SHUHUDA KUTOKA KANISA LA EFATHA MWENGE



Richard Isack AKIONYESHA SEHEMU ALIPOFANYIWA UPASUAJI WA KUONDOLEWA FIGO.

USHUHUDA:
Richard Isack AKISHUHUDIA
Naitwa Richard Isack ninamshukuru Mungu kwa Matendo MAKUU aliyonitendea mimi pamoja na familia yangu. Nilikuwa na matatizo ya figo tangu mwaka 2014, nilienda Hospitali nyingi ili kufanyiwa uchunguzi na waliponifanyia vipimo walijua kuwa figo zangu zote hazifanyi kazi, nilifanyiwa upasuaji na kuondolewa figo moja tu kwa kuwa sikuwa na pesa ya kutoa zote mbili.
Baada ya kufanyiwa upasuaji nikawa nahisi maumivu makali sana, niliporudi Hospitali nikaambiwa ndani ya figo moja kuna mpira umesahaulika, na wakati huo sikuwa na pesa ya kufanyiwa upasuaji mara nyingine, niliishi kwa kukata tamaa kwani sikuweza kufanya chochote na niliendelea kuteseka.
Siku moja Watumishi wa Efatha walifika nyumbani kwangu wakamshuhudia mke wangu, akakubali KUOKOKA lakini mimi nilikuwa bado sijaokoka, mke wangu aliendelea kuja Kanisani na mimi nikaanza kuona hamu ya KUOKOKA na siku moja akaniambia tunatakiwa kwenda Precious Center Kibaha (Mji wa maombi Efatha) kwa ajili ya Ibada ya Mkesha na Maombi.
Nilikubali kwenda na ulipofika muda wa wagonjwa kuonana na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na mimi nikawa mmoja wao, mbele yangu alikuwa ametangulia Mke wangu na mtoto, Mtumishi wa Mungu akawaombea na wakapita, na ilipofika zamu yangu nilishangaa kumuona Mtume na Nabii akiniangalia sana, nilihisi kama yale macho yananiona mpaka ndani ya figo yangu.
Baadaye Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alinigusa sehemu ya mbavu sikuona maumivu wakati siku za nyuma ilikuwa mtu akinigusa tu nilikuwa naumia sana lakini siku hiyo sikuona maumivu yeyote yale. Nilishangaa na nikaona nimepona na hata ule mpira uliokuwa umesaulika haukuendelea kunisumbua tena.
Hakika nimemuona Mungu naye AMENITETEA na Kunifanya niwe MZIMA na leo NIMEPONA, NAMTUKUZA Mungu sana juu ya Maisha yangu na juu ya familia yangu kwa ujumla, kwani hata Mtoto wangu naye aliyekuwa anasumbuliwa na kubanwa na kifua (PUMU), alikuwa kila siku ni lazima achome sindano na ameze vidonge lakini baada ya yale Maombi AMEPONYWA kabisa, na HAJAWAHI kuchoma sindano wala kumeza vidonge tena. Namtukuza MUNGU kwa mambo makubwa ALIYONITENDEA, SIFA na UTUKUFU namrudishia YEYE pekee.
YOTE YAWEZEKANA KWA YEYE AAMINIYE.



Lea Mbaga AKISHUHUDIA

 USHUHUDA:
Naitwa Lea Mbaga napenda kumshukuru Mungu kwa uponyaji juu ya maisha yangu. Ilikuwa mwaka jana mwezi wa pili tarehe 5, nilikuwa nasubiri kufanya kipindi cha safari ya imani cha Trenet TV, nikawa niko nje ya Kanisa nakunywa chai nikisubiri kufanya mahojiano na watumishi wa Mungu lakini kwa bahati mbaya pale nilipokuwa nimesimama dirisha lililokuwa limefunguliwa lilidondoka likanipiga kichwani upande wa nyuma. Kuanzia hapo sikuelewa kilicho endelea, ndipo Mtumshi Urasa akanipelea Hospitali ya Lugalo nilichomwa sindano ya kupunguza maumivu lakini maumivu hayakupungua. Nilipelekwa Muhimbili na nilipofika nilitundikiwa dripu ndipo maumivu yakapungua kidogo, nilipopigwa x-Ray ikaonekana kuna uvimbe kwenye ubongo wangu. Daktari aliniambia natakiwa kupunzika mahali palipo tulia ndipo nilipokuwa nyumbani sikujua kuwa kuongea na simu ni shida, nikaongea na simu hiyo simu ndiyo ilitibua kila kitu kwa maana kichwa kilizidi kuniuma zaidi ya mwanzo na ndipo nikashindwa kutembea kabisa na nikawa napoteza fahamu kila saa. Nikapelekwa Moi na ndipo wakajua kuwa natakiwa mapumziko sana na nisikae mahali penye kelele na ndipo nikarudi nyumbani. Nilikuwa siwezi kutembea kwa muda wa miezi miwili, namshukuru sana Mungu kwa ajili ya watumishi wake waliokuwa wanakuja kuniombea kila siku, nikawa na imani kuwa ipo siku nitatembea tena, nikaanza hatua za mwanzo kama mtoto nikaanza kutambaa na kutembea kwa kupitia ukuta. Namshukuru sana Mungu kwa kuniponya sina cha kumpa zaidi ya shukrani za moyo wangu, Sifa na Utukufu namrudishia Mungu maana yeye anastahili.

Na Mtume na Nabii: Josephat Elias Mwingira ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Efatha.

Comments