Maombi yangu kwa wachache wanaojitoa kusapoti kazi ya MUNGU katika Injili ya YESU KRISTO iokoayo.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
By Mtumishi Peter Mabula.

Maombi yangu kwa wachache wanaojitoa kusapoti kazi ya MUNGU katika Injili ya YESU KRISTO iokoayo.

1. Moyo wako ukumbukwe na MUNGU.

2. Sadaka yako ikumbuke na MUNGU.


3. Sadaka yako inene mema.


4. MUNGU akulinde na kukutendea mema.


Ukauone wema wa MUNGU Baba sawasawa na Zaburi 27:13 inayosema " Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai."

MUNGU Akumbuke Sadaka Zako Na Kutimiza Kila Hitaji La Moyo Wako sawasawa na Zaburi 20:3-4 inayosema "Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote."
MUNGU Akupe Upendeleo Mbele Ya Kila Mtesi wako Kwa Sababu Tu Ya Utoaji wako katika kazi ya MUNGU.
MUNGU Baba akutendee mema sawasawa na Zaburi 50:5-6 inayosema "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu. Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana MUNGU ndiye aliye hakimu."

Nguvu Ya Sadaka Kiroho Ifanye Kazi Maishani Mwako sawasawa na Neno la MUNGU.
MUNGU akubariki.
Mtumikie Bwana YESU KRISTO utaitwa heri.
Mtumikie kwa kuhubiri, kushuhudia injili na mtumikie kwa Mali yako.
Mithali 3:9-10 "Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."

Usione mzigo kumtumikia MUNGU kwa pesa zako maana hiyo ni kwa faida yako mwenyewe.
Kumbuka vyote ulivyonavyo ni Mali ya MUNGU na ana mamlaka navyo kwa lolote muda wowote.
Zaburi 24:1 "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake."

MUNGU akubariki na kuzidi sana.
Ukawaone watoto wa wajukuu zako.
Ishi maisha matakatifu katika YESU KRISTO kwa ajili ya Uzima wa milele.
Amen Amen.

Comments