MASWALI NA MAJIBU KUTOKA KATIKA BIBLIA

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze kupitia maswali haya ambayo mimi Peter Niliulizwa na watu mbalimbali.

Swali la 1
Je mtu anaweza akafanya dhambi hata asione umuhimu wa kutubu maana dhambi ni nyingi hata hazisameheki?

Majibu yangu.
Unapoisoma Biblia Ni Muhimu Kuisoma Kwa Macho Ya Aina Mbili. 
Macho Ya Damu Na Nyama Yakusaidie Kusoma Na Macho Ya Rohoni Yakusaidie Kuelewa Kile Ulichokisoma Kwa Macho Ya Kimwili. Hakuna Dhambi Ya Mwanadamu Isiyosameheka Kwa MUNGU Kama Mtenda Dhambi Huyo Atatubu Toba Ya Kweli.
Isaya 55:6-7 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa.   ''
 Kuna Watu Hujiona Ni Wadhambi Sana Hadi Wanatangaza Kuwa Hawawezi Kusamehewa. Huo Ni Uongo Wa shetani Wa Kuwafanya Waendelee Kutenda Dhambi. Ndugu, Kuendelea Na Dhambi Haikuidii Ila Kutubu Na Kuacha Dhambi Ndio Kusamehewa Kwenyewe. BWANA YESU Anasamehe Na Kuokoa, Mkimbilie Tu Leo Atakusamehe Na Kukuokoa.

Swali la 2.
Mke wa Kaini alitoka wapi?

Majibu yangu.
Mke Wa kaini alitoka katika mojawapo ya watoto Wa kike wa Adamu.
Kumbuka Eva aliumbwa akiwa MTU mzima na sio mtoto.
Eva aliumbwa akiwa mwanamke Wa umri Wa kuzaa(Mwanzo 2:22).
Adamu na Eva walivyoanza kuzaa waliwazaa Kaini na Habili lakini hadi kaini anamuua habili vijana hawa Wa adamu walikuwa ni watu wazima kiumri hivyo baada ya kaini na habili kuzaliwa ilipita miaka mingi hadi kifo cha habili na vijana hawa walikuwa wafugaji na wakulima hivyo waliishi umri Wa miaka mingi hata kuwa wafugaji na wakulima na Kwa miaka hiyo tu ingetosha kabisa Eva kuzaa watoto wengine wengi tu, kumbuka walibarikiwa kuzaa na kuongezeka(Mwanzo 1:28).
Baada ya kaini kumuua habili ilipita miaka mingi ndipo Sethi akazaliwa. Adamu alimzaa sethi yeye akiwa na miaka 130(Mwanzo 5:3) hivyo ni miaka mingi ilipita tangu kifo cha habili na Eva wakati huo alikuwa amezaa watoto wengi ambao nao walikuwa wamekua hata kuolewa na kuoa maana ilipita miaka mingi. Baada ya Adamu kumzaa sethi adamu aliishi miaka 800 ndipo akafa. Hivyo tunajitunza kwamba adamu na Eva kuzaa watoto zaidi ya 30 ingewezekana kutokana na kuishi kwao miaka Zaidi ya 900.
Na Biblia inasema kwamba Adamu alizaa watoto Wa kiume na Wa kike(Mwanzo 5:4) hivyo na mke Wa kaini aliyoka katika uzao huo huo Wa Adamu.

Biblia iko wazi inasema hivi

 ''Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. -Mwanzo 5:4-5'' Adamu akazaa watoto wa kiume na wa kike, hivyo hakuna swali hapo juu ya watoto wa adamu wa kike. 
Biblia imesema Adamu na Eva walizaa watoto wa kiume na Wa kike lakini Kwa majina ya watoto Wa kike Wa adamu hakutajwa hata mmoja lakini walikuwepo na ni zaidi ya mmoja ndivyo Biblia inavyosema.
Nimejibu Kwa kirefu kidogo ili kuwajulisha baadhi ya watu ambao hupotosha Kwa kusema kwamba inaonekana MUNGU aliumba watu wengine nje na adamu. Huo in uongo maana Biblia inasema Mwanadamu Wa kwanza kuumbwa ni Adamu kisha Eva na sisi wengine wote tunatokana na hao wawili tu na sio vinginevyo. Kumbuka hata akina kaini na habili kutajwa majina kwao ni Kwa sababu ya Nasaba zao tu, ndio maana baada ya habili kufa nafasi yake ya nasaba ikaja kuchukuliwa na Sethi ambaye alipatikana baada ya miaka mingi sana kupita.
Naamini umenielewa ndugu.
Kwa kumalizia ni kwamba mfano
Kijana Wa miaka 25 na binti Wa miaka 19 watafunga ndoa kisha wakaenda kuishi katika eneo lisilo na watu, MUNGU akawajaalia kuzaa watoto Wa kiume na Wa kike 12 kisha ikapita miaka 70 je eneo hilo halitakuwa na jamii kubwa inayoishi eneo hilo?

Jamii hiyo kubwa itapatikana, Kwa adamu na Eva ni zaidi maana wao walipewa agizo na kuzaa na kuongezeka. MUNGU alikuona wewe na Mimi ndani ya Adamu na Eva hivyo hakuna wanadamu wengine walioumbwa nje na Adamu na Eva.
By Peter M Mabula



  Swali la 3.
Mimi nina swali.
Wapo watu wanaosema Adam na Eva waliumbwa pamoja na pia wapo wanaosema alianza kuumbwa Adam, jibu sahihi ni lipi???

Majibu yangu yalikuwa ni haya.
Katika kitabu cha Mwanzo 5:1-2 ndipo penye huo utata

Wa kwanza kuumbwa ni Adamu Mwanzo 2:18 MUNGU anasema si vema MTU Huyu(Adamu) awe peke yake hivyo MUNGU akasema atamfanyia msaidizi(Eva) maana yake huyo Eva hakuwepo Kwa wakati huo ila tukio la Eva kupelekwa Kwa Adam ndilo linaonyesha Eva alianzia rohoni kabla ya kudhihilika mwilini ila Adam alianza kwanza kuumbwa.
Adamu hakujua kama Eva ameshaumbwa tayari kutokana na ubavu wake Adam ila Adam hakujua hili hadi alipomuona Eva.


  Nyongeza ya hilo
Unajua utata unakuja wapi?
Ni hapa 
Mwanzo 1:27.
MUNGU  akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU alimuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
hapa MUNGU aliwaumba kwanza roho zao wote wawili.
Lakini katika  mwili sasa Adamu ndiye wa kwanza kuumbwa akaumbiwa mwili wake kwa udongo  ndipo.. Eva.... akaja kuubwa katika mwili kupitia ubavu wa Aadamu.
(Mwanzo 2:7,21-23)
.(1)Alianza adamu.
(2)Akaja Eva.





Swali la 4.
Bwana Yesu asifiwe mchungaji Peter.
Nilikuwa naomba kukuuliza MTU anawezaje kuokoka? Na kuwa mtakatifu?
Mtu anawezaje kuokoka?


Majibu yangu yalikuwa haya.
Mtu anaweza kuokoka kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wake, akatubu na kuacha dhambi zote, kisha tangu siku hiyo anaanza kuishi maisha matakatifu akihudhuria ibada, maombi na kujifunza Neno la MUNGU huku akilitendea kazi neno hilo na MUNGU.
Mtu anawezaje kuwa Matakatifu?
Mtu anaweza kuwa mtakatifu kwa kukubali kufanyika mtakatifu, kukubali kufanyika mtakatifu ni Kumpokea YESU kama Mwokozi wako Binafsi.
Hatua za utakatifu ni pamoja na.
1. Kuliishi Neno la MUNGU katika kweli ya Injili ya KRISTO.
2. Kuenenda na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.
3. Kuishi maisha ya toba.
4. Kukataa dhambi zote na kuziacha daima.
5. Kuitii sauti ya MUNGU.
6. Kutimiza kusudi la kutwa kwako na MUNGU.
7. Kuishi maisha ya haki.


MUNGU awabariki sana ndugu wote.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU. 

Comments