VUNJA MADHABAHU YA SHETANI ILI UWE HURU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Maana nyingine ya dhambi ni mabaya yanayokuficha usionekane na MUNGU.
Ndugu Yangu, inawezekana  wewe ni muombaji mzuri.
  Inawezekana umeshaomba mambo mengi tu kwa MUNGU ili utendewe lakini naomba ujue hili Leo kwamba dhambi zako zinaweza kukuficha ili usionekane na MUNGU hata kupokea Baraka ulizoomba kwa MUNGU.

Madhabahu za shetani unazozitumikia zinaweza kuwa chanzo cha wewe kutenda dahambi kila leo na kwa njia hiyo maombi yako kutokujibiwa.
Ndugu, dhambi imeshakuficha Mara ngapi ili usionekane na MUNGU na kupokea Baraka zako kutoka kwa MUNGU?

Gideoni alikuwa mcha MUNGU kama wewe lakini MUNGU alipotaka kumbariki na kujidhihilisha kwake ilibidi MUNGU amwambie kwamba ahakikisha anaibomoa na kuivunja madhabahu za kipepo iliyo nyumbani kwao inayomilikiwa na Baba yake.
Waamuzi 6:25 '' Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;'

Madhabahu za kipepo ni nyingi sana na zinawaathiri watu wengi hata kama ni waombaji.
Kumbuka kuomba ni kitu kingine na utakatifu ni kitu kingine ila vinategemeana sana.
Maombi sahihi ni Yale yanayoambatana na maisha matakatifu sahihi lakini vimadhabahu vya kipepo ulivyonavyo vinaweza kuwa kizuizi cha kupokea mahitaji yako.

Ni lazima pia kubomoa na kuvunja madhabahu za kipepo ndani yako au kwenye familia yako au eneo lako.
Madhabahu za kipepo zinaharibiwa kwa.
1. Kuaharibu vitu hivyo na kujitenga navyo katika uhalisia.
2. Kuomba maombi ya kuvunja na kuharibu madhabahu hizo.

Kutambika ni madahabhu za kipepo.
roho ya uongo ni na kiburi chanzo chake inaweza kuwa ni madhabahu ya kipepo.
Pombe ni madhabahu ya kipepo.
Ziko nyingi sana madhabahu za kipepo ambazo zinaweza kuwatesa watu.

Mathayo 16:19 ''Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.''
Ukinyamaza wewe muombaji na mbingu zinanyamaza na ukitaa kalenda za kipepo na mbingu zinakataa, ukifunga wewe na mbingu zinafunga, ukifungua na mbingu zinafungua. Hivyo ukikaa kimya ukanyamaza na MUNGU naye ananyamaza.
kwanini nimesema hayo?

Silaha za nyuklia zinakatazwa ulimwenguni mwote, lakini wateule wa KRISTO tuna silaha kali katika ulimwengu wa roho kuliko silaha zote za nyuklia duniani.
Silaha zetu ni mamlaka na ni funguo za kufunga na kufungua.
  Mamlaka zetu sisi ni ;
Jina la YESU KRISTO.
Damu ya YESU KRISTO.
Nguvu za ROHO MTAKATIFU.
Neno la MUNGU.

Ndugu tumia silaha au Mamlaka  hizo na utawashinda maadui ambao hata silaha za nyuklia za kidunia haziwezi kuwadhuru.
Hakuna adui ambaye anaweza kushindana na jina la YESU akashinda.
Hakuna adui anaweza kupambana na Damu ya YESU akashinda.
Hakuna adui anaweza kushindana na nguvu za ROHO MTAKATIFU akashinda.
Hakuna adui anaweza kushindana na Neno la MUNGU.
Hizo ndizo silaha za kiroho na hizo ndizo mamlaka za kiroho na hizo ndizo funguo za kufunga na kufungua kila kitu katika ulimwengu wa roho.

Tumia mamlaka hizo kuharibu nguvu za giza kuanzia kwenye mizizi yake.
Haribu madhababu za kipepo zote ziliko kwako.
Kumbuka  ukirithi Jina Baya Lazima Na Mabaya Yakuvae.
Jina lako linaweza kubeba madhabahu ya majanga na mikosi.
Jina lako linaweza kubeba kukataliwa na kuonewa, hizo ni madhababhu ndani ya jina lako.
Jina lako linawezakubeba laana na balaa, hizo ni madhababhu ndani ya jina lako. 
Ndio Sababu Bwana YESU Alikuja Duniani Kuwasaidia Wanadamu Wanyonge Wanaoteswa Hata Na Majina Yao. 
YESU Alidhihirishwa Ili Azivunje Kazi Zote Za shetani. Mwite Naye Ataitika Na Utapona.
 1 Yohana 3:8b '' atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.''

 Wengi Walioathiriwa na madhabahu za kishetani wana tabia;
1.  Usengenyaji.
2.  Uzinzi na uasherati.
3.  Kutokuwa waaminifu.
4.  Uongo.

5.  Tamaa mbaya.
6.  Pombe.
7.  Kiburi.
8.  Kuabudu sanamu.
9.  Kumwasi MUNGU.
10. Kushirikiana na majini.

Katika madhabahu ya kishetani kuna roho Mbili;
1. Roho ya Yezebeli.
Ufunuo 2:20 '' Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.''
 
2. Roho ya uchawi na uganga wa kienyeji.

Isaya 47:12-15 ''Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto, wala moto wa kukaa karibu nao. Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.''
 
Ndugu, nakuomba leo haribu madhabahu zote zilizo katika maeneo yako.
Kwanini uombe leo?
Kuna jambo gani gumu la kushinda MUNGU?
Mwanzo 18:14A " Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?"
Biblia inajibu Luka 1:37 "kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU."
Ukijua kwamba hakuna neno la kumshinda MUNGU basi nyenyekea kwa MUNGU kwa maombi ili akukweze kwa wakati wake.
Ukijua kwa JEHOVAH anajibu maombi basi omba Leo maana yeye anaweza yote.
Kama unadhani hutaolewa/Hutaoa ni kwa sababu tu ya madhabahu za kipepo ya familia yenu iliyokushikilia au ni wewe ndio unajiumbia kutokuolewa/Kutokuoa  basi amka usingizini leo na badilisha fikra zako kwa kumtegemea MUNGU na maombi ya imani katika jina la YESU KRISTO hakika utashinda.
Ni kwa sababu tu hujaamua kuomba kwa MUNGU mweza yote.
Kama unadhani hutapona ni kwa sababu tu huamini kama YESU KRISTO anaweza kukuponya.
Kuna jambo gani gumu la kumshinda MUNGU?
Ukijua kwamba MUNGU anaweza yote omba kwake kwa jina la YESU KRISTO na utapona.
Mathayo 9:35 "Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina."
YESU aliponya magonjwa yote, hata Leo bado Bwana YESU anaponya magonjwa yote, ukiamini hakika utapona.
Walipona wote waliomwamini, hivyo na wewe mwamini na kumtegemea huku ukiishi maisha matakatifu katika yeye.
Kama wengine wanaponywa kwanini isiwe wewe?
Ndugu angalia imani yako imekwama wapi.
Angalia maombi yako kama ni sahihi.
Angalia mienendo yako kama ni sahihi.
Angalia maisha yako kama ni sahihi.

Kama kuna madhabahu ya kipepo ivunje mara moja.

 ''Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU.” 2 Wakorintho 4:3

mungu wa dunia hii[shetani] amepofusha fikra za watu wengi  ili isiwazukie nuru ya BWANA YESU ambayo ni nuru ya uzima wa milele.
Nakuomba sana tena sana usiwe miongoni mwa waliopofushwa akili na shetani.

Shetani anaweza kupofusha fkra zako kwa sababu ya madhabahu yake aliyoiwekwa kwa ukoo wenu tangu miaka mingi na wewe hujaiharibu madhabahu hiyo.
Leo vunja madhabahu zote za shetani katika maeneo yako au roho yako au ukoo  wako au familia yako.
 
MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.

0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments