PIGA MAGOTI KWENYE NENO LA MUNGU ILI USHINDE.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
Moja ya kitu muhimu sana katika maisha ya mteule wa MUNGU ni Neno la MUNGU.
Mtu Anaweza Kuomba Kwa Masaa Mengi Kama Tu Atakuwa Amepiga Magoti Juu Ya Neno La MUNGU. 
Kupiga Magoti Hapa Nina Maana Ya Kuweka Maombi Juu Ya msingi uitwao Neno La MUNGU. 
Yaani Unaomba Kwa Kulitumia Neno La MUNGU.
 Neno Li Hai Na Halitapita Daima

Waebrania 4:12 ''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. '

Ndugu Hakikisha Unapigana Vita Kwa Maombi ukitumia Neno la MUNGU.
 1. Dai Haki Zako Kwa Neno la MUNGU.
 2. Mshinde shetani Kwa Neno la MUNGU kwa njia ya maombi.
 3. Pokea Neema Ya MUNGU Kwa Neno la MUNGU kwa kulitii siku zote.
4.  Vunja Vifungo  vya giza Kwa Kutumia Neno la MUNGU kwa maombi. 
5.  Shinda Majaribu Kwa Kutumia Neno kwa maombi na kulitii Neno.

 Neno La MUNGU Ni Muhimu Sana.
Hakikisha unakuwa Mtu wa  kulisoma Neno, kulitafakari, kulitii Na kulitumia Neno La MUNGU. 

Vyote Vitapita Lakini Neno Halitapita.
Luka 21:33 ''Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. ''

Ufanye nini juu ya Neno la MUNGU?
 
1.  Liweke Neno la MUNGU  Mioyoni Mwako Ili ushinde Dhambi Na umshinde shetani.
Zaburi 119:11 '' Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. ''

 2. Kubali Kuongozwa Na Neno La MUNGU ili usiingie maovuni.
Zaburi 119:105 ''Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. ''

 3. Tambua pia kwamba Neno La MUNGU Husimamiwa Na ROHO MTAKATIFU Hivyo Kumtii ROHO MTAKATIFU Ni Kutii Kusudi La MUNGU.
Usipomhitaji ROHO MTAKATIFU katika maisha yako huwezi kulijua Neno la MUNGU kwa usahihi autakao MUNGU.
ROHO MTAKATIFU pekee ndio analijua Neno la MUNGU maana yeye ndio mwandishi wa Neno la MUNGU na ndiye alilileta Neno la MUNGU kwetu.
2 Petro 1:21 '' Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. ''

4. Neno La MUNGU Lina Pumzi Ya MUNGU Hivyo Ni Lazima Neno Liwe Karibu Yetu
 2 Timotheo 3:16-17 ''Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.''

Wanaolikataa Neno la MUNGU hupotea.
Neno la MUNGU ndilo Neno la KRISTO ukilikataa hilo hakika utapotea.
Neno Ni Muhimu Sana, Wanaopotea Ni Kwa Sababu Hawajui Neno Na Uweza.
Mathayo 22:29 '' YESU akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa MUNGU. ''

 Ndugu naomba utambue kwamba Waliopo Duniani Ni Wengi Lakini Walioondoka Ni Wengi Zaidi. 
Waliopo Wanaweza Kuamua Vyema Leo Ili Siku Wakiondoka Waende Uzima Wa Milele. 
Maamuzi Sahihi Ni Pekee Kuokoka Na Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu. 
Bwana YESU Anakuita Leo Ndugu Ambaye Hujaokoka Ili Uokoke.
Kumbuka ndugu '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.-Yohana 3:16-21

Ndugu hakikisha wewe unakuwa mmoja wa wanaompokea YESU KRISTO na kutubu na kuacha uovu.
Mara nyingi sana MUNGU amelituma Neno lake kwako ili likusaidie na kukutoa katika maangamizo, lakini sijui kama huwa unalipokea Neno la MUNGU na kulitii.
Zaburi 107:20 '' Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. '' 
Kumbuka pia MUNGU akilituma Neno huwa Neno hilo linampelekea ripoti MUNGU na huwa linatimiza kusudi la MUNGU.
Je Neno la MUNGU la wokovu ambalo hutumwa kwako kila mara huwa unalifanyia kazi? Je Neno hilo lipeleke ripoti kwa MUNGU kwamba umelipokea au umelikataa?
Ndugu hakikisha unafanyia kazi Neno la MUNGU la injili ya KRISTO YESU iokoayo.
Isaya 55:6-11 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. ''

Ndugu litiii Neno la KRISTO linalotumwa kwako na lifanyie kazi Neno hilo katika maisha yako.
 MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments