![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Katika Biblia kuna watu walifundisha Neno la MUNGU na katika mafundisho yao kuna watu waliamua kuokoka hivyo hao Watumishi wakawa Wazazi wa kuwafundisha kiroho hao ambao ndio wameokoka.
Mfano ni huu.
1 Timotheo 1:2 "kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa MUNGU Baba na kwa KRISTO YESU Bwana wetu."
◼️Paulo alikuwa mzazi wa kiroho wa Timotheo hivyo iko kwa jinsi hiyo.
◼️Kazi ya Baba wa kiroho ni kuwalea kwa mafundisho ya Neno la MUNGU ndipo walikuwa ni kama mzazi na mtoto wake, maana mzazi alihakikisha mtoto wake anakula vizuri Neno la MUNGU na kulifanyia kazi maishani mwake.
➡️Paulo anamfundisha mwanaye mambo ya MUNGU safi na kumwimalisha.
2 Timotheo 2:1 "Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika KRISTO YESU."
◼️Kwa njia hiyo wengi walizaliwa kiroho kupitia Injili na hivyo waliowazaa yaani waliowafundisha wanaendelea kuwafundisha hadi wakue kiroho.
Hivyo ndio maana halisi ya wazazi wa kiroho.
➡️Mfano Mwinjilisti Marko alikuwa Mtoto wa kiroho wa Petro.
1 Petro 5:12-13 " Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya MUNGU. Simameni imara katika hiyo. Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu."
◼️Lakini lazima wazazi wa kiroho wawe ni wanaohubiri kweli ya KRISTO na sio mafundisho ya uongo.
◼️Kama Kuna Mtumishi amekufundisha uongo huyo sio Baba wa kiroho Bali ni Nabii wa uongo aliyetumwa na shetani kupoteza watu.
Mfano Mtu anayekataza watu kuokoka huyo asiwe kamwe baba Yako wa kiroho, huyo ni Mtu mwovu na Mtu mwovu hauwezi kuzaa matunda mema.
Mathayo 7:18 "Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri."
◼️Baba wa kiroho katika KRISTO wapo na ni wa Muhimu kwa ustawi wa Watoto wao wa kiroho.
Je Wewe Baba Yako wa kiroho ni nani?
Je unafuata ushauri mzuri wa kiroho wa Baba Yako wa kiroho?
Mimi Peter Mabula Baba yangu wa kiroho Wala hajawahi kuniita "Mwanangu wa kiroho" lakini ushauri wake natembea nao Maisha yangu yote.
Baba yangu wa kiroho alinishauri mambo mengi sana ila haya matano natembea nayo siku zote.
1. Katika ushauri wote ushauri mkuu ni wa ROHO MTAKATIFU, ufuate huo daima.
2. Hata katika dhoruba Simama imara na Bwana YESU KRISTO.
3. Mhubiri YESU KRISTO bila kuathiriwa na mazingira yeyote.
4. Kataa kiburi na kujiinua utainuliwa sana na MUNGU baadae.
5. Mtumikie Bwana YESU KRISTO bila kuchoka.
Mambo hayo natembea nayo daima, vipi kwa upande wako Ndugu, Je unafuata ushauri mzuri wa Baba Yako wa kiroho aliyesimama katika kweli ya KRISTO?
Baba wa kiroho ni wa Muhimu sana kama ni Mtumishi sahihi katika KRISTO YESU.
Tito 1:4 "kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa MUNGU Baba na kwa KRISTO YESU Mwokozi wetu."
➡️Lakini pia kuna watu huchukulia kuwa Baba wa kiroho ni cheo, hiyo sio kibiblia.
➡️Kuna watu huchukulia Baba wa kiroho kuwa ni karama au madaraka, hiyo sio kibiblia.
◼️Baba wa kiroho na mama wa kiroho ni wale wanaokufundisha Neno la MUNGU hata ukamjua KRISTO, ukaacha dhambi ni Wewe kufanyika Mtumishi mwaminifu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
➡️Lakini sio cheo wala madaraka kuwa mzazi wa kiroho.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments