TOBA YA KWELI NA MALIPIZI

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza Wambua

Bwana Yesu asifiwe?
Kama nilivyoharifu; karibu kwa somo hili muhimu sana kwa wanadamu wote kwani wengi wamekuwa wakifanya toba isiyo ya kweli na unapata kuwa wamepotea.
Wokovu unapatikana kwa Yesu tu na wala sio mwingine yote.
Matendo 4:12 "Hakuna wokovu katika mwingine kwa maana hakuna jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu ambalo kupitia hilo lazima sote tupate kuokolewa"
Hapa tumejua kuwa kuokoka kunapatikana kwa Bwana Yesu kupitia kutubu na kusamehewa dhambi zote kisha kuziacha kabisa.
Luka 1:77 "Uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao"
Kuna dini sisizijua toba ya kweli; waumini wake wanaenda kutubu dhambi kwa viongozi wao badala ya kwa MUNGU wa mbinguni.Hii ni toba isiyo ya kweli kwani mwanadamu hawezi kusamehea kwa mujibu wa maandiko.
Ili toba Iwe ya kweli; ni lazima mhusika auzunike sana moyoni juu na dhambi aliyoitenda kujitambua kuwa yeye ni mtenda dhambi.(2Korintho 7:9-10; Isaya 55:7)
Mithali 28:13"Afichaye dhambi sake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye atapata rehema"
Toba ya kweli ni lazima mhusika ageuze uso na kuyaacha machukizo ya mwanzo na asiyarudie tena.
Ezekieli 14:6 "Kwa sababu hiyo nawaambia nyumba ya Israeli; Bwana MUNGU asema hivi; rudini nyinyi mgeuke na msirudie vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu tena".
Toba ya kweli ni lazima kuacha dhambi kabisa na kurudi kwa njia za MUNGU kwa moyo mpya na kuwa tayari kutenda yaliyo halali.
Mathayo 21:30 "Akamwendea yule wa pili akasema vile vile naye akajibu akasema; "sitaki" basdaye akatubu akaenda"
Toba ya kweli lazima uwe tayari kufanya malipizo ( masahihisho) uliyoyafanya kabla ya toba.Kwa mfano kama uliiba mali za watu unaowajua uwaregeshee mali zao.
Luka 19:8 " Lakini Zakayo akamwambia Bwana; tazama nusu ya mali zangu nitawapa maskini na chochote nilichonyang'anya mtu yeyote kwa shtaki la uongo nitamrudishia mara nne"
Zakayo alitambua kuwa lazima afanye malipizo (masahihisho ya makosa aliyokuwa ametenda kabla) ili toba yake ikubaliwe na Mungu.Kama hangekubali kutenda haya asingesamehewa hata akifunga na kuomba.Hata wewe uliyeokoka ni lazima uregeshe bunduki yako uliyoipata kiharamu ulipokuwa mwenye dhambi na uwe tayari kwa lolote lile.Kama umeokoka kweli polisi hawatakudhuru ukiregesha.

Kumbuka kama hautautii ujumbe huu wa MUNGU ndio utakaokuhukumu siku ya kiama.
Yohana 4:16 "Akamwambia; "Nenda ukamwite mume wako mje naye hapa"
Habari za Yesu kisimani mwa Yakobo na yule mwanamke mzinzi msamaria zilionyesha kuwa:
Yesu hangemkubalia kumpa maji ya uzima mwanamke huyu mwenye waume watano na kati yao hapana mumewe.Yesu alitumia akili kwa kumtuma akamwite mumewe na kwa maana hakuwa na mume; mwanamke akafanya toba ya kweli ya kutangaza ukweli wako kuwa:
Mstari 17 "Mwanamke akasema " Sina mume" Yesu akamwambia "umesema vema kuwa huna mume"
Yesu alijua kuwa kama angempa maji ya uzima pasipo kujihukumu na kuhuzunika moyoni; mwanamke huyo hangepata toba ya kweli.
Agizo la Yesu la kumlete mumewe lilimfinya mno moyoni yule mzinzi akajihukumu na kuutoa ukweli wake.Hapo ndipo anapojua kuwa Yesu ni nabii.
Mstari 19 "Bwana naona kuwa wewe u nabii"
Malipizo ni kutenda matendo yanayoambatana na kutubu kwetu; kufanya masahihisho ya makosa tuliokosa; tukakosea watu ili watu wasitulaumu kwa karama ya wokovu.
1Korintho 8:20-21 "Tukijiepusha na neno hili mtu adije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia...."
Baadhi ya malipizo ambayo tunatakiwa kuyafanya ni pamoja na:
1.Malipizo ya kuachana na wanaume/wanawake.
Baada ya kuokoka ni lazima tuangalie vizuri kama mume/mke tuliye naye ni halali kwa ndoa yetu.Tunaweza kuwa tulinyang'anya wenzetu make/mume wao kabla ya kuokoka; basi tukishaokoka ni lazima turegeshe vya watu.
Mke/mume wako halali ni yule wa kwanza uliomwendea kwa wazazi ukakabidhiwa (Mathayo 19:4-6)
Kama tulikuwa tukiishi na mvulana/msichana kama make/mume bila idhini ya wazazi wake ni lazima tutubu dhambi ya uasherati na kuachana naye kabisa tukishaokoka.(Yoshua 23:11-13)
Amosi 3:3 "Je; watu wawili wanaweza kutembea pamoja bila kupatana?"
2Korintho 6:14-15 " Msifungwe nira moja na wasioamini....."
Katika malipizo ya uasherati/uzinzi tunapaswa kurejesha vitu vyote tulivyopewa kutokana na dhambi hii.Kama ulikuwa umenunuliwa saa; simu; ploti; gari n.k ni lazima turejesha kwa maana tumeokoka kwani Bwana Yesu atatupe zaidi ya hivyo.
Hii inaonyesha toba ya kweli kabisa.Leo unapata watu wanaosema kuwa wameokoka na mali walizo nazo wamezipata kutokana na uasherati/uzinzi.
MUNGU anasema hivi; "Fanya toba ya kweli na ufanye malipizo ya mali ya uzinzi; sadaka ya mbwa; mshahara wa kahaba n.k.
Ulipata kazi kutokana na mitishamba; uliibia mtu mali uk
 Kwa msaada wa ushauri na maombi; Geoffrey Mwanza Wambua,
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
+254 724 656 653
geoffreymwanza@yahoo.com

Comments