Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. |
Kila dini wanasema kwamba kuadhimisha Valentine day(Siku ya wapendanao) ni machukizo, na Mimi nakubaliana nao kabisa.
Sasa tukubaliane kwamba wanaosherekea Leo ni wanaabudu shetani maana kila dini inakataa. Au labda wazee wa dini waligundua kwamba Leo ni siku ya wazinifu duniani ila kwa hadaa inaitwa Valentine day.
Mimi Leo nawaza tu lakini ukweli ni kwamba nyakati hizi ni za kuishi maisha matakatifu katika Wokovu wa KRISTO pekee, Bwana YESU yu karibu kurudi. Wadhambi wote sehemu yako ni katika ziwa la moto ndivyo Biblia inasema.
Sasa Kama kuna mtu anawaza kuzama kwenye mahaba ya ngono basi akumbuke pia kwamba huwa kuna kuzama kwenye ziwa la moto. Natamani ujumbe huu umponye mzinzi na mwasherati mmoja aliuekusudia kufanya uzinifu Leo. Biblia inasema " Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa.-Isaya 55:7"
tena Biblia ni inasema " Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru(YESU)
imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana
matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia
nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye
aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya
kuwa yametendwa katika MUNGU.-Yohana 3:19-21.
Kisha Bwana YESU anasema "Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.-Ufunuo 22:11-14.
Ndugu ni wakati wa kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
Hizo pesa ulizonunua nguo nyekundu ya Valentine ni heri ungewapa watoto yatima.
Kwanini nilisema sikubaliani na Valentine day?
Ni kwa sababu upendo na upendo tu na upendo Biblia inatuagiza kwamba tuwe na upendo wa siku zote. Hata kamusi ya kiswahili sanifu maana ya Neno upendo ni ilele ile, hivyo hakuna upendo special, hakuna upendo wa msimu, upendo ni upendo tu na hivyo inatupasa katika utakatifu. Kanisa kupendana siku zote kama warithi pamoja katika ufalme wa MUNGU.
Hebu jiulize Leo kuna mtu anaambukizwa magonjwa mabaya ya zinaa kwa sababu ya uzinzi wake, je huo ndio upendo?
Baba anatoka na hawara, huo ndio upendo?
Leo watu wengi watasema uongo mwingi kwa wenzi wao, je huo ndio upendo?
Matukio ya siku ya Valentine kwa wahusika wa sio hiyo asilimia kubwa sana hayahusiki na upendo ila dhambi na machukizo.
Ndugu zangu ni heri kulitii neno la MUNGU kwa kutembea katika utakatifu.
Nilikusudia kuandika ujumbe mfupi ila ka upako kameshuka na hadi nimefika hapa.
MUNGU akubariki sana na nakuomba kataa dhambi, iepuke dhambi, ikimbie dhambi na usifanye dhambi tena.
By Mwinjilisti Peter Mabula.
0714252292.
Mabula1986@Gmail.com.

Comments