MAMBO MATATU AMBAYO BIBLIA INAZUNGUMZIA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Biblia inazungumzia mambo matatu tu.
1. Yaliyopita.
2. Yaliyopo.
3. Yajayo.


✔✔Ndugu tengeneza kwa YESU kwa ajili ya yajayo yako.
Ufunuo wa Yohana 1:19 "Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo."


1. Yaliyopita yanatakiwa kutupa akili ili katika wakati wetu, tutende vyema tukimpendeza MUNGU Muumba wetu.
Biblia inayazungumzia yaliyopita kwamba

 "Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.-1 Kor 10:11"
Yaliyopita ni yale yaliyowapata kwa jinsi ya mwili na roho wana wa Israel pamoja na mababa wa imani walioishi kabla ya waisrael.
Hao walipewa sheria na taratibu za kuishi ili wampendeze MUNGU.
Kupitia hao tunajifunza jinsi madhara ya kumwasi MUNGU yalivyo.
Hayo yanatusadia sisi kujichunguza na kujikagua ili tusitoke katika mpango wa MUNGU wa wakati wetu. 
2 Timotheo 2:19 '' Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu.''

2. Yaliyopo yanatuonyesha tuko katika wakati gani na nini cha kufanya.
✔✔Tuko katika wakati wa Injili ya KRISTO iokoayo.
✔✔Tuko wakati wa wokovu.
✔✔Tuko wakati wa kufanyika watoto wa MUNGU waliompokea Bwana YESU na kutakaswa dhambi zote.
2 Wakorintho 6:1-2 " Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)"
✔✔Tena yaliyopo yanahitaji moyo wa toba.
Marko 1:15 " Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili."

✔✔Yaliyopo yanahitaji tuenende kwa ROHO MTAKATIFU.
Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."

✔✔Yaliyopo yanatutaka tuwe Watakatifu kama kweli tunapenda yajayo yetu yawe uzima wa milele.
1 Yohana 2:15-17 "Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele."


3. Yajayo ni siku ya hukumu.
Mathayo 12:36 "Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu."

✔✔Yajayo ni uzima wa milele kwa watakatifu wa KRISTO YESU.
''Yeye amwaminiye Mwana wa MUNGU(YESU) anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini MUNGU amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao MUNGU amemshuhudia Mwanawe(YESU).Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba MUNGU alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana(YESU), anao huo uzima; asiye naye Mwana wa MUNGU(YESU) hana huo uzima.Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa MUNGU.-1 Yohana 5:10-13 ''

✔✔Yajayo ni jehanamu ya moto kwa waliomkataa YESU na kuacha utakatifu.
Mathayo 25:41 "Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;"


Ndugu,tengeneza kwa Bwana YESU yajayo yako Leo.
Kumbuka ''Amwaminiye yeye(YESU) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU .-Yohana 3:18''

Yajayo yanamuhusu kila mwanadamu kuamua leo.
Kila mwanadamu wa dini yeyote duniani anamgoja Bwana YESU ili aje ahukumu ulimwengu.
Wakati huu ni wakati wa Kumwabudu MUNGU katika kweli yake, wokovu ndio kweli.
Huu ni wakati wa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU, Maana yeye ndiye muhuri wa MUNGU ndani yetu na ndio msimamizi wa kanisa la KRISTO Duniani.
 Waefeso 1:12-13 '' Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea KRISTO tumaini letu. Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na ROHO yule wa ahadi aliye Mtakatifu.''
 
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
 Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments