![]() |
Na Askofu Mkuu Josephat Gwajima |
Hapo Jana Askofu Mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Duniani, Dr Josephat Gwajima aliitikia wito wa polisi, baada Ya mahojiano polisi waliamua kwenda kukagua nyumbani kwake, Salasala Dar es Salaam.
Upekuzi ulianza na kumalizika kukiwa na police wa upelelezi zaidi ya sita na ushahidi wa majirani wawili. Mara baada ya upekuzi walisainiana ripoti ya ukaguzi Mbele ya mashahidi hao kukiwa hakuna kitu chochote kilichopatikana kinachohusishwa na madawa Ya kulevya Au bangi.
Baada Ya ukaguzi huo polisi waliondoka na Askofu Mkuu Dr Josephat
Gwajima na kurudi naye central police majira Ya saa nne usiku kwa
mahojiano zaidi ambapo hadi muda huu bado wamemshikilia.
Imetolewa na Ufufuo na Uzima Tanzania
Imetolewa na Ufufuo na Uzima Tanzania
![]() |
Askofu Gwajima akimtukuza MUNGU katika moja ya ibada kanisani Ufufuo na uzima Ubungo. |
Comments