MAONO YA KUWAAMBIA WATU WAMPOKEE YESU KRISTO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Sitasahau maono haya.
Siku moja usiku nikiwa nimelala, nadhani ni kati ya mwaka 2015 au 2016 niliota ndoto ambayo sijawahi kuisahau.
Siku hiyo nilijikuta Niko katika ulimwengu wa roho na Bwana YESU pamoja na baadhi ya watu. Bwana YESU alikuwa amevaa vazi jeupe likiwa na mshipi mwekundu. Na watu wote pale walikuwa wamevaa mavazi meupe, na hata Mimi nilikuwa na vazi jeupe kama wao.
Bwana YESU akaniambia "Nenda kawaambie watu wanipokee Mimi kama Mwokozi wao na kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wangu"

Baada ya kupewa maelekezo hayo nikaenda haraka kuwafuata watu na nilitumia muda mrefu sana nikiwaambia watu wampokee YESU. Baadhi ya watu walikubali na wengine walikataa. Wakati nawaambia watu kumpokea YESU nilikuwa namuona YESU ila wao hawamuoni, ila ajabu ni kwamba wale waliokuwa wanakubali kumpokea YESU Mara tu baada ya kumpokea niliwaona wote wakianza kutembea kumfuata YESU aliko.
Nilipokuwa nageuka na kuangalia alipo YESU nilimuona akipokea wale watu niliowaambia waokoke na huku akinitazama, niliongeza juhudi sana kuwaambia watu Neno la MUNGU. Na kila aliyekuwa anampokea nilianza kumwona akitembea kwenda kwa YESU na huku mtu huyo ameshavaa vazi jeupe tayari.
Nilifanya Kazi hiyo kwa muda mrefu na baadae YESU akaniita kwa sauti kwamba niache kazi hiyo ya kuwaita watu na niende aliko yeye. Nikaacha kuwaambia watu huku nawatazama sana nikiekea aliko YESU KRISTO. Nikaenda na kufika na kujumuika na wenzangu waliokuwepo pale, na ndoto ikaisha.


Nimekumbuka ujumbe huo na nimekuandikia nikiwa na maana hii.

1. Wewe unayemtumikia Bwana YESU ongeza juhudi katika kuwapeleka watu kwa YESU Mwokozi.
1 Kor 15:58 '' Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA.''

2. Wewe ambaye hujaokoka unayo nafasi Leo ya kuokoka, usikubali nafasi yako ya kuokoka ipite.
Waebrania 3:7-8 ''Kwa hiyo, kama anenavyo ROHO MTAKATIFU, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa, ''

3. Bila YESU hakuna mwanadamu hata mmoja ataingia uzima wa milele.  
Biblia imeweka limit, Yohana 14:6 '' YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba(MUNGU), ila kwa njia ya mimi. ''.
Ni MUNGU mwenyewe aliandaa Wokovu kwa wanadamu wotem na Wokovu huo uko pekee katikia YESU KRISTO.
Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.'
Kwa sababu hiyo ndio maana Bwana YESU alisema kwamba alikuja kutafuta na kuokoa wanadamu maana kabla ya kumjua YESU hakika wanadamu hao wamepotea, hivyo wanapompokea YESU ndipo wanaanza kuufuata mpango wa MUNGU wa uzima wa milele. Ukitaka usiwe miongoni mwao waliopotea basi mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
 Luka 19:10 '' Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. '
hivyo ndugu kimbilia tu kwa YESU kama kweli unautaka uzima wa milele.

4. Wewe uliyempokea YESU kama Mwokozi hakikisha unaishi maisha matakatifu kama yeye YESU alivyo mtakatifu
1 Petro 1:15 ''bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; ''

5. Usiyumbishwe na mafundisho ya mashetani, hata unataka kumwacha YESU aliye pekee Mwokozi.
2 Yohana 1:7-10 ''Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa YESU KRISTO yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo. Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya KRISTO, yeye hana MUNGU. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba(MUNGU0 na Mwana(YESU) pia. Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. ''

6. Fuata kanuni hii " Usiishi kwa sababu tu unaishi Bali ishi kwa sababu YESU KRISTO anaishi ndani yako na unamtii"
Wagalatia 2:20 '' Nimesulibiwa pamoja na KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali KRISTO yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa MUNGU, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.''

7. MUNGU wa kweli ni mmoja tu na anapatika katika KRISTO YESU pekee.
1 Timotheo 2:3-6 '' Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za MUNGU Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu MUNGU ni mmoja, na mpatanishi kati ya MUNGU na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu KRISTO YESU; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.''
 
KRISTO ndiye aliyemtambulisha MUNGU Baba kwetu.
Ndani ya MUNGU Baba kuna YESU KRISTO na ROHO MTAKATIFU hivyo ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana kwako katika maisha yako ya Wokovu wa KRISTO.

Nimeikumbuka ndoto hiyo na nikasukumwa kukuambia mambo haya muhimu sana.
Nimelikumbuka hata Neno hili kwamba wakati mwingine MUNGU husema na sisi kwa ndoto.
Ayubu 33:14-16 " Kwa kuwa MUNGU hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,"

Ndugu usishikilie dini tu huku hujaokoka.
Ndugu usishikilie dhehebu tu huku huna YESU Mwokozi moyoni mwako.
Kumbuka vya dunia ulivikuta na vyote vya dunia utaviacha, ni heri kumaliza safari ya duniani ukiwa umeokolewa na YESU KRISTO.
Anza Leo ndugu kuishi maisha matakatifu baada ya kuokoka.
Ndugu usomapo ujumbe huu naomba uombe kwa ajili ya nchi yako, ukiwa katika maombi yako ya kufunga omba kwa ajili ya nchi yako.
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments