SABABU ZA YESU KRISTO KUJA DUNIANI MARA YA KWANZA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Moja ya masomo muhimu sana kila mwanadamu kujua ni sababu za kwanini Bwana YESU alikuja duniani miaka 2000 iliyopita na kwanini atakuja tena siku ya mwisho.
Leo sizungumzii Sababu za Bwana YESU kuja duniani mara ya pili ila nazungumzia sababu za ujio wa kwanza uliotengeneza Wokovu kwa waliomtii kwa kumpokea kama Mwokozi na kisha kuishi maisha matakatifu ya wokovu wake.
Nimekuandalia sababu hizo 7 za kwanini Bwana YESU alikuja duniani mara ya kwanza.
Sio kwamba ni sababu hizi tu bali mimi naamini zipo zaidi ya Ishirini ila leo zijue hizi na mtii itakusaidia.


Sababu 7 kwanini Bwana YESU alikuja duniani mara ya kwanza.

1. Kutuhamisha sisi kutoka ufalme wa shetani na kutupeleka sasa ufalme wa MUNGU baada ya sisi kumpokea kama Mwokozi wetu.

1 Yohana 3:8b ''Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi ''


Biblia inaendelea kujulisha ni kwa jinsi gani tunahamishwa kutoka utawala wa shetani na sasa tunakuwa chini ya MUNGU Muumba wetu.

Wakolosai 1:13-15 ''Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa MUNGU asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. ''

2. Kutuondolea vifungo vyote vya giza kwa maombi yetu kupitia jina lake.

Mathayo 9:35 '' Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.''


Biblia inaendelea kujulisha kanuni ya kupokea uponyaji kwamba tuombe kupitia jina lake Bwana YESU hakika tutapona.

Yohana 14:13-14 '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.''

 
Nimewahi kuombea watu wengi sana kupitia jina la YESU KRISTO na hakika MUNGU BABA aliwaponya wengi mno mno. Na hata sasa kupitia jina la YESU KRISTO anaendelea kuponya na kufungua wengi sana kutoka vifungo vyote vya giza.
Ni raha mno kuwa katika Bwana YESU na kuishi maisha matakatifu na maombi katika yeye.


3. Ili sisi tuliomtii tuende uzima wa milele.

Yohana 3:16-18 ''6 Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. ''


Hata sasa baada ya kuondoka duniani ameenda kutuandalia makazi ya milele, ili siku akija atatuchukua kwenda kwenye makazi hayo ya milele ya uzima wa milele.

Yohana 14:1-3 ''Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi. Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.''

4. Ili sisi tuliomtii tuwe watoto wa MUNGU wenye haki zote mbele za MUNGU.

Yohana 1:12-13 ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ''


Tunapata haki nyingi sana tukifanyika watoto wa MUNGU kupitia Bwana YESU.
Hii ni moja ya haki tunayoipata kwa sababu ya kuokoka na kuishi maisha mataktifu na maombi.


Isaya 54:17 '' Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.''


5. Ili tuwe na mamlaka katika ulimwengu wa roho kupitia jina lake na damu yake.

Luka 10:19 '' Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.''

 
Hakuna yeyote anayetumika kishetani anaweza kutushinda nguvu kupitia maombi yetu katika jina la YESU KRISTO maana tumepewa mamlaka.


Mathayo 16:19 '' Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.''


Tuna sana katika ulimwengu wa roho tukiwa na KRISTO.
YESU alitupa mamlaka ya kumiliki na kutawala.


6. Ili ROHO MTAKATIFU aje kwetu na kufanya makazi kwetu na kutusaidia katika yote.

Yohana 14:26 '' Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. ''

 
ROHO MTAKATIFU ndiye sasa anayetusimamia sisi kama kanisa la MUNGU duniani.
Mteule halisi kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU na kumtii yeye siku zote.


Warumi 8:14-16 ''Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, BABA. ROHO mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa MUNGU; ''


7. Ili kutufanya tusamehewe dhambi zetu zote kwa kupitia toba katika yeye.

Isaya 43:25 ''Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.''

Ukimpokea YESU na kutubu dhambi zako hakika unasamehewa na jina lako linaandikwa kwenye kitabu cha uzima.

''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.-1 Yohana 1:9

Kwa maamuzi ya kumpokea Bwana YESU kama Mwokozi hakika MUNGU husamehe dahmbi haraka na kutuhesabia haki

''Kwa maana Wewe, BWANA, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. -Zaburi 86:5

Muhimu tu ni kutubu toba ya kweli na kusonga mbele katika utakatifu na kujifunza Neno la MUNGU na maombi.
Unaposamehewa pia kumbuka na wewe kuwasamhe wote waliokukosea na achilia hakika utaitwa heri.


''mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama BWANA alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.- Wakolosai 3:13

Ni heri mwanadamu yule anayemtii Bwana YESU.
MUNGU akubariki sana kama unamtii Bwana YESU mwenye uzima wa milele.
MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

Comments