MAOMBI YA KUPINDUA MASHAURI YA MAWAKALA WA SHETANI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
 MAOMBI YA KUPINDUA MASHAURI YA MAWAKALA WA SHETANI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu, karibu tujifunze Somo la maombi kisha tuombe maombi ya ushindi.
Leo tunapindua mashauri ya mawakala wa shetani waliyoyapanga kutuhusu sisi.
Shauri Mashauri ni nini?
Ni jambo linalojadiliwa na kuzungumzwa ili kutolewa maamuzi.
Kuna mashauri mazuri tu ambayo watu wa MUNGU wanaweza kujadili lakini pia kuna mashauri mabaya ambayo hupangwa na mawakala wa shetani ili kuwatesa watu wa MUNGU.
Watu wenye malengo mabaya dhidi ya watu wengine hupanga mambo mabaya ili yawapate watu hao.
Mwanzo 37:18-19 ''Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja ''
Huu ni mfano hai wa watu wanaoweza kupanga shauri lao ili kumdhuru mtu mwingine bila kosa lolote.
Kwenye maandiko hayo ni Yusufu ambaye hakuwa na kosa lolote lakini ndugu zake walipanga shauri ili kumuua, kwa sababu tu aliota ndoto na kuwaambia.
Hata wewe unaweza ukachukiwa tu bila kosa na watu wakapanga madhara kwako, unahitaji kumwita Bwana YESU ili akushindie.
Zaburi 2:2-5 ''Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake. Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, BWANA anawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.'' 
Inawezekana kabisa watu wakubwa kazini kwako wanapanga kukufukuza kazi bila kosa.
Inawezekana kabisa kuna wachawi wanapanga kukuua.
Inawezekana kabisa kuna watu wanataka ufilisike.
Wako maadui wengi sana katika ulimwengu wa roho na mwili ambayo hutaka mabaya fulani yawapate watu wengine.
Ndugu, Leo tunapindua mashauri ya kipepo yote.
Inawezekana kabisa kuna mashauri mabaya yanapangwa kwa ajili yako, leo tunapindua mashauri mabaya yote yanayopangwa kwenye ulimwengu wa roho wa giza ili yaje yakupate.
Hata MUNGU anawapinga wanaopanga mabaya kwa ajili yako, hivyo leo kwa maombi yako hakikisha kitu hicho kibaya kinachokusudiwa na wabaya wako kinafutika kwa damu ya YESU KRISTO.
Mithali 15:26 '' Mashauri mabaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi. ''

Tunahitaji shauri la MUNGU ndilo lifanye kazi na sio mashauri ya waganga na wachawi.
Shauri la MUNGU ni la milele na hilo shauri hakuna anaweza kulizuia. Katika maombi yako haribu mashauri ya giza yote.
Zaburi 33:10 '' BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.''
MUNGU anaenda kuyabatilisha mashauri yote ya washirikina, wachawi, waganga, wakuu wa giza na maroho ya shetani yote.
Ni kweli kabisa wachawi wanaweza wakakaa kikao kukujadili lakini ukimwita MUNGU leo hakika mashauri yao waliyoyapitisha kwenye vikao vyao vya siri  yatabatilika kwa jina la YESU KRISTO.


TUFANYE NINI ILI TUSIGUSWE NA MASHAURI YA KIPEPO.

1. Omba maombi ya kupindua mashauri yote ya giza.

'' Marko 9:23 ''YESU akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.''

Inawezekana kabisa wamepanga usiolewe/usioe, Leo kwa jina la YESU KRISTO pindua mashauri yao.
Inawezekana kabisa katika kikao cha kichawi walikusudia kukufilisi kipepo,  Leo kwa jina la YESU KRISTO pindua mashauri yao.
Inawezekana kabisa wameshapanga usipone ugonjwa, Leo kwa jina la YESU KRISTO pindua mashauri yao.
Kila walichokupangia wachawi na waganga na majini wote, Leo kwa jina la YESU KRISTO pindua mashauri yao.
 MUNGU Baba yuko tayari kukushindia.
 Ayubu 5:12 '' Yeye(MUNGU) huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.''

 2. Omba MUNGU abatilishe kila mashauri ya mawakala wa shetani kukuhusu wewe.

Ezekieli 21:27 ''Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.''
 MUNGU anaweza kuyafuta mashauri ya kipepo ya wabaya wako wako kama ukimuomba yeye.
Inawezekana kuna watu wanatumia rushwa ili kuipindua haki yako. Omba MUNGU ayabatilishe mashauri yao ya giza kupitia rushwa. 
 Mithali 22:12'' Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. ''
Inawezekana kuna watu wanatumia rushwa macho ya wanaotakiwa kukupatia haki yako.
Inawezekana kabisa wanapanga kuroga kazi yako au biashara yako, inawezekana kabisa wanapanga kukamata ufahamu wa mke wako au mume wako ili awe mtu wa kutenda machukizo tu, Leo omba MUNGU aharibu masahauri ya kipepo yote kukuhusu.
MUNGU ukimuomba hakika atayafuta mashauri ya watu wabaya wote wanaokupangia wewe mabaya. MUNGU hakuanza leo kuwasaidia watu wake bali tangu zamani za Biblia aliwasaidia wateule wake walioomba mbele zake ili mashauri ya giza yoye yapinduliwe.
Mfano hai ni huu katika andiko hilo.

Nehemia 4:15 ''Kisha ikawa, adui zetu waliposikia ya kuwa tumekwisha kupata habari, na ya kuwa MUNGU amelibatilisha shauri lao, ndipo sisi sote tukarudi ukutani, kila mtu kwa kazi yake.''
 Inawezekana kuna watu unaishi nao lakini wanakuwazia na kukupangia mabaya, Mwambie MUNGU atangue mashauari yao.

 3. Mwambia MUNGU akufiche mbali na kila mashauri ya siri mabaya kukuhusu wewe.

Zaburi 64:2 ''Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu; ''

Kama wanapanga kukufukuza kazi au kukusimamisha kazi, Mwambie Bwana YESU KRISTO akufiche mbali na mashauri ya siri ya maadui zako wa siri.\
Kama kuna mtu anapanga kukuwekea sumu kwenye chakula,  futa mpango huo leo kwa maombi yako katika jina la YESU KRISTO.
Kama kuna mtu anapanga kukurushia nguvu za giza, futa mpango huo leo kwa maombi yako katika jina la YESU KRISTO.
Omba MUNGU akufiche mbali na kila mashauri ya siri ya mawakala wa shetani.

 4. Omba MUNGU awe pamoja na wewe ili mashauri ya giza yasikuguse.

Isaya 8:10 '' Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana MUNGU yu pamoja nasi.'' 

Ni nani na wa wapi anakupangia jambo baya ili likupate?
Leo omba MUNGU akufiche mbali na machauri yote ya giza ili yasikupate.
Nani anakuendea kwa mganga?
Inawezekana kuna mtu ulikuwa na uhusiano naye kabla hujaokoka na mtu huyo alikufunga kwa vifungo vya kipepo, leo jifunge kwa jina la YESU KRISTO.
 Omba MUNGU Baba awe pamoja na wewe kazini, shuleni, kwenye biashara yako na kokote uliko ili mashauri ya mawakala wa shetani yasikupate.
Omba na MUNGU atakutendea muujiza mkuu.

Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane na nitakujulisha jinsi ya kukipata
na  Naamini kitakusaidia sana.
Hapa chini ni maombi ya Kupindua mashauri ya mawakala wa shetani kukuhusu wewe.
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake.
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini.


 MAOMBI YA KUPINDUA MASHAURI YA MAWAKALA WA SHETANI.

Baba wa mbinguni hakuna aliye kama wewe.
Ninakushukuru MUNGU Muumba wangu maana umenilinda na umenipa neema ya kuiona siku hii ya leo.
Pokea sifa na heshima wewe MUNGU wa mbinguni muumbaji wangu.
Niko mbele zako leo nikiomba ili mshauri yote ya watu wabaya wanaonipangia mimi yaharibike hayo mashauri yao.
Ninapindua kila mshauri ya wakuu wa giza kunihusu mimi, nayaharibu na kuyafuta kwa jina la YESU KRISTO.
Ninafuta kila mashauri  ya washirikina waliyonipangia mimi, Ninafuta mashauri yao kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninafuta kila mashauri ya waganga wa kinyeji waliyonipangia kutokana na kupewa taarifa na maadui zangu, Ninafuta mashauri yao kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninafuta mashauri yote ya kuzimu yanayopangwa kunihusu mimi, Ninafuta mashauri yao kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila shauri na mpanga shauri ninawaharibu kwa jina la YESU KRISTO.
 Kila anayepanga mipango ili niumwe au nidhulike, Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila anayepanga mipango ili nisipate mchumba, Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila anayepanga mipango ili kuivunja ndoa yangu, Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila anayepanga mashauri ili nifukuzwe kazini, Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila anayepanga mashauri ili nisizae,  Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila anayepanga mashauri ili nisifaulu masomo,   Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila anayepanga mashauri ili niendelee kuteseka, Ninaharibu na kufuta mashauari yake kwa, kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Majini wote walitumwa na kupewa mashauri na maadui zangu ili kunidhuri na kuondolea uwezo wa kufanikiwa, nawapiga kwa moto wa jina la YESU hao waliotumwa na hao watumaji pia.
Ee MUNGU Baba ninakuita  leo nikiomba uniondolee mashauri yote ya kipepo yaliyopangwa na kukusudiwa ili yanipate.
Neno lako linasema kwamba wewe MUNGU huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Nakuomba ee BWANA kwamba mashauri yote yaliyopangwa na mawakala wa shetani sasa yasinipate kwa vyovyote, ninafuta mashauri yao kwa jina la YESU KRISTO.

Pia BABA MUNGU ninakuomba na kila mashauri ya giza yanayopangwa au yatakayopangwa na mawakala wa shetani wao. Nifiche Ee JEHOVAH MUNGU wangu  kama Neno lako linavyosema katika Zaburi 64:2  kwamba ''Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu; ''
 Ninakuomba pia Ee MUNGU uwe pamoja na nami katika kazi yangu, ujana wangu, ndoa yangu, masomo yangu, familia yangu, biashara yangu na kila kitu changu ili mashauri ya watu wabaya yasinipate.
Neno lako linasema katika Isaya 8:10 kwamba '' Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana MUNGU yu pamoja nasi.'' 
Naamini Bwana YESU ukiwa pamoja na mimi hakuna shauri la kipepo litanipata.

 Naamuru mapigo kwa maadui zangu wote wanaopanga mashauri ya giza kunihusu mimi.
Naamuru mapigo kwa wachawi wote wanaopanga mipango mipaya kunihusu mimi.
Naamuru mapigo kwa wakuu wa giza wote na washirikina wote.
Ninaamuru mapigo kwa mapepo wote wanaopanga mipango ya kipepo kunihusu mimi.
Ninaamuru mapigo kwao wote, katika jina la YESU KRISTO mapigo mabaya na yawapate.
Neno la MUNGU katika Zaburi 2:9 linaniambia mimi kwamba ''Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.'' leo sasa ninawaponda kwa jina la YESU KRISTO Mawakala wa shetani wote waliopanga mashauri kunihusu.
Ninawaponda kwa kuamuru mapigo kwako, mapigo mabaya na yawapate ghafla sawasawa na walivyokusudia mabaya kwangu.
Nawapiga kwa jina la YESU KRISTO aliye hai milele.
Mimi kuanzia leo ni mshindi.
Nakushuru MUNGU Baba maana umenishindia.
Katika jina la YESU KRISTO ninaomba na kupokea ushindi mkuu, Amen Amen Amen.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments