USIFANYE MCHEZO NA YESU MAANA YEYE ANAO WATU WENGI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi. Ukigoma wewe kumtumikia nakuambia wako maelfu wanamtumikia kwa uaminifu mkubwa.
Ukidengua wewe kudumu katika utakatifu wake hakika wapo waelfu wengi sana wanamtukuza na wakiishi maisha matakatifu.
Usifanye mchezo na YESU maana ana watu wengi sana wanaomtii.
Ukijiona kwamba bila wewe kazi ya MUNGU haiendi naomba utambue kwamba huko ni kujidanganya kulikopitiliza, Yeye MUNGU wetu anao wengi sana na wako tayari kumtumikia na Kumtii kwa uaminifu wote.
Ukigoma kuokoka wewe tambua tu kwamba huwa kuna ziwa la moto.
MUNGU wala hana hasara ila hasara ni kwako muasi usiyependa kumtii Mwokozi wako.

Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.
'' Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na KRISTO atakuangaza.Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA. Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe ROHO;-Waefeso 5:14-18 ''

Usifanye mchezo kwa YESU maana yeye anao watu wengi.
Ukigoma wewe kuokoka tambua kwamba wapo waelfu wanaokoka na uzima wa milele wataenda.

Hebu ona mfano huu  mmoja tu katika mingi sana ya watu walioamua kumpokea YESU na kuokoka, japokuwa wewe unafanya mchezo.
Matendo 2:41-42 '' Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.'' 
Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.
Kwa siku moja waliookoka watu 3000 katika eneo moja ambalo akina mtume Petro walikuwa wanahubiri injili. Hebu jiulize watu 3000 wameokoka kwa siku moja. Je kwa miaka 10 ya kuhubiri injili kutakuwa na waamini wapya wangapi? Hakika ni wengi hivyo wewe ukifanya mchezo na YESU yeye hana hasara maana wewe utakosa mbingu huku walioamua kumtii wakifurahi uzima wa milele. Usijione wa thamani sana wewe hata unasahau kuishi maisha matakatifu, ukidhani kuna unakaye mkomoa.
Jehanamu ameandaliwa shetani na majini yote lakini kuna wanadamu wataenda huko kwa sababu tu wamemkataa YESU KRISTO na Wokovu wake.
Ndugu kumbuka  ''Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. YESU aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.-Mathayo 13:49-51'' 
Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi. 


Ukikataa wewe kuacha uzinzi wako na ulevi wako na uchawi wako na wizi wako tambua kwamba MUNGU anao watakatifu wake walioitii injili yake ya wokovu lakini wewe utaangamia, unayemkataa YESU na Wokovu wake.

Utaangamia wewe unayetenda maovu.
MUNGU anao watakatifu wake, wale waliookoka na wanaishi maisha matakatifu katika KRISTO  na hao MUNGU anasema anapendezwa sana nao.
Ukisema hakuna mtu mtakatifu duniani kwa sababu wewe umeshindwa kuacha dhambi zako, tambua kwamba watakatifu ni wengi tu duniani, wameokoka na wanamtii KRISTO na Neno lake na tena hao watakatifu kwa sababu wako wengi tu MUNGU nasema ''Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.-Zaburi 16:3''

Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.
Pole wewe unayesema hakuna mtu mtakatifu duniani wakati MUNGU anajua wapo na anasema hao ni wa muhimu sana.
Usifanye mchezo kwa YESU maana yeye ana watu wengi sana.
Tengeneza ndugu leo maisha yako kwa kuokoka na kuacha dhambi zako zote.
Anza kumtii Bwana YESU na injili yake na utaitwa heri.

 Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.
 Mhuburi 12:14 '' Kwa maana MUNGU ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya. '' 

Wengine waliitwa na MUNGU ili wamtumikie lakini wamejiona wakubwa kuliko hata Neema ya MUNGU iliyowaita na sasa wanatenda mabaya na sio mema tena.
Ndugu kumbuka,Aliyeitwa katika KRISTO anatakiwa kusimama kwa niaba ya KRISTO.
Mtumishi huyo akijitambua hakika utumishi wake utakuwa mzuri sana.
Aliyeitwa katika YESU kwa imani anaweza kuombea wagonjwa na wakapona kwa sababu ameliitia jina la Bwana YESU na jina hilo huyo mtu ameitwa ili amtumikie KRISTO lakini kumbuka hii kwamba
''Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha KRISTO, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya-2 Kor 5:10''
 Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.

 Kuna Wasichana Na Wavulana Huwa Wana Juhudi Kubwa Ya Kumtumikia MUNGU Kabla Hawajaingia Kwenye Ndoa, Lakini Wakishafunga Tu Ndoa Ndio Utajiulize Je Binti Au kijana ........ Alikuja Kanisani Kumtumikia Bwana YESU? Au Alikuja Kutafuta Tu Mke Au mme Na Kuondoka? Wengi Kama Walikuwa Wanakwaya Wakishapata Tu Wenzi Wao Wanaacha Huduma, Wengi Wamejiondoa Kwenye Vikundi Vya Maombi Na Kila Huduma Na Badala Yake Wanaenda Kanisani Jumapili Tu Tena Kwa Kuchelewa. Ni Mbaya Sana. 
Kuna Wengine walikuwa Wahubiri Wazuri Lakini Walipooa Au Kuolewa Wameacha. Mmmmmmmh! Ni Mbaya.
Tumika Siku Zote Za Maisha Yako. Ndoa Isiwe Jaribu Kwako. Tumika Kwa Bwana YESU Siku Zote Utaitwa Heri.
Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.

 Miguu ya watu wengi ni myepesi sana kukimbilia disko kuliko kukimbilia kwenye mikutano wa injili, miguu ya watu wengi ni myepesi sana kukimbilia tamasha la bongo fleva kuliko kukimbilia maombi kanisani.
Ni heri kutafuta uzima wa milele kuliko kukimbilia machukizo.

Mathayo 25:31-34, 41 '' Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;''

Ndugu Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.Ukikataa wewe kuishi maisha matakatifu hakika hiyo ni kwa uangamivu wako mwenyewe.

Moyo wako unaweza kuwadanganya watu lakini hauwezi kumdanganya MUNGU.
Uwe makini maana waongo hawataurithi ufalme wa MUNGU.

Hivyo ni muda wa kutubu na kuacha maovu.
 ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye(MUNGU) ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. -1 Yohana 1:9''

Kuna mtu anajisifu kwamba yeye hufanya dhambi ndogo ndogo tu.
Biblia inamwambia hivi dhambi zote ni kubwa Tena hazifai"
" Kwa maana yeye aliyesema, usizini, pia alisema, usiue, Hivyo ukikosa katika moja umekosa katika yote(Yakobo 2:10-11).

 Ndugu Usifanye mchezo na YESU maana yeye anao watu wengi.Ukikataa wewe kuishi maisha matakatifu hakika hiyo ni kwa uangamivu wako mwenyewe.
''Amwaminiye Mwana(YESU) yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU  inamkalia.-Yohana 3:36''


KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA MATAKATIFU.

''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi, lakini leo nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike jina langu katika kitabu cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Amen.

 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments