MAREKANI YAITAMBUA YERUSALEMU KAMA MJI MKUU WA ISRAELI.

Rais Donald Trump wa Marekani
Marekani imeitambua Yerusalemu kama Mji mkuu wa Israeli.
Rais Trump wa Marekani amefanya maamuzi ya kihistoria ya kuipindua sera za miaka mingi ya Marekani kwa kuutambua mji wa Yerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel.
Rais huyo pia ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Trump amesema uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za dhati za kuleta amani ya kudumu bali inataka kutafuta suluhu ya mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina ambapo Marekani haifungamani na upande wowote, na haiwezi  kuingilia mipaka ya Israel na mamlaka zake,  pia akasema ''na hatuko tayari kuingilia katika migogoro yao ,hayo ni mambo yao wenyewe.''
 Turudi nyuma kidogo, Israel ilitangaza 1980 Jerusalem yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi duniani hazikukubali azimio hilo.
 Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim
 Ndani ya mji huu maarufu zaidi duniani na Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale. 
Kuna maeneo manne makuu na kila eneo, majengo huwa tofauti. Kuna eneo la Wakristo, Wayahudi, Waislamu na Waarmenia. Eneo hilo huzungukwa na ukuta mkubwa wa mawe. Hapo, kunapatikana baadhi ya maeneo yanayoaminika kuwa matakatifu zaidi duniani.

 Picha ya Yerusalemu
Kila eneo kati ya maeneo hayo manne (unaweza kuyaita mitaa) huishi watu wa aina moja. Wakristo wana maeneo mawili, kwa sababu Waarmenia pia ni Wakristo. Eneo lililotengewa Waarmenia, ambalo ndilo ndogo zaidi kati ya hao manne, lina vituo vya kale zaidi vya Waarmenia duniani.
Jamii ya Waarmenia imehifadhi utamaduni wake wa kipekee ndani ya Kanisa la St James na nyumba kubwa ya utawala. Maeneo hayo mawili yamechukua sehemu kubwa ya mtaa huo wa Waarmenia.
 Ndani ya mtaa wa Wakristo, kuna Kanisa Kuu la Kaburi na Ufufuo wa YESU KRISTO, ambalo ni muhimu sana kwa Wakristo kote duniani.
Hupatikana katika eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika kisa cha kusulubiwa, kufariki na kufufuka kwa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Kwa mujibu wa utamaduni wa Kikristo, YESU alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary. Kaburi lake linapatikana ndani ya kanisa hilo la kaburi na inaaminika kwamba hapo ndipo alipofufuka.

Kanisa hilo husimamiwa kwa pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kikristo.
Sana huwa ni wahudumu wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia.
Kuna pia wahuudmu kutoka kanisa la Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.
Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la YESU na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.
 Imekuwa ni wakati mzuri kwa Waisraeli baada ya uamuzi wa Rais Trump.
Rais Donald Trump amesema kuwa Marekani inaitambua rasmi Jerusalem kuwa ni Mji Mkuu wa Israel na mara moja mchakato wa kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv umeanza, wakati tukio hilo likikaribisha mvutano hasi kutoka nchi nyingi duniani.
“Jerusalem siyo kwamba tu ni kitovu cha dini kubwa tatu duniani, lakini hivi sasa ni kiini cha demokrasia yenye mafanikio makubwa duniani,” Trump amesema katika hotuba yake Jumatano.
Amesisitiza kuwa Marekani bado imejikita katika kusaidia kurahisisha kupatikana mkataba wa amani ambao unakubalika na pande zote “Israel na Palestina.” Nakusudia kufanya kila ninachoweza katika utawala wangu kusaidia pande mbili kufikia makubaliano,” Trump amesema.
Mapema Jumatano Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson alisema Jumatano kuwa Marekani bado inafikiri kuwa “kuna fursa nzuri sana ya kufikia amani” kati ya Israeli na Palestina huko Mashariki ya Kati.
Amesema licha ya Rais Donald Trump kuwa ameanza kutoa matamko yenye utata kuwa Marekani itautambua mji wa Jerusalem kuwa ni makao makuu ya Isreali bado kuna fursa ya kufikia amani.
Akiwa huko Brussels, Tillerson amesema Trump anania ya kuendeleza mchakato wa mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati. Tayari ana timu ambayo ameiuunda.
Timu hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa bidii.” Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani amehimiza watu “kusikiliza kwa makini hotuba yake yote” aliotoa Trump.

Huku waziri mkuu wa Israel ,Benjamin Natanyahu ameonekana kuunga mkono hatua ya rais Trump kwa kuelezea kuwa ni maamuzi ya kihistoria licha ya kuwa wapalestina wamemkosoa na huku Uingereza na nchi nyingine wanachama wa baraza la usalama wa umoja wa mataifa wameitisha kikao cha dharura ili kujadili maamuzi yaliyofanywa na rais Trump.
 Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana.

Benjamin Netanyahu
Netanyahu alisema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mkuu wa watu wengine wowote.
Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu alisema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya.
"Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi, kinaitwa Biblia, alisema. Unaweza kuyaskia katika historia ya jamii wa wayahudi kote duniani, Ni wapi tena kuna mji wa Israel, isipokuwa Jerusalem?
Kibiblia Israeli ni Taifa la MUNGU, Ni taifa pekee ambalo halikutokana na Mikutano ya duniani ya kutengeneza taifa, mfano ilivyokuwa kwa Berlin Conference bali Kikao cha kufanya Israeli kilifanyika Mbinguni, ndio maana Biblia inasema 
 Kumb 33:29 '' U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.''

Comments