WATAI MZURI NI SASA.

Na Mtumishi Generali Geoffrey Mwanza Wambua,
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
Bwana Yesu asifiwe?
Kwa mara nyingi kuna wakati utakuwa umetulia mahali ukiwaza jambo fulani; unaweza kuwaza kuacha kunywa pombe; unajiwa na wazo la kukuambia usiache leo; ngojea utaacha mwezi ujao.
Unaweza kuwa unahisi kuwa sasa ni wakati wako wa kutenda mambo mema; na kuyaacha maovu.Hiyo kitu inayokushuhudia kuwa wewe u mwenye dhambi na ni wakati wa kutubu na kuokoka ndiyo inayoitwa ROHOMTAKATIFU wa MUNGU.
Unaweza pia kuwa kupitia machungu unayopitia katika ndoa yako kuna wazo linakujia umwache huyo mumeo; utafute kazi na kujipangishia nyumba mwenyewe; kisha laja wazo lingine kuwa hamna haja kumwacha! Msamehe tu na uamini atabadilika.
Hilo wazo la upole na lenye kukupa faraja na matumaini huitwa ROHOMTAKATIFU na humshuhudia mtu kuacha dhambi; kusamehea; kuishi maisha matakatifu yanayompendeza MUNGU na mambo mengine mazuri.
Kuna makanisa mengi hayaamini uwepo wa ROHOMTAKATIFU huku mengine yakitumia rohomtakavitu kuwapotosha waumini wao.
Matendo 2:1 "Basi siku ya pentekoste ilipofika walikuwa wote pamoja mahali pale pale na ghafla kukatokea kutoka mbinguni kelele kama upepo wenye nguvu na unaovuma nao ukaijaza nyumba yote ambamo walikuwa wameketi.Nao wakaona ndimi kama moto; naza zikagawanyika huku na huku.
4 "Nao wote wakajazwa ROHOMTAKATIFU wakaanza kunena lugha tofauti kama vile ROHO alivyokuwa akiwawezesha"
Mtu anapookoka kisha kubatizwa anapokea ROHOMTAKATIFU ambaye humwezesha kumfundisha Neno la MUNGU; kumwongoza katika wokovu.
Mtu hawezi kuwa ameokoka na hana ROHOMTAKATIFU kwani unapotubu; kuokoka na kubatizwa unampokea ROHOMTAKATIFU wa MUNGU.
Unapopokea ROHOMTAKATIFU unaanza kunena lugha mpya; unaacha lugha za matusi; masengenyo; ulevi na kila aina ya dhambi unayofanya unaoacha kabisa bila kuirudia tena.
Unions mtu anayedai kuokoka ila anatusi; anasengenya; ana kiburi; anadaliti; anafanya uasherati; anapaka midomo rangi; anavaa mavazi yampasayo mwanamke/mwanamume; huyo hana ROHOMTAKATIFU na ina maana kuwa hajaokoka maana mtu aapookoka hatendi dhambi kikusudi.
Ndugu yangu hakikisha umejazwa ROHOMTAKATIFU ila sio rohomtakavitu ili usimtende MUNGU dhambi.
Mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele.
Muulize aliye karibu nawe kwa sasa:
"Je; ulipookoka ulimpokea ROHOMTAKATIFU ?
MUNGU wangu Yehova akubariki sana.
 KAMA HAUJAOKOKA; NIPIGIE SIMU TUOMBE PAMOJA UOKOKE SASA MAANA HAKUNA MUDA MWINGINE WA KUTUBU NA KUOKOKA. Generali Geoffrey Mwanza Wambua;
The Global Evangelism Ministries (Kenya);
+254 724 656 653;
geoffreymwanza@yahoo.com

Comments