USAHIHI WA MCHUMBA WAKO UNATAKIWA UTOKANE NA HAYA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Sio wote watakupenda na sio wote watakuchukia.
Waombee wale wanaokupenda na wasamehe wanaokuchukia.
Uking'ang'ana na YESU na utakatifu ipo siku waliokuchukia watajuta kukuchukia na waliokupenda watafurahi kukupenda.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Katika ulimwengu wa leo kumjua Mchumba sahihi imekuwa tatizo kubwa sana kwa baadhi ya watu.
Ni kweli kabisa kila kijana ana mpango wa kumpata Mke sahihi kutoka kwa MUNGU.
Kila Binti anataka kumpata mume mzuri sahihi kutoka kwa MUNGU.
Changamoto ni kwamba usahihi wa huyo mwenzi haotokani na muonekano wake.
Biblia inasema '' Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.-Mithali 31-10''
Kumbe kunahitajika umakini katika kumjua mke mwema na mume mwema pia.
Kumbe kunahitajika jicho la kiroho la kumtambua mke mwema au mume mwema.
Biblia inaendelea kusema '' Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.-Mithali 19:14'' 
Kumbe Mke mwema yaani mwenye Busara wewe kaka utapewa na  MUNGU.
kumbe mume mwema mwenye busara kutoka wewe Dada utapewa na MUNGU.
Agizo kuu la Biblia mkiingia kwenye ni kwamba '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu.-Waebrania 13:4 ''

Kwanini sasa imekuwa changamoto kwa wengi jinsi ya kuchagua mwenzi sahihi wa maisha yao?
Ni kwa sababu zifuatazo;
Mke/Ume mwema hatokani tu na sura yake au muonekano wake.
Mume/Mke mwema hatokani tu na kazi yake au kipato chake.
Mume/Mke mwema hatokani tu na tabasamu lake
Mume/Mke mwema hatokani tu na mwili wake
Mume/Mke mwema hatokani tu na familia anayotoka
Mume/Mke mwema hatokani tu na anavyokujali wakati wa uchumba.
Mume/Mke mwema hatokani tu na rangi ya mwili wake.
Mume/Mke mwema hatokani tu na ukoo au kabila analotoka.
Mume/Mke mwema hatokani tu na Elimu yake.
Mume/Mke mwema hatokani tu na wingi wa marafiki zake unaomuona nao.
Mume/Mke mwema hatokani tu na taifa analotoka.
 Biblia inasema  Bali mume/mke mwenye busara, mtu hupewa na MUNGU.
Na baada ya ndoa hakuna kuachana 
1 Kor 7:10-11 '' Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila BWANA; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.'' 

Je tufanyeje?
Majibu ni haya, Binti sahihi akiolewa na kijana sahihi wataingia katika ndoa sahihi.
Usahihi wa Mchumba wako unatakiwa kuletwa  na haya yafuatayo:

1.  Utakatifu katika maisha ya Wokovu wa KRISTO.
1 Petro 1:14-15 '' Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;''

Utakatifu humfanya mtu awe mwema na anayestahili.


2.   Upendo thabiti wa Ki MUNGU
Mthayo 7:12 ''Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.''

 Kama ana upendo na rohoni mwako ukawa na amani ya KRISTO ikiamua huyo anaweza kustahili.


3.  Tabia njema 

2 Petro 1:4-7 ''Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.''
Tabia njema ni tabia ya Uungu ambayo iko ndani ya wateule wa MUNGU.
Tabia njema hudhihilika kwa kukataa uasherati wakati wa uchumba na kukataa dhambi.
Tabia ya kiungu huonekana kwa kuwa watu wa maombi na watu wa haki.
 

4.  Hofu ya MUNGU.
  1 Petro 1:16-17 '' kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.''
Utakatiffu ni lama ya Mkristo yeyote.
Kila anayezingatia maisha ya utakatifu huyo ni mtu sahihi hata katika ndoa maana hofu ya hutufanya tukae mbali na maovu.

  5. MUNGU kwanza.
 Mathayo 22:37-40 ''Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.''

Kila mwanadamu lazima awe na utaratibu wa ''MUNGU kwanza''
Kumtii MUNGU kwanza.
Kulitii Neno la MUNGU.
Kujali kazi ya MUNGU kabla ya yote.
 
MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

Comments