KURUHUSU POMBE KANISANI NI MATOKEO YA KUONGOZWA NA VIONGOZI WENYE MAPEPO YA POMBE.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Zipo biashara za aina mbili.
1. Biashara kwa utukufu wa MUNGU.
2. Biashara kwa utukufu wa shetani.
Wewe unafanya biashara gani?
 ''Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.-Luka 6:45'' 

Nakuomba hakikisha unafanya biashara kwa utukufu wa MUNGU, yaani unambariki MUNGU na unafuata misingi ya Neno lake.
Usikubali kupitia biashara yako anatukuzwa shetani.

Pombe ni moja ya biashara za shetani na kumpa shetani utukufu.

Mithali 23:29-35  ''Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.   Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.''. 

 
-Ulevi huibua ugomvi.
-Ulevi huleta makelele yasiyo na sababu.
-Pombe imesababisha jeraha nyingi tu kwa watu.
-Moyo husema yaliyopotoka kwa sababu ya pombe.
Ndugu yangu, ukisikia fundisho la kuwataka watu kunywa pombe hilo halitokanani na MUNGU ila linatokana na shetani. na mafundisho ya mashetano ni pamoja na hayo.

Kuna kanisa linaweza kuwa na waumini wengi lakini hilo kanisa likawa na waenda mbinguni wachache sana.
Kuna kanisa linaweza likawa na waumini wachache sana lakini hilo likawa na waenda mbinguni wengi kuliko kanisa kubwa.


Wengi hujikwaa kwa sababu ya andiko hili.

1 Timotheo 5:23 " Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara."

 Ufafanuzi wa Biblia habari njema(BHN) kwenye andiko hilo la 1 Timotheo 5:23  unasema ''Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara''.


Andiko hili watu hutumia kuhalalisha kwamba kunywa kidogo ila usilewe.
Japokuwa wao ni wazima wala hawaumwi tumbo kama timotheo.
 Huo ni ufunuo Kwa timotheo binafsi Kwa ajili ya afya yake, sisi haituhusu. Watu Kwa kutokuelewa hutaka kila jambo kwenye biblia liwe lao.
Mbona watu hawa hawamuuigi yuda Kwa kujinyonga? Maana imeandikwa yuda alijinyonga.
Wamemuiga timotheo tu Kwa pombe?
Mbona kila wakimuona kipofu hawachukui matope ili kumpaka machoni kama Bwana YESU alivyofanya?
Kuna ufunuo ni kwa Mtu binafsi na sio jumuia hata wote tuige.

Kuruhusu pombe kanisani ni matokeo ya kuongozwa na viongozi wenye mapepo ya pombe.
Biblia inasema walevi yaani wanywa pombe hawana sehemu katika ufalme wa MUNGU.
1 Kor 6:9-10 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.''.

Kuna wengine hujikwaa katika andiko hili pia.
Mithali 31:6 "Mpe kileo yeye aliye karibu kupotea;"
Maana yake watu husema ni sawa kabisa kunywa pombe.
Lakini  andiko hilo Maana yake ni hii mwambie neno gumu Mtu  aliye katika kupotea ili limlevye ageuke.
Ni kama unamuona Mtu  ameshika kisu akitaka kujiua kisha wewe unamwambia ukijiua ujue mbele yako kuna ziwa la moto maana anayejiua ni sawa na anayeua hivyo funza wa ziwa la moto sasa wanashangilia maana wanakuona ukitaka kwenda huko hivyo wanajiandaa tu kukutoboa macho, maneno hayo yatamlevya na ataacha kujiua hivyo hapo utakuwa umempa kileo ili kimlevye. Neno kileo hapo limetumika kama maneno magumu sana unayoweza kumwambia Mtu aliyekaribu na kupotea. Mfano mwingine ni kama kumuambia mzinzi kwamba wiki hii ukizini unaukwaa ukimwi maana MUNGU ameniambia hivyo, yule ndugu hatazini maana umemuambia neno gumu la kumlevya ili ageuke. Biblia sehemu nyingi tu imeandikwa Kwa mifano: ukisoma Kitabu cha Ufunuo  ya  17 au 18 utaona pale kuna mama anaitwa mama Wa makahaba ambaye amezini na wafalme wote Wa dunia, sasa unaweza kujiuliza je kuna mwanamke anaweza kuzini na marais wote Wa dunia? Kumbe neno kuzini pale limetumika kama mapatano ya kipepo ili kuifanya dunia iwe chini ya mpingakristo na sio ngono kama ilivyoandikwa,
 Mtendo ya mwili yaliyo machukizo ambayo Biblia inayakataza ni pamoja ulevi. 
Waefeso 5:18 '' Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe ROHO; ''

 Hata ukitafuta tu maana ya pombe kwenye Kamusi ya kiswahili sanifu utakuta kwamba pombe ni kinywaji kinacholevya.
Kwa mantiki hiyo ni kwamba ili iwe pombe ni lazima ilevye yaani ileweshe na huo ndio ulevi na Biblia inasema hakuna uzima wa milele kwa walevi. Ndugu zangu walevi dawa ni kutubu tu na kuachana na pombe.
Maana ya ulevi ni kitu kinacholewesha na kazi hiyo ya kulewesha ni kazi ya pombe.
Ukiepuka pombe maana yake umeepuka ulevi na ukiepuka ulevi umeepuka dhambi mojawapo ambayo huwapeleka wengi kuzimu.
Wanadamu wanaweza wakaepukana na ghadhabu ya MUNGU sasa lakini wakishupaza shingo na wasiokoke sasa, wanaweza kutokuepukana na ghadhabu ya MUNGU baada ya kufa kwao.

Isaya 5:11 '' Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! ''

Usikubali kuwa wakala wa shetani kwa kudanganya watu kwamba wanywe kidogo ila wasilewe.
Wakati ukwelli ni kwamba waliokuwa wanakunywa kidogo zamani ndio walevi maarufu wa sasa.
Kipi bora watu wanywe pombe au wasinywe? Ninachokuomba kama unamiliki bar tambua kwamba shetani anakutumia kama chombo chake kiteule cha kupeleka watu jehanamu.
Kama unauza pombe au unahudumia katika vilabu vya pombe basi hakika wewe ni mteule wa shetani ili kuwapeleka watu jehanamu.

Wagalatia 5:19-21 '' Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ULEVI, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.''
 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

Comments