KANUNI NNE ZA UFALME WA MUNGU KATIKA MAISHA YA MKRISTO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Ziko kanuni nyingi za ufalme wa MUNGU katika maisha ya Mkristo.
Leo nakuletea kanuni nne katika hizo nyingi.
Karibu

Kanuni Nne(4) za ufalme wa MUNGU katika maisha ya Mkristo.



1.  KUSOMA NENO LA MUNGU NA KULITAFAKARI.

Kanuni ya pili ya ufalme wa MUNGU kwa Mkristo ni kusoma Neno la MUNGU na kulitafakari.
Utamjua MUNGU na mpango wake kwa kusoma Neno lake.


''Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.-2 Timotheo 2:15''

Utamjua Mwokozi YESU kwa kulisoma Neno lake.
Neno la MUNGU ni kanuni muhimi sana kwa mteule wa KRISTO.
Uponyaji mwingine huja kwa sababu tu ya Neno la MUNGU.
Neno la MUNGU litakuongezea Imani.
Neno la MUNGU litakupa uhakika wa ushindi wako.
Neno la MUNGU hutupa nguvu za kiroho.


''Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;-1 Petro 2:2''

Utamjua ROHO MTAKATIFU kwa kujifunza Neno la MUNGU
Neno la MUNGU husaidia kuleta utulivu wa ndani.
Neno linatakasa.
Kulisoma Neno la MUNGU na kulitafakari ni kanuni ya kudumu ya ufalme wa MUNGU katika maisha ya mteule wa KRISTO.


Zaburi 119:105 "Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu."

2. MAOMBI.

Tabia ya mteule wa MUNGU ni maombi.
Ushindi hupatikana kwa maombi.
Maombi ni kanuni ya kupokea kutoka ufalme wa MUNGU.


''Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.-Yeremia 29:13 ''

  Uvuvio wa nguvu za MUNGU katika Kanisa unahitaji maombi na waombaji makini.
Maombi ni kanuni ya ufalme wa MUNGU.
Ni muhimu kuomba hadi MUNGU akubariki.
Omba hadi MUNGU akubadilishe.




''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.-1 Yohana 5:14-15''

 Katika Kanisa kunahitajika sana maombi sana.
Jambo la kujua ni kwamba ni watu waliobadilishwa na maombi tu ndio wataleta mabadiliko katika Kanisa la MUNGU.
Ukitaka kuleta mabadiliko katika Kanisa lenu basi hakikisha unakuwa muombaji sana.
Omba maombi katika ROHO MTAKATIFU na omba hata maombi ya kufunga.


1 Wathesalonike 5:17 "ombeni bila kukoma;"


Usipokuwa muombaji basi unakuwa unapishana na kanuni muhimi sana ya ufalme wa MUNGU katika maisha ya Mkristo.


2. KUMTUMIKIA KRISTO.

Kama umeamua kumchagua KRISTO kama Mwokozi wako inakupasa pia kumtumikia.

Marko 16:15-16 ''Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.'' 

Tunamtumikia MUNGU kwa kumwabudu katika Roho na kweli.
Tunamtumikia MUNGU kwa kuipeleka injili yake mbele.
Kuna jinsi nyingi za kumtumikia MUNGU
Kumtumikia MUNGU ni kanuni ya ufalme wa MUNGU.
Fanya kazi ya MUNGU kwa nguvu zote.
Usikubali kufanya kazi ya MUNGU kwa ulegevu.
Usikubali kufanya kazi ya MUNGU kwa madaha, kujiona na kujionyesha.



2 Kor 15:58 '' Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.''

Ndugu Fanya kazi ya Injili kwa nguvu na kwa moyo wa upendo.

Kazi ya MUNGU inahitaji utayari,uhodari, ujasiri na unyenyekevu mkubwa sana kwa MUNGU.
Hapo ndipo utatimiza kusudi la kuitwa kwako katika Wokovu wa Bwana YESU Mwokozi.



3. TEMBEA KATIKA NGUVU ZA MUNGU.

Kutembea katika nguvu za MUNGU ni kanuni muhimu sana ya ufalme wa MUNGU kwa mkristo.
Kama unataka kuwa katika ufalme wa MUNGU kwa kusudi la MUNGU basi tembea katika nguvu za MUNGU.
Ngoja mitume walivyotembea katika nguvu za MUNGU.


Matendo 4:13-21 " Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na YESU. Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao, wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili. Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la YESU. Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za MUNGU kuwasikiliza ninyi kuliko MUNGU, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza MUNGU kwa hayo yaliyotendeka;"


Matendi ya muujiza inayotokana na maombi ni kanuni ya ufalme wa MUNGU kwa Mkristo.
Mamlaka ya maombi tumepewa wateule wa KRISTO wote maana hiyo ni kanuni ya ufalme wa MUNGU kwetu.


Marko 16:17-18 ''Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. ''

 Huhitaji elimu ya darasani ndipo utembee katika nguvu za MUNGU.
Kumbuka masomo ya kidunia yanaweza kukupa maarifa lakini ROHO MTAKATIFU anatupa ufunuo wa kutembea kwa nguvu za MUNGU.
Utatembea katika nguvu za MUNGU ukiwa tu na ROHO MTAKATIFU.
Unapookoka MUNGU hukupa nguvu hivyo tembea katika nguvu za MUNGU.
Nguvu za MUNGU zina ROHO MTAKATIFU.

Ukizingatia kanuni hazi tatu yaani maombi, kulisoma Neno la MUNGU na kutembea katika nguvu za ROHO MTAKATIFU hakika utakuwa na MUNGU daima.

 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

Comments