ROHO MTAKATIFU NI WA MUHIMU MNO KWA KILA MKRISTO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze Neno la Uzima.
Kuna tofauti Kati ya ROHO MTAKATIFU kuwa ndani yako na ROHO MTAKATIFU kuwa juu yako.
ROHO MTAKATIFU kuwa ndani yako ni ujazo wa ROHO MTAKATIFU ndani yako, ni kujaa nguvu za MUNGU ndani yako.
1 Kor 12:13 ''Kwa maana katika ROHO mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa ROHO mmoja.''


ROHO MTAKATIFU kuwa juu yako ni kupakwa mafuta na ROHO MTAKATIFU ili uifanye kazi ya MUNGU katika kusudi alilokupangia ROHO MTAKATIFU.





Luka 4:18-19 ''ROHO wa BWANA yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa.''   
ROHO MTAKATIFU kuwa juu yako huja baada ya ROHO MTAKATIFU kuwa ndani yako.
ROHO MTAKATIFU akiwa juu yako haina maana kwamba hatakuwa ndani yako.


ROHO MTAKATIFU huwa haji na kuondoka kwa mteule wa KRISTO, Bali dhambi zako tu ndizo zinaweza kumwondoa ndani yako.
Kunena kwa lugha ni udhihirisho wa nguvu za ROHO MTAKATIFU ndani ya mwamini.

Kama hutaongozwa na ROHO MTAKATIFU hakika ni vigumu wewe kuwa mtakatifu halisi.
Anayetaka kuwa mtakatifu ni muhimu sana amtii ROHO MTAKATIFU.

Ndugu, wakati unamngoja MUNGU, Je umekataa katika njia ya ROHO MTAKATIFU?
Katika nafasi yako ya kumtumikia MUNGU, Je umempa ROHO MTAKATIFU nafasi kubwa kiasi gani?
Hata marafiki zako ulionao inapasa ROHO MTAKATIFU awathibitishe.

ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana kwa waenda mbinguni.
ROHO MTAKATIFUni wa muhimu katika maisha yetu, huduma zetu, kazi zetu na karama zetu.
Ni lazima uongozwe na ROHO wa MUNGU ili uyapate mahitaji yako.
Zaburi 23:1 "BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu."
Kuyatenda mapenzi ya MUNGU kutakusaidia usipoteze baraka za MUNGU.
Uongozi wa ROHO MTAKATIFU katika kila ufanyacho mteule ni muhimu sana

Ishara ya Mteule kujua kama ROHO MTAKATIFU anakuongoza ni Kusikia sauti ya ROHO MTAKATIFU na kuona ile hali ya kutokupungukiwa na kitu(Zaburi 23:1)
Kila Mara unatakiwa umsikilize ROHO MTAKATIFU ndipo utafanikiwa.

Warumi 8:14 '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''
Kama macho yako ya rohoni hayaoni hakika kuna vitu utakuwa kwenye wakati mgumu sana kuvijua, unahitaji ROHO MTAKATIFU akuongoze na kukujulisha.
Uongozi wa ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana hata tunapopewa vitu au zawadi na watu.
Ndugu, ni lazima uongozwe na ROHO MTAKATIFU ili uweze kuishi mahali ambapo MUNGU amekusudia kukubariki.
Ishara ya kwanza ya kujua pale alipokusudia MUNGU kukubariki utaona na kuwa na amani.

Wagalatia 5:25 ''Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.''

Kila anayemtumikia KRISTO ni mtumishi wa MUNGU, lakini ni lazima uongozwe na ROHO wa MUNGU ili uweze kuyafanya mapenzi ya MUNGU makamilifu.
Ni lazima uongozwe na ROHO MTAKATIFU ili MUNGU akuinue.

MUNGU anapotaka kukutumia;
1. Hukupa shauku ya kwenda nyumbani mwake na kujifunza yaliyo yake kwenye kusudi alilokuitia.

2. Kadri unavyozidi kumtii MUNGU ndipo MUNGU atakupa nafasi ya wewe kuwaongoza wengine.
ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana kwa waenda mbinguni.


JINSI YA KUJENGA UHUSIANO MZURI NA ROHO MTAKATIFU.
1. Kuwa mtii kwa ROHO MTAKATIFU.
Yohana 14:26 ''
Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.''
Kazi ya ROHO MTAKATIFU kwa mteule wa MUNGU ni kumfundisha, kumkumbusha na kuelekeza, hivyo ukimtii katika dasara lake unakuwa unamtii, na kwa njia ya kumtii utakuwa unajenga uhusiano na yeye.

2. Weka Neno la KRISTO kwa wingi ndani yako na litafakari hilo.
Wakolosai 3:16 ''
Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu.''
ROHO MTAKATIFU ndiye mletaji wa Neno la MUNGU kwa wanadamu, yaani ndiye mwandishi wa Biblia akiwatumia wanadamu aliowachagua.
ROHO MTAKATIFU hulitumia Neno la KRISTO lililo ndani yetu ili kutusaidia .
Neno la KRISTO huufanya uhusiano kati yetu  na ROHO MTAKATIFU kuwa safi maana ROHO MTAKATIFU hulitumia Neno la KRISTO kutusaidia.

3. Tenga muda wa kuomba katika yeye.
Yuda 1:20 ''
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU,''
ROHO MTAKATIFU hutuombea kupitia maombi yetu.
ROHO MTAKATIFU anaweza kutuombea kupitia maombi yetu ya Kunena kwa Lugha katika yeye.
ROHO MTAKATIFU hutoa maelekezo katika maombi ili kutusaidia sisi.
Maombi huboresha uhusiano na MUNGU na maombi katika ROHO MTAKATIFU hutengeneza uhusiano mzuri kati yetu na ROHO MTAKATIFU na MUNGU pia.
Katika Maombi ROHO MTAKATIFU huzungumza hivyo maombi huujenga uhusiano wetu na ROHO wa MUNGU.

Zingatia sana hayo wewe mtu uliyeokoka.
Kwa ambaye hujaokoka hakika unaokoka kwanza maana Bila kumpokea YESU huwezi kumpata ROHO MTAKATIFU.
Kitu muhimu sana kingine ni hiki;
Baada ya hayo Muombe ROHO MTA
KATIFU akujulishe kusudi la YESU KRISTO kukuokoa.

Waefeso 3:16 '' awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya ROHO wake katika utu wa ndani. ''


ROHO MTAKATIFU  ana vitu vingi lakini sio vyote vinampasa kila mteule.
Vingine
ROHO MTAKATIFU  hugawa kama zawadi kwa aliowachagua.
Mfano karama na Huduma na vipawa.

1 Kor 12:4-7 '' Basi pana tofauti za karama; bali ROHO ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na BWANA ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali MUNGU ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa ROHO kwa kufaidiana.''

 Wateule wa MUNGU tuna safari inayoendelea. Jambo muhimu ni kumtii Kiongozi wa safari ambaye ni YESU KRISTO.
Maisha ya wokovu ni safari ndefu inayohitaji utii kwa MUNGU na kuendelea na safari.

Lengo la shetani tufe lakini lengo la Bwana YESU tuishi, ndio maana tunaishi Leo.
Ndugu endelea mbele na safari, endelea na utakatifu na endelea na maombi na imani.

 Kutafuta ukamilifu ndio kazi pekee iliyobaki kwako mteule wa KRISTO.
Ndugu yangu nakuomba tafuta ukamilifu.
Kutafuta ukamilifu ndio kazi ya Kanisa iliyobaki kwa Kanisa la MUNGU duniani.
Ndugu tafuta ukamilifu.
Shetani hakudai chochote Bwana YESU amekulipia madeni yako yote, uko huru sasa ndani ya Mwokozi YESU KRISTO hivyo tafuta ukamilifu.
Ni lazima uongozwe na ROHO MTAKATIFU ili kutimiza ukamilifu sahihi.
Kumbuka Kanuni ya sheria ni kwamba ukiitii utaitwa heri, lakini usipoitii itakufunga.
Tafuta ukamilifu.
Bwana YESU yu karibu kuchukua Kanisa lake.

Kama hukui kiroho maana yake unadumaa kiroho?
Kwanini udumae kiroho?


Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

BWANA YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.

Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

+255714252292.


mabula1986@gmail.com
 Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments