FAIDA ZA KUMWAMINI YESU NA KULITII AGIZO LAKE.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Jambo la kwanza nataka ujue ni  kwamba Bwana YESU anawatafuta watu walio waaminifu ili waipeleke injili yake.
Anawatafute wateule wanaojua wajibu wao, majukumu yao na wito wao.
Ndugu, inakuaje unapenda kusifiwa na bosi wako kazini lakini hutaki kusifiwa na Bwana YESU aliyekupa injili yake ili uipeleke kwa watu wote?
Wewe hutaki kuipeleka injili, uko busy tu na kazi yako yenye malipo duniani tu na sio mbinguni.
Ndugu peleka injili ya KRISTO mbele, peleka injili kwa kuhubiri watu. Kama huna muda wa kuhubiri basi ipeleke injili kwa pesa yako kwa kuwasapoti wanaoipeleka injili. Peleka injili hata kwa kusambaza vipeperushi vya Neno la MUNGU, peleka injili hata kwa kuwaalika watu kwenda kwenye mikutano ya injili na ibadani kanisani, ni jukumu lako kuipeleka injili, ndugu timiza jukumu lako.
Kuna faida katika kumwamini YESU KRISTO na kulitii Neno la MUNGU.


Faida baadhi za kumwamini YESU na kulitii neno lake ni:

1. Kuwa pamoja na KRISTO.
Mathayo 28:19-20 " Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU ; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

 Kuwa pamoja na KRISTO ni faida kubwa mno.
Kuwa pamoja na KRISTO ni ulinzi kwako na uhakikia wa uzima wa milele kwako.

3. Kushiriki pendo la MUNGU baada ya kumaliza kazi duniani.
Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

Faida kuu ya kumwamini YESU KRISTO na kumpokea kama Mwokozi ni uzima wa milele. 

Lakini pia ni muhimu sana Kutenda mema.
2 Timotheo 3:16-17 " Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema." 

Kutenda mema ayatakayo MUNGU chanzo chake ni kumwamini YESU KRISTO na kulitii Neno lake.
Kumwamini YESU hukufanya umpendeze MUNGU na kutemba mema ambayo ni faida kwako.Lakini pia Ndugu nakuomba pia usiishie kumwamini YESU tu bali mtumikie pia huku ukiishi maisha matakatifu katika yeye.

Ndugu yangu nakuomba sana ihubiri injili ya KRISTO siku zote, huku ukiishi maisha matakatifu katika yeye na huku ukimtii ROHO MTAKATIFU.
Sababu ya kanisa kuwepo ni ili kwenda ulimwenguni kuhubiri injili ya KRISTO, Ni agizo la kila aliye Kanisa kutoka kwa mwenye Kanisa.
Marko 16:15-16" Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa."

Kanisa ni wateule wa MUNGU hivyo ni muhimu sana kila aliye Kanisa hai la MUNGU aende ulimwenguni kuipeleka injili ya KRISTO kwa watu wote.
Kuna watu wanaikalia injili, wala hawaipeleki.
Kuna watu wamekaa mbali na kuihubiri injili ya KRISTO.
Kumbuka Kanisa ni wateule wa MUNGU waliookolewa kwa damu ya YESU KRISTO.

Yohana 1:12-13 '' Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;
 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''

 
Kazi ya Kanisa ni kuipeleka injili.

Katika kanuni ya kiroho ni kwamba ukifundishwa Neno la MUNGU la injili inakupasa na wewe kuwafundisha wengine.
Wokovu wa KRISTO ndio jambo muhimu kuliko yote la wewe kujifunza na kisha wewe kufundisha wengine.
2 Timotheo 2:1-2 "Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika KRISTO YESU. Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine."


Ni muhimu sana injili iende mbele.
Mtaji wa injili ni wewe mteule uliye tayari kuipeleka injili mbele.
Unapoacha kuipeleka injili unakuwa unapingana na maono ya KRISTO ambaye ndiye mwenye Kanisa.
Mitume walihubiri injili kwa bidii, kwanini wewe usihubiri injili?
Hebu ona jinsi mitume walivyojitoa kuhubiri.
Matendo 28:30-31 " Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za ufalme wa MUNGU, na kuyafundisha mambo ya Bwana YESU KRISTO, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu."

Ndugu yangu hubiri injili.

YAMPASAYO MTEULE WA MUNGU.

1. Kudumu katika fundisho la KRISTO.
Wakolosai 3:16 ''
Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu.''
 Ni muhimu sana Kudumu katika kuumega mkate wa kiroho yaani kulila Neno la MUNGU ili likalete afya ya rohoni.
Mathayo 4:4 ''
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha MUNGU.''
Kama ambavyo tunakula chakula cha kimwili ili tuwe hai  vile vile tunakula chakula cha kiroho ili tuwe hai kiroho.
Chakula cha kiroho ni Neno la MUNGU.

2. Kudumu katika ushirika na ROHO MTAKATIFU.
2 Kor 13:14 ''
Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.''
Yaani ya KRISTO ilituvuka kwenye Wokovu ndio maana tukampokea YESU KRISTO kama Mwokozi wetu.
Upendo wa MUNGU ni msamaha kwa wanaotubu na kuacha uovu.
Upendo wa MUNGU ni kumleta Mwanaye wa pekee ili tupate uzima wa milele bure.
Baara ya kuokoka jambo kuu linalofuata ni kuwa na ushirika na ROHO MTAKATIFU ndipo utashinda.
Bibla ROHO MTAKATIFU ni vigumu kuwa mtakatifu, ni vigumu kumpendeza MUNGU.
Nila lazima sana kila mteule wa MUNGU kuwa na ushirika na ROHO MTAKATIFU ndipo atampendeza MUNGU.
Kumbuka Tunamkaribia MUNGU BABA katika YESU KRISTO kwa njia ya ROHO MTAKATIFU.
Tunamwabudu MUNGU BABA kwa njia ya YESU KRISTO katika ROHO MTAKATIFU.
Tunaomba kwa MUNGU BABA kwa njia ya ROHO MTAKATIFU katika jina la YESU KRISTO.
Biblia RHO MTAKATIFU wa MUNGU hakika wateule hatuwezi kukamilika katika viwango vya MUNGU.
Warumi 8:14 ''Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

3. Kudumu katika kusali.
Matendo 2:42. ''
Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.''
Kanisa la kwanza linatupa kanuni njema ya maisha ya Mkristo yanavyotakiwa kuwa.
Kwanza Mkristo anatakiwa kudumu katika fundisho la Neno la MUNGU.
Jambo la pili Mkristo anatakiwa kuwa na ushirika na ROHO wa MUNGU na pia ushirika na Kanisa la MUNGU.
Jambo la tatu ni muhimu sana mteule kudumu katika kuumega mkate.
Jambo la nne muhimu sana kwa kila mteule wa MUNGU ni kudumu katika kusali.
Kusali kunaunganisha mambo mengi sana yakiwemo maombi, ibada, kusifu na kuabudu.
Je wewe unadumu katika hayo?
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Umeshashare sana jumbe zisizo na maana leo
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments