MAOMBI YA KUFUNGULIWA MACHO YA ROHONI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Ujumbe wa leo ni Maombi ya kufunguliwa macho ya moyo.
Kuona kitu chochote ni lazima uwe na macho na macho hayo yawe yanaona.
Kuona kitu chochote cha rohoni ni lazima uwe na macho ya rohoni na yawe yanaona vyema.
Macho ya rohoni ndio hayo hayo macho ya moyo, ndio Biblia inayaita katika baadhi ya maandiko.
Waefeso 1:17:18 " MUNGU wa Bwana wetu YESU KRISTO, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;"


Moyo wa mteule wa MUNGU unatakiwa uwe na macho ya moyo yanayoona.
Macho ya moyo ni muhimu sana.
Macho ya moyo wako yakiwa yanaona hakika utawabaini watu wabaya kwako, utaibaini mipango mibaya dhidi yako.

Yeremia 33:3 "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua."

Mambo makubwa na magumu usiyoyajua kwanza utayafahamu kama utakuwa na macho ya rohoni yanayoona.
Biblia inasema kwamba MUNGU atakuonyesha mambo makubwa usiyoyajua. Atakuonyesha maana yake utakuwa na macho ya kuona hayo mambo makubwa usiyoyajua ili MUNGU kupitia kuona kwako anataka akuonyeshe.
Macho ya rohoni ni muhimu sana.

Isaya 42:18-22 " Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona. Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA? Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii. BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha."

Kumbe hata mtumishi wa MUNGU anaweza kuwa kipofu kama haoni rohoni.
Kuna watu wamekuwa mateka wa shetani kwa sababu ya kukosa macho ya rohoni.
Kuna watu wako sasa katika vifungo vya giza kwa sababu tu ya kukosa macho ya rohoni.

Kuna kanisa walipata udhamini kutoka Ulaya, wenye macho ya rohoni kanisani waliona kwamba udhamini ule ulikuwa wa kishetani na wakalionya Kanisa, viongozi wa kanisa wakashupaza shingo. Baada ya muda wale wafadhili walifika na kuleta mambo ya kishetani hadi viongozi wa kanisa wakajuta na ndipo wakajua umuhimu wa macho ya rohoni.
Kama huna macho ya rohoni hakika maadui watakuwa nawakutesa sana na hutajua uombeje maana huoni rohoni.
Siku moja mimi Peter niliona kwa macho ya rohoni kwamba kesho yake ningeandikiwa kupewa Tsh 45,000 lakini hizo pesa niliziona kwenye ulimwengu wa roho kwamba ni nyeusi na nikaambiwa rohoni kwamba nisichukue. Niliona hayo nikiwa hata sijui kama kesho yake kungekuwa na jambo hilo, nilikuwa tu nimeitwa kesho yako kuhudhuria mahali Fulani kwa ajili ya masuala ya injili. Kesho yake ni kweli ikawa vilevile kama nilivyoona Jana yake, nilikuwa na uhitaji mkubwa sana wa pesa lakini nilizikataa zile pesa hata tuliokuwa wote pale wakanishangaa sana.
Ndugu macho ya rohoni ni muhimu sana. Macho ya rohoni yana ROHO MTAKATIFU.
Omba Leo ili ipewe macho ya rohoni.
1 Yohana 2:27 "Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake."

Inawezekana huna macho ya rohoni ndio maana hujui chanzo cha mgogoro katika ndoa yako.
Inawezekana huchumbiwi kwa sababu tu hujaona rohoni chanzo cha tatizo.
Wengine wamewahi kuoa wachawi kwa sababu tu ya kutokuona rohoni.
Inawezekana kabisa umekuwa unapona ugonjwa na baada ya muda ugonjwa ule unarudi, hujui chanzo lakini macho ya rohoni yanaweza kukujulisha.
Wengine wana macho ya rohoni lakini ni kwa kiwango kidogo sana.
Kuna mtu huona rohoni mambo madogo madogo tu lakini sio makubwa.
Ndugu nakuomba dumu sana katika utakatifu na maombi katika ROHO MTAKATIFU.
Omba MUNGU akupe Leo macho ya moyo yanayoona.
Bwana YESU amekuokoa ili pia akuonyeshe mambo makubwa usiyoyajua, hayo utayaona kwanza kwa macho ya rohoni.

 Pambana kiroho na sio kimwili.
Pambana na wachawi kwa maombi makali katika jina la YESU KRISTO.
Pambana na majini kwa maombi.
Pambana na waganga wanaotaka kukugeuza remote yao ya kufanikiwa, pambana nao kwa maombi kupitia jina la YESU KRISTO.
Pambana na mizimu ya ukoo wenu kwa maombi kupitia jina la YESU.
Mamlaka ya MUNGU kupitia KRISTO YESU ipo tayari kukushindia ukiamua kushinda.
Jambo muhimu kujua ni kwamba utapokea ushindi kulingana na kiwango chako cha Imani.
Kama unaamini MUNGU anaweza kukuondolea vifungo vya mikono tu lakini vifungo vya tumbo hawezi basi hatakuondolea vifungo vya tumboni maana umemwekea mipaka.
Mwamimi MUNGU asilimia zote na omba ukipambana hakika utashinda.
Katika maombi wakati mwingine fuata kanuni hii.
Marko 13:33 "Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo."
1. Angalia ROHO MTAKATIFU anasema nini.
2. Kesha macho ya rohoni.
3. Omba kwa Imani na utakatifu.


Kumbuka usimchekee mfilisti anayetaka kukuangamiza Bali omba maombi makali kumhusu ili ajue kwamba wewe una JEHOVAH MUNGU wako.
1 Samweli 17:37A " Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu."
Nani amekuwa mfilisti kwako hata anataka kukuangamiza?
Nani anataka kuangamiza ajira yako?
Nani anataka kuangamiza ndoa yako na uzao wako?
Je mchawi anajisifu sana kwamba amekuroga usiolewe au usioe au usizae au usipate kazi?
Leo Mwambie huyo kwamba " MUNGU ataniokoa na mikono yako ewe mfilisti"

Kama unataka kufukuzwa kazi kwa sababu ya tamaa ya mfanyakazi mwenzako aliye juu yako, Leo omba kwa Imani ukisema "MUNGU ataniokoa na mikono yako ewe mfilisti "
Nani anataka akufanye uwe kichaa?
Nani anataka akufanye tasa?
Nani anataka akufanye uonekane unanuka katika jamii?
Nani anataka akufanye uonekane sio lolote?
Wewe pambana kiroho na wakala huyo wa shetani.
Omba kwa Imani kama Daudi aliyesema "MUNGU ataniokoa na mikono ya mfilisti huyu"

MUNGU aliyekulinda tangu utotoni mwako anaweza kukuokoa dhidi ya anayekufanyia hila za kichawi ili ukataliwe.
MUNGU anaweza akakuokoa na anayekuwangia kila siku.
Amuru mapigo kwa wachawi wote wanaokuroga, amuru kwa njia ya maombi katika jina la YESU KRISTO.
Omba MUNGU awaangamize wafilisti wako wote.
Wafilisti wako ni pamoja na.
1. Majini.
2. Mizimu.
3. Wachawi.
4. Waganga.
5. Washirikina.
6. Wakuu wa Giza.
7. Wanadamu wanaotumika kipepo ili kukuangamiza.

akini utashinda kwa usahihi ukiwa na macho sahihi ya rohoni na yanayoona.
Kwepa laana zao kwa maombi.
Mkimbilie Bwana YESU ili akufanye uwe salama.
Omba na viapo vyao vya kipepo vitawarudia wao.
Omba na hila zao zitawarudia wao.
Wambie kwamba MUNGU kwako ni MUNGU wa kukuokoa.
Usiwahurumie maana watakuangamiza hivyo kata rufaa mbinguni ilia Bwana YESU akushindie.

Zaburi 68:20 "MUNGU kwetu sisi ni MUNGU wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, MUNGU atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa."
Wakikutisha wambie kwamba
"MUNGU ataniokoa na mikono yako ewe mfilisti "

Omba ndugu na hata ukisikia kufunga basi funga na MUNGU wa mbinguni atakushindia.
Unahitaji sana kuwa na macho ya rohoni ili ushinde, omba ili ROHO MTAKATIFU akupe macho ya rohoni.
 Ndugu mmoja aliona katika ulimwengu wa roho kuhusu rafiki yake ambaye shetani alikuwa amemfunga vifungo saba ili asizae katika maisha yake, Bila ROHO wa MUNGU kujulisha hakika angeendelea kuwa katika ndoa bila mtoto, na ndoa yake ilikuwa na zaidi ya miaka mitatu. Ndugu unamhitaji sana ROHO wa MUNGU katika maombi ili akupe macho ya rohoni.
Siku moja nilikuwa namuongoza sala ya toba ndugu mmoja, katikati ya maombi ROHO wa MUNGU akaniambia niache kwanza na maombi yale, niakaacha na kumuuliza yule ndugu juu ya kile alichonificha na kunidanganya. Yule ndugu akasema siri za ajabu sana ambazo alikuwa nazo akasema ameanguka kwenye uzinzi na viongozi kanisani kwao watatu(Ila hawajaokoka) na amekwisha kutoa mimba zaidi ya kumi, na mambo mengi alisema, ndipo nikaanza kumuongoza sala ya toba upya na akafunguliwa na kuokoka.
Macho ya rohoni ni muhimu sana kwa wateule wa KRISTO.
Macho ya rohoni kumbuka anayo ROHO MTAKATIFU hivyo omba atakupa.
1 Kor 2:10-11 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya MUNGU hakuna ayafahamuye ila ROHO wa MUNGU.''

Lakini pia ni muhimu sana kutambua kwamba macho ya rohoni hayapatikani tu kwa kuomba pekee bali yanapatikana kwa sababu hizi.
1. Kuishi maisha matakatifu na ya haki.
2. Kuiliishi kusudi la MUNGU la mwito wa MUNGU kwako.
3. Kuishi maisha ya maombi na kujifunza Neno la MUNGU.
4. Kuongozwa na kuenenda katika ROHOO MTAKATIFU.
Kwa hiyo tunapoenda kuomba ni muhimu ukatambua na hayo ambayo nimekueleza.

Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane na nitakujulisha jinsi ya kukipata
na  Naamini kitakusaidia sana.
Hapa chini ni 
MAOMBI YA KUFUNGULIWA MACHO YA ROHONI.

Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.


 MAOMBI YA KUFUNGULIWA MACHO YA ROHONI.

Baba yetu wa mbinguni, MUNGU wetu tunakuabudu na ninaungana na maserafi na makerubi kukuabudu.
 Naomba unisamehe YAHWEH MUNGU wangu kwa jambo lolote ambalo nimeenda kinyume na Neno lako takatifu.
Bwana YESU ninatubu kwako dhambi zangu zote, makosa yangu yote na uovu wangu wote.
Ninatubu pia kwa ajili ya lolote ambalo MUNGU Baba ulisema na mimi lakini sikuzingatia wala kuitii sauti yako.
 Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimi kwa ndoto, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimi kwa maono, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimi kwa Neno lako la ufunuo, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimi kwa njia ya watumishi wako, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimi kwa njia ya mazingira  niliyokuwepo, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimiusiku au mchana, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
Ninatubu kwa ajili ya pale uliposema na mimi kwa njia ya ROHO wako Mtakatifu, ila zikuzingatia, naomba unisamehe MUNGU Baba.
 Kwa neema yako MUNGU wangu ninaomba ee BWANA unipe macho ya rohoni ya kuona na unipe sikio la kusikia sauti yako.
Nipe kuwajua maadui zangu katika ulimwengu wa roho na nipe mbinu za kuomba ili kuwashinda.
Katika jina la YESU KRISTO ninaharibu kila mipango ya giza iliyosababisha nisione rohoni.
Kila adui mchawi au mganga anayepambana na mimi rohoni, sasa namharibu kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila jini niliyemuona kwenye ulimwengu wa roho akivaa sura za nyoka, binadamu au chocgote, kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninamharibu adui na atoke katika maisha yangu, biashara yangu, ndoa yangu, uchumba, familia yangu na chochote changu.
Kuanzia leo kila ambacho nitakiona katika ulimwengu wa roho nitaomba kwa jina la YESU KRISTO ili kama ni hila za shetani zife, ziteketee na kuharibika.
Nitaomba ili kama ni mapenzi ya MUNGU basi yatimie maishani mwangu.
Niko kinyume na kila madhabahu za giza, niko kinyume na kila mchawi na uchawi wake, na sasa naharibu uchawi na madhabahu za giza, kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Macho yangu ya rohoni sasa yataona na mawakala za shetani kuanzia sasa nitawaona na kuwaponda kwa moto wa jina la YESU KRISTO.
Ninakushukuru MUNGU Baba maana sasa masikio yangu yatasikia sauti yako tu na macho yangu yataona kila jambo la siri katika ulimwengu wa roho, na ROHO MTAKATIFU atanifundisha jinsi ya kutenda.
Bwana YESU, Neno lako linasema katika Luka 4:18 kwamba ulikuja ili vipofu wapate kuona, ee Bwana YESU, nami nahitaji kuona rohoni, nifanye kuona rohoni Ee Mfalme na Mwokozi wangu.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kushukuru.

Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen.
Hakika umeshinda.
Ukiweza kufunga unaweza kufunga hata siku 1 au 3 au 3 au hata 5 au zile ambazo wewe utaona unaweza ukihusika kila siku na kipengele kimoja kuombea na kumbuka baada ya maombi ya kufunga au hata maombi ya bila kufunga fanya tendo la imani kwa MUNGU kwa kutoa sadaka nzuri ikiambatana na maombi kutoka kwako na kwa mtumishi hai wa Bwana YESU juu ya ukomo wa kuteswa na madhabahu za uharibifu.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments