WAJIBU WA MKRISTO DUNIANI NI HUU

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
Wateule wa KRISTO ni wasafiri duniani.
Ni wageni duniani.
Niwapitaji duniani.

1 Petro 2:11 '' Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.''
 
Kwa sababu hiyo nakuomba wewe Ndugu mteule  usiishi kana kwamba hapa duniani ni kwako na utakaa milele katika maisha haya.
Wenyeji wa dunia hutimiza matakwa ya dunia na ya shetani.
Wenyeji wa dunia wanadhania kwamba hakuna kuondoka.
Wenyeji wengine hudhani watabaki duniani milele.
Wenyeji wetu sisi wateule wa KRISTO ni mbinguni.

Wafilipi 3:20-21 ''Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana YESU KRISTO; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.''

Ndugu ishi kama mpitaji na msafiri na usikubali kama ndoa umefika.




            WAJIBU WA MKRISTO NI.

1. Kumwabudu MUNGU katika ROHO na kweli.

 Yohana 4:23-24 '' Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba(MUNGU) katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.''

2. Kusimama imara katika Wokovu.

 Haijalishi kuna kukatishwa tamaa au kuuziwa lakini muhimu ni kusimama imara katika YESU KRISTO na kusonga mbele katika Wokovu.
Mtume Paulo anatupa kielelezo cha kusimama imara katika Wokovu wa KRISTO ulio na faida kuu.

Wafilipi 3:7-13 ''Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya KRISTO. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua KRISTO YESU, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate KRISTO; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika KRISTO, haki ile itokayo kwa MUNGU, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na KRISTO YESU. Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; ''

Anayejua wajibu wake katika KRISTO anamsimamo.


3. Kumtumikia MUNGU katika kusudi lake.


1 Kor  4:1 ''Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU.''
Kwanini kumtumikia MUNGU?
Ni kwa sababu  kila mtu atatoa hesabu.
 Warumi 14:12 ''Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za MUNGU.''

4.Kuishi maisha matakatifu ya haki na kweli.

1 Petro 1:14-17 '' Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.'' 
 
5. Kuvumilia na kuthibitika hata mwisho.

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."



Ni lazima sana kama Kanisa la MUNGU tutimize wajibu wetu kwa MUNGU.
MUNGU anawapenda sana watoto wake walisafishwa kwa damu ya Mwanaye pekee YESU KRISTO.
MUNGU anasema
 "Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.-Mithali 8:17"
Sio neno langu
Ila nimenukuu MUNGU akisema kupitia Neno lake Biblia.

Swali. Je, unampenda MUNGU hata na wewe uwe na sifa ya kupendwa na yeye?
Ni ka tafakari kagumu kidogo lakini napenda ujue kwamba.
Kumpenda MUNGU ni;
Kutii Neno lake✔✔✔
Kutii sauti yake✔✔✔
Ni kumtumikia KRISTO katika kweli✔✔✔
Ni kuacha dhambi✔✔✔
Ni kuishi maisha ya wokovu✔✔✔
Ni kuenenda kwa ROHO✔✔✔✔
Ni kuokoka✔✔✔
Ni kumkimbia shetani na kazi zake zote✔✔✔
Ni kumtii YESU KRISTO✔✔✔✔
Kwa ufupi sana hivyo ni baadhi tu ya vigezo vinavyoweza kukuonyesha wewe kama kweli unampenda YAHWEH MUNGU wa uzima.
Lakini mwisho kabisa naomba utambue kwamba Kumpenda MUNGU haiko katika kutamka kinywani tu Bali maana halisi ya kumpenda MUNGU iko katika matendo yako.
Je, unampenda MUNGU?


Msimamo wa Kikristo ni kudumu katika yaki ya MUNGU.
Msimamo wa Kikristo ni kumfuata KRISTO na kulitii Neno lake.
Msimamo wa Kikristo ni kumcha MUNGU katika kweli yote.
Msimamo wa Kikristo ni kumtii ROHO MTAKATIFU na kuenenda katika yeye siku zote.

Wafilipi 4:4-9 "Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na MUNGU. Na amani ya MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISTO YESU. Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na MUNGU wa amani atakuwa pamoja nanyi."

 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments