Mungu aitwaye Naboth, Ahabu alikuwa karibu na hilo shamba na watu walilisifia sana.
Mfalme huyu alikuwa na wivu juu ya lile shamba akitaka liwe lake, akaamua kumwendea Naboth ili amuuzie shamba hilo lakini Naboth akataa akisema mali aliyopewa ya urithi Mungu aepushe mbali jambo hili haliwezekani akakataa kabisa, hata kabla Mfalme hajasema bei atakayo mpatia Naboth aligoma kuliuza. Mfalme alipokataliwa alienda nyumbani kwake kwa huzuni nyingi na mke wake Yezabeli akamwona na kumwambia atalishughulikia jambo hilo yeye atulie alale.
Yezabeli huyo aliamua kuandika waraka akawaambia watu watafute mashahidi watatu waongo waende wakamsingizie Naboth amemtukana Mfalme na Mungu (kwa kawaida kwenye sheria za Israel wakipatikana mashahidi watatu kwenye jambo unapigwa mpaka unakufa) ule mchoro wa Yezabeli mke wa Mfalme ukatimia wale mashahidi wakaenda kutoa ushahidi wa uongo kwa Mtumishi wa Mungu Naboth naye akapigwa kwa mawe akafa.Baadaye mke wa Mfalme akaenda kumwambia Mumewe tayari shamba lipo mkononi mwake ainuke akalitazame.

Mfalme Ahabu akaenda kwenye lile shamba akawa analitembelea na ghafla akatokea mtu mmoja aliyeitwa Eliya mtishibi akaibuka akamwambia Mfalme umemuua mtu ili umiliki shamba, kwasababu hiyo na wewe utakufa kama yeye na damu yako itachuruzika ikilambwa na mbwa kama mtu huyu wa Mungu.
Baadaye ikatoke vita ya kawaida ambayo lengo lake lilikuwa Mfalme afe. Lakini Mfalme kwa vile alijua alishatamkiwa maneno na Nabii Eliya, aliaamua kuwaita manabii nyumbani kwake ili awaulize aende Ramoth gileadi kupigana vita au asiende?, manabii wote walimwambia kwea ee mfalme lakini kulikuwa mmoja alitwaye Sedekia alimwambia Mfalme nenda ukapigane ee mfalme (hata waovu nao huwa wanajifanya wanamtumikia Mungu).

Ila ndani ya moyo wa Mfalme Ahabu, moyo wake ulikua unawasiwasi, akamua kuwaita manabii wengine 400 na wote wakasema kwea ee mfalme, bado mfalme hakuridhika akaamua kuulizia kama kuna nabii mwingine ndipo akaambiwa yupo aitwaye Mikaya lakini hana maneno mazuri sana, mfalme akaamuru aitwe.
Nabii Mikaya akaenda kuongea na Mfalme Ahabu akamwambia na wewe sema neno kwamba niende au nisiende, kwasababu Mikaya aliona manabii wengine wamesema nenda mfalme, yeye naye akasema Mfalme kwea Ramoth Gileadi ukapigane, lakini Mfalme hakuamini Mikaya amemtamkia maneno mazuri, akamwambia nakuapisha kwa jina la Bwana wa Majeshi sema tena, ndipo Nabii Mikaya akasema ukweli wenyewe, akasema tazama niliwaona wana wa Israeli wamekwea Ramoth Gileadi lakini wamepigwa wakatawanyika kama kondoo asiye na mchungaji, baada ya maneno hayo Mfalme akaamuru nabii Mikaya akamatwe akaenda kupigana Ramoth Gileadi kupigana akawaambia wamfunge na kummpa chakula kibaya mpaka atakaporudi, wakati akiyasema hayo Nabii Mikaya na yeye akasema kama utarudi salama basi Mungu hakunituma ila mfalme akaendelea kwenda. (kama lipo jambo Duniani la kuepuka ni kushindana na watu waliotumwa).
“Wale wanaoshindana na bishara yako uliyopewa na Mungu, wanaoshindana na ndoa yako uliyopewa na Mungu, wanaoshindana na familia yako hawatakushinda kwa jina la Yesu”
Nabii Mikaya akamwambia Mfalme kama unakwenda kupigana utakufa, Mfalme akaamua kuvaa nguo za chuma badala ya za kifalme. Zamani mtu alikuwa anachaguliwa kuwa mfalme kwa uhodari wake wa kupigana vita na kwenye vita ilikuwa ukiona mtu amevaa mavazi ya dhambarau unakaa mbali kwasababu alikuwa ni Mfalme, ilikua Mfalme na Mfalme walikua wanapigana.

Siku moja Ilitokea mbinguni Mungu aliuliza ninani nimtume aende duniani kumdanganya Ahabu, mbingu nzima ikanyamaza hakuna aliyejitokeza lakini ikasikika sauti kutokea kuzimu shetani akasema nitume mimi nitaenda kumdanganya, Mungu akamuuliza utaenda kumdanganyaje yule pepo akasema nitaenda nitaingia mdomoni mwa wasaidizi wake ili wamdanganye kwa ushauri mbaya. Mungu akasema nenda ukafanye hivyo na ikawa. (kuwa makini unapopewa ushauri unaweza kupokea ushauri sio).

VITA YA AHABU

Mfalme Yehoshafati alikuwa amevaa mavazi ya Kifalme ahabu (kwenye vita usivae mavazi yasiyo yako utakufa) alipoonekana kwenye vita ile kumbe ilipangwa Mfalme akimbizwe apigwe mpaka afe, wakamfuata wakamzingira ili wamuue lakini Yehoshafati akapiga kelele akasema si yeye wasimuue nao wakamwachia. Askari mmoja katikati yao akasema anajisikia katikati ya watu hawa yupo mfalme Ahabu. Mtu mmoja akaamua kurusha mshale wa nasibu juu ili umtafute Mfalme Ahabu katikati ya watu wale, mshale ukamwona Ahabu ukashuka mpaka alipo ukatafuta mahali penye maongeo ya chuma kwenye mavazi yake maana alikuwa amevaa mavazi ya chuma ukamchoma mpaka kwenye moyo.
Kule Mikaya aliyefungwa hakusema namwachia Bwana haya yote yaliyotokea bali alisema apewe haki yake. Mfalme Ahabu alipopigwa na mshale ule alikimbizwa mpaka akaenda kuanguka na damu zikachuruzika mbwa wakaja wakaanza kumla kama Neno la mtu wa Mungu Eliya lilivyonena juu yake likatimia.
Baada ya hayo Wakaenda kumtoa Mikaya kwa heshima zote wakasema Nabii Mikaya wewe ni Mtumishi wa Bwana achana na wengine na mikaya akatoka na nchi nzima ikafurahi ikasema Hakika Mikaya ni nabii wa Mungu.


Ukiri:
“Kwa jina la Yesu nafuta ramani ya mikosi namabaya iliyopandwa kwenye kazi yangu na kwa jina la Yesu, nafuta maumivu na mikosi iliyochorwa juu ya bishara yangu, ninaharibu michoro ya giza juu yangu kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu wale waliotengeneza ramani za ubaya kwenye maisha yangu na familia yangu iwarudie wao kwa jina la Yesu. Nakusanya kundi la malaika waletao mabaya nawatuma waende kwale waliopanga mabaya juu yangu kwa jina la Yesu.” Amen

Naamuru kila ramani ya ubaya iliyochorwa juu yako iharibike na impate Yule aliyeichora juu yako kwa jina la Yesu. Amen.

Comments