UKITAKA KUISHI MAISHA MAREFU DUNIANI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuna kanuni nyingi Biblia imeziainisha ili kutusaidia yatupasayo kutenda.
Kuna kanuni za baraka, kanuni za kudumu katika upendo wa ki MUNGU, Kanuni za kutembea na uwepo wa MUNGU, Kanuni za kuishi maisha marefu na kanuni nyingine nyingi sana sana.

Zaburi 90:10 "Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara."

Mimi kwa ufupi nataka tuangalie kanuni ya kuishi miaka mingi.
Kabla sijafafanua naomba pia tujue kwamba sio kila wanaoondoka katika umri mdogo wamekosea Kanuni, hilo ni angalizo maana kuna sababu nyingi pia za mtu kuondoka hata kama hajazeeka.
Kuna watu hufa kwa sababu ya kutokuomba.
Kuna watu hufa kwa sababu muda wao wa kukaa duniani unakuwa umeisha.
Kuna watu hufa kwa kurogwa na wao kushindwa kuomba vyema.
Kuna watu hufa kwa sababu ya magonjwa ambayo chanzo chake kinaweza kuwa shetani au kutokumtii kwa MUNGU.
Kuna watu hufa kwa sababu ya tamaa mbaya.
Ziko sababu nyingi za mtu kuondoka duniani lakini hivyo havifuti Kanuni ya Bibliaya kumfanya mtu aishi miaka mingi.
Lakini Biblia inaweka vizuri pia jinsi ya kuzingatia kanuni ya kukufanya uishi maisha marefu.

Ukitaka kuishi maisha marefu duniani Zingatia yanfuatayo ambayo Biblia inasema.
.
1. Waheshimu Baba yako na mama yako.

Kutoka 20:12 ''Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.''

Kuna Baba wa kimwili yaani waliokuzaa kimwili.
Kuna wazazi wa kiroho yaani waliokufundisha Neno la MUNGU ukaachana na mabaya na kuwa mteule wa MUNGU na hata sasa wanakufundisha Neno la MUNGU ili uendelee kumpendeza MUNGU.

Biblia inapozungumzia habari za kuishi muda mrefu inakupa kanuni ya kuwaheshimu Wazazi wako.
Ni ahadi ya MUNGU kwa mwanadamu anayetaka kuishi maisha marefu duniani.
Kumb 5:16 "Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako."

2. Kumcha MUNGU na kumtumikia na kutembea kwenye kusudi lake.

Mithali 7:2 '' Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.''
Kuzishika amri za MUNGU maana yake ni kutii maelekezo ya MUNGU, Ni kuitii Biblia na jambo hilo Biblia inasema ukitii maelekezo ya MUNGU utaishi.
Maana yake hata kama maadui walikupangia kufa lakini kwa wewe kutii maagizo ya MUNGU kunaweza kufuta kisho hicho bali ukaishi.
Ukimtumikia MUNGU lazima MUNGU akulinde ili uendelee kumtumikia hadi utakapomaliza kusudi la MUNGU la kuokolewa kwako.

Amosi 5:4 '' Maana BWANA awaambia hivi nyumba ya Israeli, Nitafuteni mimi, nanyi mtaishi; '
Waisraeli waliambiwa wamtafute MUNGU wataishi.
Wewe ndio mwisraeli wa leo, hivyo mtafute MUNGU utaishi.
Unaweza kumtafuta MUNGU kwa njia zifuatazo.
1 Maombi.
2. Maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
 3. Kwa matoleo safi.
4. Kumtumikia MUNGU.
5. Kumcha MUNGU kwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.
Hebu ona kile alichosemaBwana YESU katika  Luka 10:27-28 ''Akajibu akasema, Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. ''

3. Kumuomba MUNGU kwa usahihi na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.
 
Maombi yana faida nyingi na moja ya faida hizo ni kukuepusha na mitego ya mawakala wa shetani waliokusudia kifo.

Huwa kuna ofa ya miaka ya kuishi kutoka
Isaya 38:1-5 "Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, neno la BWANA likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano."


  Sio wote wanaipata ofa hiyo ya kuongezewa miaka ya kuishi.
Miaka ya kuishi kibiblia ni miaka 70 lakini MUNGU anaweza kukupa ofa ya miaka 10 ukafika miaka 80 na ukipata neema ya MUNGU unaweza kuendelea na kuendelea na ofa hiyo hadi hata miaka 120.

Moambi ni muhimu sana na ya kazi nyingi.
Kuna mtu zamani alitaka kufa kwa sababu ya kutaka kufanya uovu lakini neema ya MUNGU ikamgusa na akaambiwa amwendee mtumishi wa MUNGU amuombee na ndipo hatakufa bali ataishi.
Mwanzo 20:7 '' Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao. '' 

Kumcha MUNGU kuna faida nyingi sana.
Kuna watu wanadumu na kudumu kwa sababu ya kumcha MUNGU.
Inatupasa sana kucha MUNGU siku zote na Kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU. Warumi 8:13 '' kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. ''

 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments