TULIKUWA TUNAJADILIANA WHATSAP NA MTUMISHI WA MUNGU ALIYE RAFIKI YANGU SANA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU
TULIKUWA TUNAJADILIANA WHATSAP NA MTUMISHI WA MUNGU ALIYE RAFIKI YANGU SANA.
Jifunze kitu ndugu kupitia majadiliano yetu.

MTUMISHI: Mtumishi wa Mungu Peter Mabula, tunayo majina mbalimbali mfano mtu wa Mungu, Mtumishi wa Mungu, mwana wa Mungu nk
Je, mtumishi huyu wa Mungu anapoanguka katika dhambi, bado anaitwa mtumishi wa Mungu au mwana wa Mungu?
Kwamba maadam Mungu alituumba kwa mfano wake basi mwana wa Mungu huyu hata akitenda dhambi bado tu atakuwa mwana wa Mungu?


PETER MABULA: Mtumishi wa MUNGU akianguka dhambini anakuwa sio mtumishi wa MUNGU.
Mtumishi wa MUNGU ndio mwana wa MUNGU pia.


MTUMISHI: Je, kuna Mstari unaosema hivyo na hasa neno mwana wa Mungu

PETER MABULA: Mtumishi Ni Neno Linalotokana Na Neno "TUMIKA" Na Utatumika Kama Tu Kuna Unaowatumikia.
Mtumishi Kama Hana Anaowatumikia Huyo Sio Mtumishi. Mtumishi Wa MUNGU Ni Mtu Aliyetokana Na MUNGU Na Ametumwa Na MUNGU.
Mtumishi haanzi tu kujiita kwamba yeye ni mtumishi ila watu wakiona utumishi ndani yake na akitumika watamwita tu ''Mtumishi''
Ipo mistari hiyo ngoja nikutumie


MTUMISHI: Kuna hii hapa Uliwahi kunitumia
Mistari hii yaweza kutusaidia kujua kama wewe umeokoka ama la
Tofauti ya Mtoto wa Mungu, na mtumishi wa Mungu na mwana wa Mungu.
Mtoto wa MUNGU ni yule aliyezaliwa Mara ya pili au niseme ni yule aliyeokolewa na Bwana YESU na anaishi maisha matakatifu katika Wokovu wa KRISTO.
Yohana 1:12-13 "Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."
Watoto wa MUNGU ndio hao hao wana wa MUNGU na wanaishi maisha matakatifu katika YESU KRISTO huku wakiongozwa na kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.
Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."
Mtumishi wa MUNGU ni mtu anayeifanya kazi ya MUNGU. Mtumishi wa MUNGU ni mtu anayetoka katika kundi la watoto wa MUNGU. Mtumishi Ni Neno Linalotokana Na Neno "TUMIKA"
Mtumishi Wa MUNGU Ni Mtu Aliyetokana Na MUNGU Na Ametumwa Na MUNGU.
Mtumishi haanzi tu kujiita kwamba yeye ni mtumishi_
Ila watu wakiona utumishi ndani yake na akitumika watamwita tu ''Mtumishi''.
Hebu ona mfano wa Danieli kama mtumishi wa MUNGU.
Mfalme alimtambua Danieli kama Mtumishi wa MUNGU na alimwita kwa jina hilo la utumishi. Danieli 6:20 "Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa MUNGU aliye hai, je! MUNGU wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? ".
MUNGU alimponya mtumishi wake.
Pia Danieli katika maombi alijitaja kama mtumishi wa MUNGU, Danieli 9:17 "Basi sasa, Ee MUNGU wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya BWANA."
Mwana wa MUNGU ndio mtoto wa MUNGU. Hivyo sisi tu watoto wa MUNGU kama tu tumeokolewa na Bwana YESU.
Sisi tuliookoka ndio watoto wa MUNGU
Watu wote ni wa MUNGU lakini waliookolewa na KRISTO ni watoto wa MUNGU na wanangoja uzima wa milele.

Mistari hii huthibitisha hayo sio tu mtu anajipendelea

PETER MABULA: Amen amen sana
Mingine ni hii
1 Wathesalonike 3:2 "Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, MTUMISHI WA MUNGU katika Injili ya KRISTO, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu;"


2 Wakorintho 6:3-4 "Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi usilaumiwe;
bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama WATUMISHI WA MUNGU; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;"


MTUMISHI: Maana swali la msingi ni kuwa tunayo tayari mistari inayosema kuhusu mwana wa Mungu
Sasa huyu mwana wa Mungu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu kule kwenye Kitabu cha Mwanzo. Baadaye ametenda dhambi. Anaendelea kuitwa mwana wa Mungu?
Refer sana kuhusu mwana wa Mungu
Wewe si mwana wa Mungu... Mstari upi huo


PETER MABULA:Mimi ni mwana wa MUNGU kulingana na Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."

MTUMISHI: Sawa kabisa kuhusu mwana
Haki ya kutokuwa mwana, Mstari huo ni upi?


PETER MABULA: 2 Wakorintho 6:17-18 "Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,"

Ni lazima tutoke kwa shetani ndipo tutakuwa wana wa MUNGU.
Kama mtu yuko kwa shetani hakika huyo sio mwana wa MUNGU.

Labda ngoja tuangalia maandiko yanayowathibitisha wana wa shetani ndipo itatusaidia kubaki tukiwa Sana wa MUNGU

MTUMISHI: Amen

PETER MABULA: "Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake.-1 Yohane 3:10
Andiko hili linaweza kutusaidia kujua watoto wa MUNGU na watoto wa shetani na tofauti zao
Sijui kama nimejibu mtumishi na hii


PETER MABULA: Hii nayo ni muhimu sana, Biblia iko wazi kwamba watu wote ni viumbe wa MUNGU (Wakolosai 1:16), na kwamba MUNGU anaipenda dunia nzima (Yohana 3:16), lakini ni wale tu ambao wamezaliwa mara ya pili ndio watoto wa MUNGU (Yohana 1:12; 11:52; Warumi 8:16, 1 Yohana 3:1-10).

MTUMISHI: Amen Ngoja nami nisome some kwenye biblia tuone.
Maana saa zote tuko shambani
Na wana wa Ibilisi wako dhahiri
Nao hutafuta kila mahali pa kuwashika watu wa Mungu


PETER MABULA: Ni kweli mtumishi

MTUMISHI; Amen

PETER MABULA: Tukumbuke pia Bwana YESU aliwaambia watenda dhambi kwamba ni watoto wa Ibilisi

MTUMISHI: Ni wapi hapo Mtumishi

PETER MABULA: Yohana 8:41-44 "Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, MUNGU.
YESU akawaambia, Kama MUNGU angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa MUNGU, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.
Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu. Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo."


MTUMISHI :Amen

PETER MABULA: MUNGU akubariki sana mtumishi

MTUMISHI: Amen

MTUMISHI: Kwa kweli kazi ya Mungu ni kwa uwezo wake.


MTUMISHI: Watu ni wabishi sana


PETET MABULA:Ni kweli mtumishi

 
Tuliishia hapo.
MUNGU akubariki sana uliyejifunza kitu.
Songa mbele na Bwana YESU aliye Mwokozi.

Comments