MAOMBI YA KUIFUTA AIBU ILIYOPANGWA KIPEPO ILI IKUPATE.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU

  Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU kisha tuombe maombi ya ushindi.
Siku moja nilipangwa kufundisha somo la utumishi wa Kanisa kwa viongozi.
Niliandaa somo linaloitwa UMEITWA KUONGOZA NINI?
Nilipofika madhabahuni somo lile lilipotea kwenye daftari yangu ya masomo. Nilitafuta na  sikuliona, nilipitia ukurasa kwa ukurasa lakini sikuliona somo hilo. Watu walikuwa wameandaa karamu na daftari zao na Biblia ili kunisikiliza na kuandika lakini ilinichukua kama dakika tano nikiwa nawasalimia watu huku nikiwasifia kwa mavazi lakini huku nikitafuta somo kwenye daftari  bila mafanikio. Baadae nikaamua kufanya maombi na kisha kuanza kufundisha Neno la MUNGU bila daftari. Namshukuru ROHO wa MUNGU maana alinifunika na kila kitu kilienda vyema kabisa japokuwa nilikuwa hadi nilifike andiko kwenye Biblia ndipo nawaambia watu wafungue hapo. Baada ya ibada nilishangaa sana siku hiyo maana kuna mtumishi hadi aliniambia ni somo zuri sana nimefundisha na akaniomba nilichapishe na kumpa nakala moja, mimi nilibaki namshangaa MUNGU maana kumbe hakuna aliyegundua kwamba somo langu sikuliona.
Baada tu ya ibada somo lile nikaliona na kubaki nikishangaa sana sana. Shetani alitaka niabike kwa kushindwa kufundisha somo husika lakini hakufanikiwa.
Shetani siku zote hutamani watu wa MUNGU waabike lakini kwa kumtegemea MUNGU hakika adui zetu katika ulimwengu wa roho huabika wao.
Yeremia 17:18 '' Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.''

Kuabisha ni nini?
Kuabisha ni kumfanyia mtu jambo la kumvunjia heshima.
shetani na mawakala zake hujaribu kufanya mambo ya kuwavunjia heshima wateule wa MUNGU, Lakini kwa maombi aibu waliyoipanga kipepo itawapata wao.
Zaburi 6:10 ''Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.''
 
 Vifungo vya kipepo anavyofungwa mtu ni vitu vitakavyomfanya aabike.
Kama mawakala wa shetani watakupiga piga la kupoteza kumbukumbu na kuchanganyikiwa, ujue kifungo hicho kitazaa aibu kwako.
Binti kufungwa kipepo ili usiolewe, huko ni kuabishwa.
Kijana kufungwa kipepo ili usipate mchumba, huko ni kuabishwa.
Mwanafunzi una akili nzuri lakini mitihani inakaribia wewe unaumwa ghafla na ugonjwa huo ni wa kichawi na  hauonekani, huko ni kutafutiwa aibu.
Mawakala wa shetani hujaribu mara kadhaa ili kukufunga na ili uabike.
Leo futa kila aibu iliyopangwa kipepo ili ikupate.
Maombolezo 5:1 ''Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.'

Ziko aibu za kipepo nyingi sana na hizo unatakiwa uzikatae kwa jina la YESU KRISTO.
Kuzushiwa uongo ni hila za shetani ili uabike.
Kufilisiwa kipepo ni kazi ya shetani ili uabike.
Leo kataa kuabishwa kipepo.
Leo mtegemee MUNGU kwa maombi ya kukataa kuabishwa kipepo.
Zaburi 25:2-3 '' Ee MUNGU wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.''

Kwa jinsi gani unaabishwa kipepo?

1. Kukuzushia uongo.
1 Timotheo 4:2 '' kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;   '' 

2. Kufilisiwa kipepo.
Yohana 10:10a '' Mwivi(shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;''

3. Kufungwa vifungo vya giza ili usifanikiwe.
Vifungo vya giza viko vingi, baadhi ya hivyo ni.
A. Kufungwa fahamu ili uwe na maamuzi mabaya.
B. Kufungwa kifungo vha kukuzuia kuzaa.
C. Kufungwa kifungo cha kukuzuia kuoa/kuolewa.
D. Wanaotumika kipepo kuiondoa amani katika ndoa yako.
E. Kifungo cha kukuzuia kupata kazi.
Leo haribu mipango ya waliokufunga kipepo.
Zaburi 71:13 '' Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.''

4. Wanaotumika kipepo kuwa watawala wako.
Kutoka 1:8-10 '' Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.''

5. Mashambulizi ya giza.
Waefeso 6:16 ''zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.''

Mambo ya kufanya ili usiabishwe kipepo.

1. Tiisha kinywa chako ili usiongee yasiyokustahili.
Zaburi 71:24 '' Ulimi wangu nao utasimulia Haki yako mchana kutwa. Kwa maana wameaibishwa, Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.''
Kinywa chako simulia haki ya MUNGU na Neno la MUNGU na sio kuongea mambo ya kidunia ambayo mengine yanaweza kukugeuka na kukuabisha.

2. Kataa kuwa katika mazingira yanayotengeneza aibu kwako.
Yeremia 50:2 ''Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.''

3. Vunja maagano ya giza na futa kila kifungo cha kishetani
Zaburi 40:14-15 ''Waaibike, wafedheheke pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. Wakae hali ya ukiwa, na iwe aibu yao, Wanaoniambia, Ewe! Ewe! ''

 4. Usivae mavazi yasiyokustahili.
1 Petro 2:11 '' Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. ''
Tamaa za kimwili zinaweza kumfanya mtu akawa na kimwili na sio kiroho na kujiletea aibu kubwa kwenye kipengele cha mavazi.
Siku moja nilikuwa ibadani kanisa fulani mkoa fulani, kanisa hilo eneo la madhabahu liko juu sana hivyo inabidi upande ngazi ili kufika madhabahuni. Dada mmoja kutoka Nchi jirani na Tanzania alitakiwa kupanda madhabahuni, ilikuwa ni aibu kubwa sana maana hata sehemu za siri zilionekana wakati akipanda madhabahuni. Alipopanda madhabahuni alishindwa hata kuongea Neno moja, wakati yuko madhabahuni ndipo alionekana uchi kabisa, nilipowatazama wamama wa kanisani pale wote walikuwa wameinama chini wengine wakilia kama wanaomba kumbe wanasikitika sana. Wanaume tu ndio sikuona wameaangalia chini, ilikuwa ni aibu kubwa ya kujitakia kabisa.
Ndugu unahitaji kuwa makini na mambo ya kidunia, mavazi yanaweza kukuabisha kama utavaa mavazi yasiyostahili.

5. Omba ROHO MTAKATIFU awe pamoja na wewe.
Zaburi 32:8 '' Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.''
ROHO MTAKATIFU akikuonyesha njia hakika utakwepa mitego mingi ya kishetani iliyopangwa ikuabishe.

Maombi ya leo.
1. Ifute kwa maombi  aibu inayokukabili
 2. Haribu wanaopanga kukuabisha.
3. Kataa kuabishwa.

 Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane na nitakujulisha jinsi ya kukipata
na  Naamini kitakusaidia sana.
Hapa chini ni 
MAOMBI YA KUIFUTA AIBU ILIYOPANGWA KIPEPO ILI IKUPATE. Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake.
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.


 MAOMBI YA KUIFUTA AIBU ILIYOPANGWA KIPEPO ILI IKUPATE.

BABA katika jina la YESU KRISTO niko mbele zako nikikushukuru kwa kunilinda na kunipa uzima.
Pokea shukrani zangu MUNGU Muumba na asante sana kwa kunipenda hata mimi na ukanipa nafasi katika Wokovu wa Mwanao YESU KRISTO.
Niko mbele zako MUNGU wangu nikiomba kwa ajili ya kuharibu na kufuta kila aibu iliyopangwa kishetani ili inipate.
Kwa jina la YESU KRISTO, ninafuta kila aibu ya kipepo iliyokusudiwa inipate.
Wanaopanga niabike katika maisha yangu, naikataa aibu hiyo ya kipepo kwa, jina la YESU KRISTO aliye hai.
Sasa katika jina la YESU KRISTO ''Waaibike, wafedheheke pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. Wakae hali ya ukiwa, na iwe aibu yao, Wanaoniambia, Ewe! Ewe! '' kama Neno la MUNGU linavyosema katika Zaburi 40:14-15
 Wanaotaka kuniabisha katika ndoa yangu, naifuta aibu yao kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
wanaopanga nifukuzwe kazi na kuabika, nakataa mpango huo  na nafuta hiyo aibu inayopagwa kipepo, naifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Wanopanga nionewe mahakamani na kuabika, naikataa aibu hiyo ya kipepo.
Wanaopanga ndoa yangu ivunjike, naufuta mpango huo na naifuta aibu hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Wanaopanga niachwe na mchumba siku chake kabla ya ndoa,
naufuta mpango huo na naifuta aibu hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
Wanaopanga nisizae, naufuta mpango huo na naifuta aibu hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
Wanaopanga familia yetu inichukie bila kosa, naufuta mpango huo na naifuta aibu hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
Wnaopanga niumwe, naufuta mpango huo na naifuta aibu hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU
Wa naopanga jambo lolote baya linipate, naufuta mpango huo na naifuta aibu hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU 
Sasa kwa jina la YESU KRISTO  '' Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.'' Kama Neno la MUNGU BABA linavyosema katika Zaburi 71:13

 Kila anayepanga kuniabisha kipepo namharibu yeye kwa damu ya YESU KRISTO na naharibu kazi zake zote kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mchawi au mganga wa kienyeji anayetaka kuniabisha katika ndoa yangu au uzao wangu, namharibu yeye na kuifuta aibu aliyoikusudia, naifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila jini na kila mkuu wa giza anayetka aniabishe katika uchumi wangu, kipato changu au ajira yangu, nakataa kuabishwa na naifuta hiliyo aibu ya kipepo, naifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila eneo lililopangwa aibu inipate, naifuta hiyo aibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila ofisi au kila barabara ambako imepangwa aibu kipepo ili inipate, naifuta hiyo aibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
 Kila mtu anayetumika kipepo ili aniabishe, naifuta hiyo aibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila vikao vya siri vinavyopanga mipango ya kuniabisha, 
naifuta hiyo aibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtu wangu wa karibu anayeshirikiana na wabaya wangu ili kuniabisha na kuniharibia,
naifuta hiyo aibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Nafuta aibu zote zilizotengenezewa kwenye ulimwengu wa roho, nazifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru MUNGU BABA maana katika wewe mimi sasa ni mshinde.
Katika jina la YESU KRISTO naomba na kupokea ushindi.
Amen Amen Amen.

 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments