MAOMBI YA KUWAHARIBU WANAOTAKA KUCHELEWESHA KUSUDI LA MUNGU JUU YAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
 Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU na kisha tuombe maombi ya ushindi mkuu.
Kusudi la Ki MUNGU ni  nini?
Kusudi la Ki MUNGU ni  wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama ramani ya kuongoza maisha yako  katika kutimiza lengo la MUNGU.
MUNGU ana kusudi jema sana juu yako kama unamtii na unatembea kwenye kusudi lake.
Yeremia 29:11-13  '' Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.''

Kazi ya shetani na mawakala zake ni kutaka kuchelewesha  baraka zako zilizo katika kusudi la MUNGU kwako.
Shetani anajua kabisa kwamba hawezi kulizuia kusudi la MUNGU kwako lakini anaweza kulichelewesha kama wewe humsikilizi MUNGU. Shetani anaweza akakuingia wewe ili wewe ndio uzuie kusudi la MUNGU kwako.
Unahitaji kuwa makini sana na kusudi la MUNGU juu yako.
Ayubu 42:2 ''Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako(MUNGU) hayawezi kuzuilika'

Ni kusudi la MUNGU kabisa wewe upate Mchumba na mfunge ndoa takatifu.
Ni mpango wa MUNGU kabisa kwamba wewe kwenye ndoa yako upate uzao.
Ni Kusudi la MUNGU wewe ushinde vita ya kiroho unayopitia.
Shetani kuna makusudi Mengine hawezi kuyazuia ila anaweza kuchelewesha kama wewe mhusika utamfungulia mlango katika maisha yako.
Ingawa ni kusudi la MUNGU wewe ufunge ndoa lakini shetani anaweza akakuchelewesha kupata mchumba, kwa jinsi gani?
1. Kukupa mafunuo ya uongo yaani anakufunulia mtu asiye kusudi la MUNGU kwako.
Kumbuka shetani akikufunulia chochote ujue ni cha uongo na usikubali kukifanyia kazi katika maisha yako.
 
2. Kukufanya utende dhambi.

3.Kukufanya uwe katika kutafuta mchumba miaka mingi sana.
Kuna mtu anaweza kutafuta Mchumba kwa miaka 7 au zaidi.

4. Mapepo kukuvamia au kumvamia Mchumba wako ili muachane kabla ya ndoa.

Huo ni Mfano mmoja tu katika mingi ambayo shetani anaweza kumchelewesha mtu kupata haki yake iliyo kusudi la MUNGU.
Ni kweli kabisa ni kusudi la MUNGU wewe uolewe/Uoe kama ahadi ya MUNGU ilivyo katika Neno lake,
Mwanzo 2:24 '' Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. '' lakini ukikaa vibaya hakika shetani anaweza akakuchelewesha au akakufanya usiolewe kabisa maishani mwako au usioe kabisa maishani mwako.

Ni kweli kabisa ni kusudi la MUNGU wewe katika ndoa yako upate uzao, Mwanzo 1:28 '' MUNGU akawabarikia, MUNGU akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.'' lakini shetani anaweza akakuchelewesha kupata uzao.

Ni kweli ni kusudi la MUNGU wewe uokoke, Yohana 1:12 ''Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;'' Lakini shetani anaweza kukuchelewesha au kukuzuia kabisa kama ukimruhusu maishani mwako.
Wengine hupata Neema ya Wokovu  mapema kabisa lakini hushupaza shingo zao, baadae anapata magonjwa au mapigo ndipo anaokoka.
Wengine hupata Neema ya wokovu mapema kabisa lakini wanaidharau na kuendelea na dhambi, baadae kwa sababu ya wizi anapigwa na kwa neema ndipo anakumbuka kuokoka.
Kusudi la MUNGU ni wewe umpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako binafsi na kuishi maisha matakatifu.
Shetani ukimruhusu anaweza akachelewesha baraka yako ndio maana Biblia inakutaka uwe muombaji.
1 Thesalinike 5:17 '' ombeni bila kukoma;''

Inawezekana unasikia msukumo wa kufungua biashara, inawezekana kabisa ni kusudi la MUNGU ufanikiwe katika bishara hiyo, lakini shetani anaweza akakuchelewesha kwa kuwatumia watu ili wasikupatia eneo la kufungua biashara hiyo, au ukosefu wa mtaji, au kukuletea majanga ili uachane na kusudu la MUNGU hilo la kufanikiwa kwako.
Leo haribu kila adui anayelichelewesha kusudi la MUNGU la kufanikiwa kwako.

Kwa njia gani shetani anaweza  akakuchelewesha kupata baraka yako iliyo kusudi la MUNGU?

1. Kukufunga ufahamu wewe ili usijitambue kwamba unaihitaji hiyo baraka ya MUNGU.
2 Kor 4:4 '' ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU.''
Shetani anaweza kupofusha fikra zako  ili usikubaliane na kusudi la MUNGU la kufanikiwa kwako, huko ndiko kufungwa ufahamu wako kipepo.

2. Kukuletea marafiki wabaya au washauri wabaya.

Yakobo 4:4 '' Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU.''

 Marafiki wabaya wanaweza kukupoteza hata ukapishana na kusudi la MUNGU la kufanikiwa kwako.

3. Kukufanya utende dhambi.

2 Kor 11:3 ''Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa KRISTO.''
 Dhambi ni kikwazo kikuu cha kusudi la MUNGU.

4. Kukufanya uwe mbali na Neno la MUNGU la kukupa ufahamu juu ya baraka yako na jinsi ya kuipata.
Zaburi 12:6 '' Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. ''
Kukaa mbali na Neno la MUNGU ni kukaa mbali na ushindi wako.

5. Kukufanya udharau maongozo ya ROHO MTAKATIFU.

Yohana 14:26 ''Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.''

ROHO MTAKATIFU na Neno la MUNGU ndio pekee hutujulisha kusudi la MUNGU, Hivyo kumpinga ROHO MTAKATIFU ni kuukataa ushindi wako na ni kumkataa MUNGU anayebariki.
 
6. Kukufanya uutumie vibaya muda wako.
Waefeso 5:15-17 ''Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA.''
 Muda wako unaweza ukautumia vibaya hata ukabishana na kusudi la MUNGU la baraka kwako.
 
7. Kukuletea roho ya hofu, kiburi na tamaa mbaya.
''Maana MUNGU hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. - 2 Timotheo 1:7''

Kama MUNGU hakukupa roho ya woga, je hofu na woga unaoupata unatokana na nini? Wakati mwingine ni hila za shetani ili upishane na kusudi la MUNGU la kufanikiwa kwako.
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane na nitakujulisha jinsi ya kukipata
na  Naamini kitakusaidia sana.
Hapa chini ni 
MAOMBI YA KUWAHARIBU WANAOTAKA KUCHELEWESHA KUSUDI LA MUNGU JUU YAKO.
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.



MAOMBI YA KUWAHARIBU WANAOTAKA KUCHELEWESHA KUSUDI LA MUNGU JUU YAKO.

JEHOVAH MUNGU wa upendo, hakuna aliye kama wewe.
Ninakushukuru na kukuabudu katika jina la YESU KRISTO.
Asante Bwana YESU maana Jina lako lina nguvu,  Eee Bwana wangu YESU KRISTO, Ninakutukuza na ninasema asante kwa Neema yako na ukombozi wako.
 Niko muda huu mahali hapa nikiomba Neema na rehema zako. Naomba unisamehe MUNGU kwa popote na kwa lolote ambalo ni mimi nilihusika kukwamisha kusudi lako jema juu ya maisha yangu.
Neno lako katika Yeremia 29:11 linasema kwamba Wewe MUNGU muumbaji wangu unaniwazia mema.
Nakushukuru MUNGU BABA kwa kuniwazia mema na ninaomba unisamehe BWANA kwa kosa langu la kuzuia mema yako uliyoyakusudia yaje maishani mwangu.
Naomba unisamehe dhambi zangu zote, makosa yangu yote na uovu wangu wote. Naomba unipe neema yako Eee BWANA katika YESU KRISTO Mwokozi.
Niko muda huu mahali hapa nikikataa kila mpango wa shetani wa kuchelewesha baraka zangu zilizo kusudi lako MUNGU wa uzima.
Kila adui mchawi anayetumika kipepo ili kuchelewesha kusudi la MUNGU la baraka maishani mwangu, huyo adui ninamharibu yeye na kazi zake zote, katika jina la YESU KRISTO na aharibike sasa.
Kila mganga aliyetumika kuchelewesha kusudi la mimi kubarikiwa, ninamharibu huyo mganga na kazi zake zote nazifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mwanga na mshirikina aliyehusika kuchelewesha baraka zangu, ninamharibu huyo wakala wa shetani na kazi zake nazifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila Mwanadamu anayetumika kipepo dhidi yangu ili kuchelewesha au kuzuia baraka zangu, ninamfukuza atoke katika maisha yangu na aiachie baraka yangu sasa, katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila wakala wa shetani anayezuia nisifunge ndoa,  ninamfukuza atoke katika maisha yangu na aiachie baraka yangu sasa, katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila wakala wa shetani anayenizuia nisifanikiwe katika kazi yangu au biashara yangu, ninamfukuza atoke katika maisha yangu na aiachie baraka yangu sasa, katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila wakala wa shetani anayeondoa amani na furaha katika ndoa yangu, ninamfukuza atoke katika maisha yangu na aiachie baraka yangu sasa, katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila adui anayetumika kipepo ili kuchelewesha kusudi la MUNGU la baraka zangu, ninamfukuza atoke katika maisha yangu na aiachie baraka yangu sasa, katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Niko kinyume na kila madhabahu za giza zinazotumika kunichelewesha kupata baraka katika maisha yangu, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai nishinde.
Niko kinyume na kila agano la giza linalozuia kubarikiwa kwangu, Ninalifuta agano hilo la giza kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kuanzia leo katika jina la YESU KRISTO sitazuiliwa na Mchawi, mkuu wa giza, mshirikina na mganga yeyote.
Kila majini wanaotumwa na madhabahu za giza ili wacheleweshe kusudi la MUNGU katika maisha yangu ninawafukuza watoke katika maisha yangu na hawatarudi tena.
Neno la MUNGU katika Yoshua 23:10-11 linanipa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ya kufukuza maadui zangu 1000 katika maisha yangu,  Neno la MUNGU linasema '' Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia. Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.''
Hivyo katika jina la YESU KRISTO ninamfukuza kila adui anayewinda baraka zangu, ninamfukuza kwa damu ya YESU KRISTO  na kwa jina la YESU KRISTO.
Katika jina la YESU KRISTO sasa mimi ni mshindi.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen.
Hakika umeshinda.
Ukiweza kufunga unaweza kufunga hata siku 1 au 3 au 3 au hata 5 au zile ambazo wewe utaona unaweza ukihusika kila siku na kipengele kimoja kuombea na kumbuka baada ya maombi ya kufunga au hata maombi ya bila kufunga fanya tendo la imani kwa MUNGU kwa kutoa sadaka nzuri ikiambatana na maombi kutoka kwako na kwa mtumishi hai wa Bwana YESU juu ya ukomo wa kuteswa na maadui katika ulimwengu wa roho
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
+255714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments