MJUE MUNGU UNAYEMTUMIKIA.


Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu unayefuatilia masomo yangu. Karibu sana tujifunze Ujumbe mwingine muhimu sana.
Leo tunajifunza Kumjua MUNGU.
Watu wengi hawamjui MUNGU.
Hata wakristo wengi hawamjui MUNGU wanayemtumikia.
Kuna baadhi ya watumishi hawamjui MUNGU wanayemtumikia.


Ayubu 22:21-22 " Mjue sana MUNGU, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako."

Neno hilo "Mjue sana MUNGU" kwenye tafasiri zingine za Biblia limetafasiriwa kwamba "Kubaliana kwa kila kitu na MUNGU" ndipo mema kutoka kwa MUNGU yatakujia.
Jambo la kwanza ambalo ni muhimu sana kwa mtu yeyote anayempokea YESU kama Mwokozi wake ni kumjua MUNGU anayemtumikia na kumwabudu.

Ndugu yangu naomba uzingatie haya katika kumjua JEHOVAH MUNGU wako.

1. Mjue MUNGU ni nani kwako.

Ukimjua MUNGU ni nani kwako hakika ndipo utapata amani na mema ya MUNGU yatakujia.


Mfano Zaburi 68:20 inasema "MUNGU kwetu sisi ni MUNGU wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana."


Njia za kutoka mautini yaani njia za kutoka kwenye uharibifu zina MUNGU.
Hivyo kama ni mtu wa kanisa unaumwa na unaamua kwenda kwa mganga jambo la kwanza kwako ni kwamba haumjui MUNGU hata kidogo.
Kuna watu kwa sababu hawamjui MUNGU basi wamemwekea mipaka.
Unakuta kuna mtu akipatwa na matatizo ndipo humwitaji MUNGU na kunyenyekea kwake, lakini wakati wa raha na amani hamhitaji MUNGU wala kumtegemea, huyo ndugu hamjui MUNGU.
Biblia inasema mjue sana MUNGU ndio mema sahihi yatakujia.
Kupata kazi isiwe sababu ya kuacha ibada.
Kuolewa au kuoa isiwe sababu ya kuacha Huduma kanisani.
Wasio mjua MUNGU tu ndio wanaweza wakaacha ibada na na Huduma lakini wamjuao MUNGU wao hakika hata wakati wa Baraka
Kwao MUNGU ni MUNGU tu na ni tegemeo milele.
Ukitaka MUNGU akuponye malaria tu atakuponya lakini ukitaka MUNGU akuponye ukimwi hakika atakuponya, inategemea unamjuaje MUNGU na kanuni zake.


2. Mjue MUNGU anataka nini.

Wengi sana hujichanganya na kufanya machukizo kwa MUNGU na kanisani wapo, hao tatizo lao hawamjui MUNGU kwamba anataka nini kwao.


Kumb 10:12 "Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;"


Ni rahisi tu, kumjua MUNGU hakupo katika kutamka tu Bali kupo katika kutenda maagizo yake.
Anayemjua MUNGU ni lazima ajue kutenda tu yasiyomchukiza MUNGU, yaani ajue kutenda mema.


3. Mjue MUNGU anahitaji ufanyeje.

A. MUNGU anahitaji uokoke.


Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."


B. MUNGU anahitaji uishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO.

1 Petro 1:15-16 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."


C. MUNGU anahitaji umwabudu katika Roho na kweli.

Yohana 4:24 "MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."


D. MUNGU anataka umtumikie kwa kuipeleka injili yake mbele.

1 Wakorintho 15:58 " Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

4. Mjue MUNGU na njia yake ya wokovu.

Njia ya wokovu ya MUNGU ni YESU KRISTO.


Matendo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."


Njia hiyo ni moja tu na nje na hiyo hakuna uzima wa milele.
Ukiona Mkristo anamwacha YESU na kufuata dini nyingine ambazo moja kwa moja ni dini za shetani hakika huyo mtu hakuwa anamjua MUNGU wake na hakuwa anajua njia ya MUNGU ya wokovu wa milele.
Kuna watu anapata mchumba wa dini nyingine ambayo ni ya shetani kabisa na huyo ndugu anamwacha YESU ili apate mke au mume, huyo ndugu anajiangamiza mwenyewe na huyo ndugu tangu mwanzo hakuwa anamjua MUNGU hakika.
Ndugu mjue sana MUNGU ndipo mema yatakujia.
Mema ya kwanza ni uzima wa milele.
Mema mengine ni ushindi dhidi ya nguvu za Giza na kila majini yaliyotumwa na shetani.
Wamjuao MUNGU wao wanaishindania Imani ya uzima maana iko moja tu yaani Wokovu wa Bwana YESU.


Yuda 1:3 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."

5. Mjue MUNGU na njia zake za Baraka, ulinzi, uokoaji na uponyaji.

Chanzo cha kila baraka na kila kitu cha ki MUNGU ni maombi katika ROHO MTAKATIFU.
Maombi ni ufunguo wa kufungua kila kitu.
Kama una tatizo tambua kwamba unatakiwa kuomba kwa MUNGU ili tatizo liishe.
Usiseme tu "MUNGU yupo na ananiona" wakati unatakiwa umwite ndipo utapona.
Maombi ni lazima sana yaambatane na utakatifu na yawe maombi ya Imani.


Waebrania 11:6 " Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."

Ni muhimu kujua kanuni ya kupokea kila baraka uitakayo kutoka kwa MUNGU.
Mfano kuna baraka zitakuja kwa sababu wewe unazingatia kanuni ya MUNGU ya kutoa sadaka na fungu la kumi kwa uaminifu.
Kuna wakati utapona kwenye mitego ya kipepo kwa sababu wewe unamtikia MUNGU, hiyo ni kanuni muhimu sana.
Sasa katika kutaka kujua kila kanuni ya MUNGU ya kukupatia baraka Fulani ni lazima sana ulisome sana neno la MUNGU na kulitafakari.
Neno la MUNGU ni kitu muhimu sana ambacho MUNGU anataka ukizingatie katika maisha yako.
Ndugu mjue sana MUNGU ndipo utakuwa mteule wake sahihi.
Mjue sana MUNGU ndipo hutakuwa mtu wa kuangukaanguka dhambini.
Mjue sana MUNGU ndipo hutaweza kumwogopa shetani na mawakala zake.
Mjue sana MUNGU na matendo yake ndipo utakuwa na uhakika wa ushindi kila siku.
Mjue MUNGU katika nyakati zote unazopitia.
Ni muhimu sana kumjua MUNGU.
Mjue Bwana YESU na mpango wake kwako.
Mjue ROHO MTAKATIFU na maongozi yake kwako.


Danieli 11:32 "Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao MUNGU wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu."


MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

Comments