KWANINI IMANI ITOFAUTIANE KATI YA MTEULE NA MTEULE?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuwa mteule wa MUNGU haiishii tu kwenye kumpokea YESU KRISTO, Bali hatua za baada ya kumpokea YESU ni za muhimu sana ili kukuthibitisha kwamba hakika u mteule wa MUNGU.
Hatua za kukuthibitisha kwamba u mteule wa MUNGU ni nyingi, chache katika hizo ni hizi;
1. Kumtii MUNGU katika mambo yote.
Yakobo 4:8-10 ''Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza.'' 
 
2. Kuenenda katika ROHO MTAKATIFU.
Wagalatia 5:16-18 ''Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na ROHO kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na ROHO, hampo chini ya sheria.''
 
3. Kujitenga mbali na kila dhambi za zamani yaani dhambi za kabla hujaokoka.
Zaburi 34:14 ''Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.'' 

4. Kuendelea mbele katika imani ya Wokovu wa Bwana YESU.
Wakolosai 2:6-7 ''Basi kama mlivyompokea KRISTO YESU, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;  wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. ''
 
5. Kumtumikia Bwana YESU.
1 Kor 15:58 ''Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA. ''

Kuna tofauti kati ya mwanafunzi na Mwamini.
Kuna tofauti hakika kati ya Mwanafunzi wa kiroho na Mwamini.
Mwanafunzi ana malengo ya kufikia kuwa mtu fulani, mwamini hubaki kuamini tu.
wanafunzi wa kiroho wote hutoka katika kundi la waamini maana wote walimwamini YESU na kumpokea YESU kama Mwokozi. 

Hapa ndipo imani ya kumwamini MUNGU hutofautiana baina ya Mteule na mwingine.
Mwanafunzi huwa haishii tu kwenye kuwa mwamini Bali hujipambanua kwamba yeye ni Mwanafunzi wa YESU aayejifunza sana ili ajue mambo mengi ya ki MUNGU na ili baadae akiwa katika nafasi Fulani kiutumishi basi atende vyema na vizuri.
Sijui kama umenielewa ndugu ila lengo langu usiishie tu kwenye kuamini Bali jifunze Biblia na uwe muombaji na Fanya kila jambo la ki MUNGU ambalo waliofanikiwa kiroho walifanya.
Wapo watu ili afunge na kuomba ni hadi tangazo litoke madhabahuni ndipo atakufunga.

Imani inatofautiana baina ya mtu na mtu kwa sababu ya:
1.Uelewa na uzingatiaji wa Neno la MUNGU.

 1 Petro 2:2 ''Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;''

2. Imani huwa ina macho ya kuona hivyo ili Imani yako iwe kubwa ni lazima uipalilie Imani hiyo.
2 Kor 5:7 ''Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. ''
Unaipalilia kwa maombi ya Mara kwa Mara, kujitakasa, kusoma neno la kulihamishia katika matendo.


3. Kumtumikia MUNGU.
1 Kor 4:1 ''Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU.''
 
Hayo ndiyo yanaweza kutofautisha Imani baina ya mtu na mtu.
Kumbuka Imani chanzo chake ni kusikia, hivyo kumbe unavyovisikia Mara kwa Mara vinaweza kujenga Imani.
Je kama husikii neno la MUNGU Mara kwa Mara Imani yako itajengwa katika nini?
Je Imani hiyo itakuwezesha kuomba kwa MUNGU kwa imani na kupokea?
Jibu ni hapana.
Kumbe tunajifunza kwamba kuna watu wanaongezeka viwango vya imani na kuna wengine hawaongezeki kiimani, tofauti ndio hiyo


Watu wengi hawawazi yaliyo ya MUNGU Bali huwaza yaliyo ya dunia.
Wakati mwingine mambo ya dunia hupindisha fahamu za watu.
1 Yohana 2:15 " Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba(MUNGU) hakumo ndani yake."

Ndugu hakikisha unatumia muda wako kuwaza yaliyo ya MUNGU ndipo utafanikiwa.
Mithali 3:5-6 " Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako."

Ni muhimu sana kuwaza yaliyo ya MUNGU maana tuko kipindi za uongo mwingi.
Hata akili zako tu usizitegemee Bali mtegemee MUNGU na waza yaliyo ya MUNGU.
Usiwaze mabaya ya dunia Bali waza mema.
Waza yaliyo ya MUNGU na sio ya dunia.
Isaya 55:8 "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA."

Kuwaza yaliyo ya MUNGU ni;-
1. Kuwaza Neno la MUNGU na na kisha kuanza kulitii.

2. Kuwaza maombi na kisha kuamua kuwa mtu wa maombi.
3. Kuwaza ibada na kisha kuamua kuwa mhudhuliaji wa ibada.
4. Kuwaza njia za MUNGU za kufanikiwa kwako.
5. Kuwaza Wokovu wa KRISTO na kisha kuchukua hatua za kuyaishi maisha ya Wokovu.
6. Kumtafakari Bwana YESU na kazi zake kwenye maisha yako.
7. Kumuwaza ROHO MTAKATIFU na kwa jinsi gani umtii daima ili umpendeze MUNGU.
Mambo hayo ndio yanaweza kuwatofautisha wateule katika ukuaji wao wa kiroho.
 Waefeso 5:15-17 "Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA."

Umepewa nafasi ya kuomba lakini wewe huombi, vikija vifungo vya kipepo utalalamika?
Umepewa nafasi ya kumtumikia Bwana YESU lakini hutumiki, nafasi hiyo ikiondolewa kwako hakika utatumia nguvu nyingi sana kuitafuta nafasi hiyo.
Umepewa nafasi ya kushuhudia injili, hujashuhudia na watu uliotakiwa kuwafikia kwa injili yako wameondoka duniani. Je utapata furaha gani?
Ndugu yangu nakuomba itumie vyema nafasi aliyokupa MUNGU katika kazi ya injili ya KRISTO YESU Mwokozi.

Unalihitaji sana Neno la MUNGU ili ukue kiroho na ili imani yako iongezeke.
MUNGU amekuletea waalimu wengi tu ili wakupe maarifa ya MUNGU yatakayoinua imani yako hivyo inakupasa kuzingatia fundisho la Neno la MUNGU.
Katika injili ya KRISTO kuna Walimu wengi wa Neno la MUNGU.
Kuna Walimu wapole, kuna Walimu wakali.
Kuna Walimu wenye hekima sana na kuna Walimu wa Neno wanaojua zaidi kufundisha masomo Fulani Fulani.
Kuna ambao wako vizuri sana katika kufundisha maombi, wengine Siku za Mwisho, wengine Utoaji n.k lakini vitu viwili tu ambavyo kila Mwalimu wa Neno la MUNGU amepewa kufundisha ni Utakatifu na Wokovu.
Kila Mwalimu wa Neno la MUNGU ni muhimu sana.
Ndugu usichague Mwalimu wa kukufundisha Neno la MUNGU labda tu wale walimu wa uongo ambao wanafundisha kinyume na Biblia.
Lakini kama yuko Mwalimu wa Neno la MUNGU na anafundisha kwa usahihi na kusudi la MUNGU huyo Mwalimu ruhusu moyo wako akufundishe Neno la MUNGU.
Haijalishi ni Mwalimu mkali au huwa anakemea sana. Haijalishi ni Mwalimu wa Neno anayesisitiza jambo lilelile moja siku zote.

Na Mwalimu ninayemzungumza Mimi sio lazima aitwe Mwalimu Bali ni kila anayefundisha Neno la MUNGU, haijalishi ni mchungaji au Mwinjilisti au Nabii au Mtume, au kiongozi Kanisani.
Kama anafundisha Neno la kweli la MUNGU basi msikilize na fanyia kazi Neno la MUNGU.

Kumbuka Tabia ya mteule wa MUNGU aliyeokolewa na Bwana YESU huwa inathibitishwa na mambo wawili.
1. Matendo yake.
 1 Petro 2:11-12 ''Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze MUNGU siku ya kujiliwa.''
 
2. Maneno ya kinywa chake.
 Wakolosai  3:9-10 '' Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.''
 
Mteule wa MUNGU ni lazima hayo mawili yakuthibitishe.
Wakristo wengi vinywa vyao haviikiri Injili Bali vinakiri mambo ya kidunia tu.
Wakristo wengi midomo yao imefunikwa siku zote, maana hawatangazi injili ya KRISTO iokoayo.
Wakristo wengi matendo yao hayana ushuhuda wa Injili ya KRISTO.
Ndugu hakikisha kwa maneno ya kinywa chako unahubiri habari njema za ufalme wa MUNGU.
Hakikisha matendo yako unahubiri Injili ya KRISTO.
Hakikisha kwa maneno ya kinywa chako na kwa matendo yako unahubiri habari njema za ufalme wa MUNGU katika KRISTO YESU.

Maneno yako ni ushuhuda kukuonyesha wewe ni mtu wa aina gani.
Matendo yako ni ushuhuda mkubwa kuliko vyote.

Kataa dhambi, iache dhambi, ikimbie dhambi na usifanye dhambi tena.

Kitu kingine muhimu sana katika kukua kiroho na kuongezeka kiimani ni ibada.
Saa ya ibada huwa kuna uponyaji.
Saa ya ibada huwa kuna ushindi wa kiroho.
Ni muhimu sana kila mmoja kuwa ni mtu wa ibada.
MUNGU anatafuta watu wamuabudu katika kweli yake ya Wokovu.

Yohana 4:24 " MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
  Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments