FAIDA TANO(5)ZA MAOMBI YA KUKESHA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU


Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo tunajifunza kuhusu maombi ya kukesha au kwa jina lingine maombi ya muda mrefu ukiomba mfululizo.
Maombi ya kukesha ndio maombi ya muda mrefu.
Maombi ya kukesha huanza na kuomba saa moja nzima na kuendelea.
Mathayo 26:40 "Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?"

Maombi ya muda mrefu ni muhimu sana.

Faida  za maombi ya kukesha ni hizi;

1. Yatakusaidia ili usiingie majaribuni.

Mathayo 26:40-41 ''
Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.''
Maombi ya muda mrefu yana maana nyingi sana.
Muda huo utautumia kwa MUNGU na sio katika mengine.
Katika maombi utapata ufunuo na utatiisha mwili N.k
 Majaribu mengi sana unaweza ukayafuta kupitia maombi yako ya muda mrefu.
Jiulize kwa saa moja nzima utakuwa umeombea mambo mangapi? Hakika ni Mengi, na kama unaenenda kwa ROHO MTAKATIFU hakika utakuwa umefuta vitu vingi vibaya ambayo ilikuwa vije kwako, lakini kwa maombi yako vinafutika.
 Marko 14:38 ''Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu. ''

Maombi ya muda mrefu yanakupa mlango wa kutokea katika Majaribu, Hivyo ni muhimu sana kuomba maombi ya kukesha.

2. Yana uwezo wa kukufungua kutoka kwenye vifungo vilivyokufunga na kukuweka huru.
Matendo 16:24-33 ''
Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba MUNGU na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Wakamwambia neno la BWANA, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.''
Akina Mtume Paulo na sila walikamatwa lakini huko huko gerezani waliomba maombi ya kukesha na MUNGU akawatoa katika kifungo hicho.
Hata wewe unaweza ukatoka katika vifungo mbalimbali kupitia maombi yako ya kukesha.

Maombi ya kukesha yana uwezo wa kukuokoa na taratibu mbaya zilizowekwa na maadui zako za kukuangamiza, kama yalivyomuokoa Danieli pia.
Danieli 6:5-10 '' Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danielii huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya MUNGU wake. Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.  Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.  Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za MUNGU wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.''

3. Yanakufanya utu wako wa ndani kufanywa upya kila siku.
2 Kor 4:16-17 ''
Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; ''
 Sehemu mojawapo kubwa kabisa ya kuufanya utu wa ndani ya mtu ufanyike upya kila siku ni maombi.
Maombi ya kukesha ni muhimu zaidi katika kuufanya utu wako wa ndani uwe mpya kila siku.
 
4. Yana uwezo wa kujenga mahali palipobomoka na kuwafanya maadui zako wakuogope.
Nehemia 1:3-5,11 ''
Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto. Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni; nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake; Ee BWANA, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nalikuwa mnyweshaji wa mfalme). ''
 Nehemia baada ya kusikia jinsi ambavyo Mji wa Yerusalemu ulivyoharibika aliingia kwenye maombi na majibu sahihi yakatoka na akaenda kuujenga tena mji wa Yerusalemu.
 Nehemia 6:16 '' Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na MUNGU wetu.''

5. Yanakupa kujua kupambanua sauti ya MUNGU na sauti ya shetani.
Matendo 16:16-18 ''
Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la YESU KRISTO, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.''
Maombi ya kudumu  yalimsaidia mtume Paulo kupambanua roho iliyokuwa ndani ya huyo kijakazai japokuwa huyo kijakazi aliwasifia sana akina Paulo.
Maombi ya kukesha ni muhimu sana katika maisha yetu wateule wa Bwana YESU.
 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu


Comments