KUITWA NA KRISTO ILI KUWARUDISHA WATU KWA MUNGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe wapendwa.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Nasukumwa sana kumshauri mtu mmoja jambo hili.
Ni muda sasa Leo nasukumwa kumshauri hata kama simjui na sijui anaishi wapi na dhambi yake ni nini, sijui kama ni mtumishi au kama ni mtu wa aina gani na ana hadhi gani, ila kwa sababu ya msukumo huo ndani yangu basi naamini atausoma ujumbe wangu na  aliyeniongoza Mimi kumshauri ndugu huyu, basi atamsaidia ndugu huyu katika hili kama akitii.
Jambo lenyewe ni hili:

"Hiyo dhambi ambayo umeshindwa kuiacha naomba ujue kwamba dhambi hiyo inaiba maisha yako.
Sasa kwanini uendelee kuibiwa maisha yako kila siku?
Kumbuka kuna ziwa la moto kwa watu wadhambi kama wewe, lakini pia ukitubu kwa YESU KRISTO na kubadilika leo hakika kuna uzima wa milele. Mlango wa kuingia mbinguni umeandikwa UTAKATIFU NA HAKI. 

YESU KRISTO hakika anaokoa, ukimpokea Leo hakika unaokoka. Hata kama dhambi zako ni nyingi kiasi gani, ukitubu kwake na kuziacha dhambi hizo hakika unaokoka"
Isaya 1:16-20 ''16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya. ''
Hicho ndicho nilisukumwa sana kukushauri ndugu yangu.
Neema ya KRISTO bado ipo hivyo ni vizuri wewe kutubu na kuacha uovu huo.
Hata Mimi sijui kwanini nimekuambia maneno haya lakini yule aijuaye kesho yako ameniambia nikuonye.
Wakati wa wewe kuokoka haswaa ni sasa.

Mathayo 3:2 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''
Bwana YESU anakupenda sana na anataka usiende ziwa la moto, Bali uende uzima wa milele.
Ubarikiwe sana kama ukiacha uovu huo na kuanza kumtii MUNGU Baba.

Zaburi 34:14 '' Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie. ''

Hakuna Mtumishi Yeyote Wa MUNGU Ambaye Hajaitwa Na MUNGU. 
Unaweza Ukawadharau Baadhi Ya Watumishi Wa MUNGU Kwa Sababu Ya Mazingira Yao Na Huduma Zao Lakini Ukweli Ni Kwamba Mazingira Yao Magumu Hayawaondoi Katika Kuitwa Kwao Na MUNGU. 
Ndugu, Mweshimu Kila Mtumishi Wa MUNGU Hata Kama Anachunga Kanisa Lenye Watu Watatu Wakati Wewe Kanisani Kwenye Mko Waumini Zaidi Ya Elfu Mbili. 
Mheshimu Mtumishi Huyo Maana Ni MUNGU Aliyemuita. 
Kama anakuonya katika KRISTO hakina badilika.
Kama anakukemea katika haki na kweli hakika tengeneza maisha yako kwa Bwana YESU.
Hakuna aliye wa kudumu duniani, ni wajibu wa kila mtu kumtii MUNGU na Neno lake.
MUNGU hulituma Neno lake kupitia watumishi wake aliowachagua yeye bila kujali elimu wala ufahari wa mali.
Kazi ya watumishi wa MUNGU ni kuwarudisha wanadamu katika njia ya kweli na uzima.
Biblia inawataka watumishi wa MUNGU kuisema kweli ya KRISTO bila woga.
2 Timotheo 4:1-2 ''Nakuagiza mbele za MUNGU, na mbele za KRISTO YESU, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;  lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.''

Watumishi wa MUNGU wameitwa na MUNGU ili kulitimiza kusudi la MUNGU la injili ya Wokovu.
Waliookoka wote wanaishi maisha matakatifu ni watumishi wa MUNGU, kumbuka hiyo usije ukasahau hata siku moja. Lakini Ukimuona Mtu Ni Mtumishi Mzuri Kanisani Ujue Ni Kwa Sababu Tu Aliandaliwa Vizuri Ili Aje Awe Mtumishi Mzuri. Kazi Ya Kuwaandaa Watumishi Wazuri Inaweza Isiwe Nyepesi Lakini Siku Zote Watumishi Wazuri Kanisani Ni Wale Walioandaliwa Vizuri. Yoshua Aliandaliwa Na Musa Ndipo Akawa Mtumishi Mzuri. Elisha Aliandaliwa Na Eliya Ndipo Akawa Mtumishi Mzuri. Je Wewe Unaandaliwa Na Nani Ili Uje Uwe Mtumishi Mzuri Kanisani?
Kazi ya wateule wa KRISTO kama watumishi wa MUNGU ni kuishi maisha matakatifu ya Wokovu na kuwarudisha wanadamu wote kwa JEHOVAH MUNGU wao.
Wito wa MUNGU kwa watumishi wake ni huu
 '' Wahurumieni wengine walio na shaka, na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili. Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye MUNGU pekee, Mwokozi wetu kwa YESU KRISTO Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.-Yuda 1:22-25 ''

Tahadhari ni hii kwa wateule; siku hizi watumishi wengi hawataki kukaa chini ya uongozi wa Kanisa kwa ajili ya kuandaliwa, bali hukurupuka na kuingia katika huduma. Hapo utawatambua kwa utumishi wao, kwani hufanya yaliyo yao,wala siyo ya Mungu.
Ndugu, kila mtu atalipwa sawasawa na matendo yake.  Hakuna Anayezijua Dhambi Za Wakristo Kama Mtenda Dhambi. Mtenda Dhambi Akimuona Mkristo Anatenda Isivyo Atamwambia "waliookoka Huwa Hawafanyi Hivyo" Japokuwa Yeye Hufanya Hivyo Kila Siku. Hiyo Huwasaidia Sana Waliookoka Kudumu Kwenye Utakatifu Sahihi Huku Mtenda Dhambi Akiendelea Kudumaa Kwenye Dhambi Zake. Kila Mmoja Atalipwa Sawasawa Na Matendo Yake. 
BWANA YESU Anasema " Mwenye Kudhulumu Na Azidi Kudhulumu; Na Mwenye Uchafu Na Azidi Kuwa Mchafu; Na Mwenye Haki Na Azidi Kufanya Haki; Na Mtakatifu Na Azidi Kutakaswa- Ufunuo 22:11"

  Ndugu yangu naomba nikushauri kitu hiki, Msogelee Zaidi MUNGU Ili Akutakase Zaidi. Maombi Ni Njia Mojawapo Muhimu Ya Kumsogelea MUNGU Zaidi.
Ni muhimu sana ukatii agizo la MUNGU la kuitwa kwako katika Kanisa la MUNGU.
Wakati wengine wanajihubiri wao, wewe mhubiri YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati wengine wanahubiri madhehebu yao, wewe mhubiri YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati wengine wanawahubiri waanzilishi wa madhehebu yao,wewe mhubiri YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati wengine wanawahubiri viongozi wao wakuu wa madhehebu yao, wewe mhubiri YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati wengine wanahubiri sabato tu ya kiyahudi, wewe mhubiri Bwana wa sabato YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati wengine wanahubiri baraka tu,  wewe hubiri Wokovu wa YESU KRISTO anayeokoa, hubiri ufalme wa MUNGU na baraka zote utazipata.
Mathayo 6:33 '' Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.''
Wakati wengine wanavihubiri vitabu visivyo Biblia, wewe mhubiri YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati wengine wanamtumikia shetani, wewe mtumikie  MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi.
Siku moja nilisikia sauti hii '' Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo?-Yeremia 47:7a '' nikagundua hakika waliookoka wote tumeokolewa kwa kusudi ili tuwalete na wengine kwa YESU.
Naomba nimalize kwa ushauri huu.
Kama mtu anataka kuwa mtumishi mzuri na kiongozi mzuri kanisani basi ahakikishe anakuwa na:
1. Moyo wa upendo kwa watu wote.
2. Imani thabiti katika KRISTO.
3. uvumilivu katika magumu na furaha njema.
4. Awe muombaji na anayejali mahitaji ya wengine na kuwaombea.

Ndugu unayetaka kumtumikia MUNGU katika KRISTO hakikisha huna  roho hizi chafu, au kama unazo zifute kwa damu ya YESU KRISTO zikuachie:
1. Roho ya Absalom ambayo ni roho ya usaliti.
2. Roho ya Kora ambayo ni roho ya uasi.
3. Roho ya uchawi na ushirikina.
4. Roho ya Jezebel ambayo ni roho ya kuabudu miungu, uzinzi na kujipamba kipepo.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments