MTEULE USITENDE DHAMBI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
MUNGU kwa Neema yake alimleta YESU KRISTO ili atuokoe na damu yake itusafishe  uovu na dhambi zetu zote.
Yohana 3:16-18 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''
Baada ya kumpokea YESU kama Mwokozi wako inakupasa sasa  uishi maisha matakatifu.
1 Petro 1:13-15 '' Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake YESU KRISTO. Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; ''
Hivyo kumbe ni agizo la Biblia kwako uliyempokea YESU kwamba inakupasa kuishi sasa maisha matakatifu.
Kumbe kutenda dhambi kwako Mkristo ni mapendekezo yako mwenyewe, na ni hasara yako mwenyewe.
Hivyo una uwezo wa kuyakataa mapendekezo yako mwenyewe ya kutenda dhambi.
Kumbuka shetani anajua kudanganya na anajua sana kubembeleza lakini ukimtii mwisho wake ni mbaya sana.
Lakini ndugu kwanini ukubali kudanganywa na shetani?
Ndugu nakuomba usikubali kudanganywa na shetani kupitia watu anaowatumwa kwako.
Uwe makini sana na litii Neno la KRISTO utaitwa heri.

1 Yohana 3:8-10 ''atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na MUNGU hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na MUNGU. Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake. ''

Ndugu kumbuka  Shetani anakaa sehemu chafu siku zote yaani ndani ya mtu mchafu kiroho.
Kama wewe ni mchafu rohoni ujue shetani atakaa na wewe maana shetani hukaa sehemu chafu tu.
Ndugu, usikubali kuwa mchafu na kama wewe ni mchafu yaani mdhambi hakikisha unasafishwa kwa damu ya YESU KRISTO kupitia toba.
Warumi 6:23 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika KRISTO YESU  Bwana wetu. '' 
Jitahidi ndugu usiwe mchafu maana ukiwa mchafu rohoni ujue shetani atakaa kwako maana shetani hukaa tu sehemu chafu.
Shetani hupandikiza tabia ndani ya mtu .
Je umepandikiziwa tabia gani na shetani?
Ndugu hakikisha unaachana na ambazo shetani amekupandikizia.
Zikatae tabia hizo na tiisha kwa Neno la KRISTO na tabia hizo zitakukimbia.
Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu.
Waefeso 5:1-3 '' Hivyo mfuateni MUNGU, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama KRISTO naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa MUNGU, kuwa harufu ya manukato. Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;''
 
Sumaki hii ya uasherati imewanasa hata ambao hawakutegemewa wala kutarajiwa.
Uzinzi uzinzi uzinzi umekuwa kama perfume ya kujipulizia kila Mara mtu akipenda.
Uasherati umekuwa kama heshima ya kibinadamu kwa vijana wengi.
Mbingu zimenyamaza kwa sababu iko jehanamu inawangoja wazinzi na waasherati.
Dhambi hii imekuwa sumaku kubwa ya shetani ya kukamata wanadamu ili waende jehanamu.
Wanadamu wa Leo ukimwambia kwamba aache uzinifu maana wazinzi na waasherati hawataenda uzima wa milele, mtu huyo anakuambia unamhukumu.
Ni Neno la MUNGU ndile limesema katika maandiko mengi tu kwamba wazinzi na waasherati sehemu yako itakuwa katika ziwa la moto.
Hata makanisani baadhi ya watu wamenasa kwenye sumaku hii.
Dada mmoja ambaye kila wiki anasimama na kushika mic kanisani kwao siku moja aliniambia kwamba hawezi kumaliza wiki bila kufanya ngono, na hajaolewa. Niliumia sana rohoni nikamwambia aache kutumika madhabahuni, yeye akasema itakuaje maana yeye ndiye tegemeo.
1 Kor 6:9-10 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.'

Mama mmoja alisema yeye ana mume mema sana na mume wake ni mwaminifu sana katika ndoa yao lakini yeye huyo mama ndio hutoka nje ya ndoa Mara kwa Mara, ni hatari inayohitaji neema ya MUNGU tu ili kutubu na kuacha.
Mama mmoja yeye ana watoto zaidi ya wawili na yuko katika ndoa lakini hana uhakika kama watoto wale ni wa mume wake wa ndoa, ni hatari sana.
Baba mmoja akiwa ndani ya ndoa amezaa watoto zaidi ya watatu nje ya ndoa tena wanawake zaidi ya wanne(4) tofauti tofauti.
Mwanaume moja ambaye husimama madhabahuni yeye kila Mara humdanganya mkewe kwamba anaenda safari kumbe ana mahawara karibia kila mkoa, ni hatari sana.
Watu wengi sasa wanaona uzinzi na uasherati ndio fashion nzuri ya wakati kuu.
Kila kijana ana girlfriend kwa lengo la ngono tu na sio vinginevyo.
Kila binti ana boyfriend kwa ajili ya uasherati.
Ukitaka watu wakuchukie basi kemea uzinzi na uasherati.
Watu wengi wamekuwa vipofu wa kiroho kwa sababu ya uzinzi na uasherati.
Mathayo 24:37-42 '' Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
''

Lakini upo mwisho mmoja kwa watenda dhambi wote ambayo ni jehanamu.
 Mathayo 25:31-34,41,46 ''Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.''
 
Ndugu unahitaji kutubu Leo na kuacha dhambi.
Ndugu mmoja akasema yeye anaishi maisha matakatifu ila dhambi moja tu yaani uzinifu ndio imemshinda, hiyo ni hatari.
Leo hata ndoa takatifu zimeadimika maana wahusika huanza kwanza uzinzi na uasherati ndio baadae ndoa, ndugu mnahitaji kutubu.
Ndugu yangu unayenisikiliza kwa njia ya ujumbe huu nakuomba tubu na acha dhambi hiyo.
Amua kuokoka.
Mwisho wa uzinzi na uasherati ni kifo(Mauti) na baada ya kifo ni hukumu
Waebrania 10:27 '' bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.''
 
Nimekuonya wewe Leo ili ukishupasa shingo usije ukalaumu siku ile ukiwa katikati ya bahari ya moto huku kifo kimezuiliwa ili uteseke milele.
Ni ROHO MTAKATIFU amenipa ujumbe huu live ili baadhi watubu na kumpokea Bwana YESU na kuokoka.
Isaya 55:6-7 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;  Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. ''
Mimi naamini utatengeneza ndugu baada ya kuusoma ujumbe huu.
Mimi naamini utaachana na mahawara na kuanza kuiheshimu ndoa yako.
Mimi naamini hutamsaliti tena mkeo/Mumeo.
Mimi naamini utaachana na huyo girlfriend/Boyfriend, wengine wanao zaidi ya mmoja, nakuomba ndugu achana nao.
Kijana au binti kaa tulia hadi wakati wako wa ndoa.
Uliyenisikia na utatubu na kuacha dhambi hiyo, MUNGU akubariki sana.
Mathayo 3:2 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''  
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu
.

Comments