MASOMO YA MTUMISHI PETER MABULA

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya ambaye umekuwa ukijifunza ujumbe wa Neno la MUNGU kupitia masomo yangu ninayoandika na kupost kila mara.
Nimekutana na changamoto moja ambayo kuna baadhi ya watu hujikuta wakisema vibaya na kuchukia, sio lengo langu nimkwaze mtu hata mmoja kupitia utumishi wangu kwa KRISTO.
Kuna watu husoma masomo yangu fulani na kuyapenda na baada ya muda mrefu iwe ni mezi kadhaa au miaka kadhaa wananiomba tena niwatumie mosomo hayo inbox Whatsapp, watu hao ni wengi mno.
Kuna mtu mwingine akiona somo Facebook anaomba nimtumie kwenye Email yake, hao ni wengi mno.
Mwingine akiona somo kwenye blog anaomba nimtumie Whatsapp, hao ni wengi sana.
Kuna watu hupoteza masomo, nikiwa na maana alisoma somo langu kisha akasema atakuja kuendelea baadae lakini akikaa siku kadhaa anakuta nimepost masomo mengine mengi kiasi kwamba kila akitafuta somo alitakalo haliona, hao ni wengi sana.
Watu hawa wote hawafanyi vibaya hata kwa nukta moja ila mara nyingi wengine nimeshindwa kuwatimizia matakwa yao kwa sababu na mimi nina majukumu mengi mno, huwa natamani muda mwingi niandae masomo na nikipata nafasi pia nijibu maswali au niwashauri walioomba ushauri maana hao ni mengi mno, hivyo kukosa kabisa muda wa kumhudumia kila mmoja, maana pia nina majukumu mengi na huduma nyingi.
Hivyo naomba kutumia fursa hii kuwaomba ndugu zangu wapendwa kwamba;
Endelea kujifunza Neno la MUNGU kupitia kule ambako huwa unanifuatilia, kama ni blog endelea kufuatilia, kama ni whatsap groups endelea kufuatilia, kama faceboog page au profile au groups endelea kufuatilia na ukiona kitu umekipenda andika pembeni au ukiona somo lefu basi copy na paste sehemu ambako utaliona ukilihitaji.
Na wengine wanalalamika kwamba naandika masomo marefu sana lakini nina sababu mbili za kufanya hivyo.
Hata mimi najua kabisa kuna masomo unahitaji kulifundisha hata mara 4 ndipo unamaliza lakini huku ni mtandaoni, niliwahi kuandika masomo mawili yakiwa na sehemu mbili kila moja lakini hiyo huwa inanisumbua hadi leo maana mtu akiona sehemu ya kwanza ananitafuta ili nimtumie sehemu ya pili maana haioni, sasa kama ningeandika masomo 100 kati ya 822 ambayo nimeshaandika hadi leo, na hayo 100 yawe na sehemu 2 hadi 3 kila moja hakika ningukuwa siwezi kufanya chochote zaidi ya kuwasaidia watu kupata masomo wanayoyataka.
Inbox pekee kuna siku nimejikuta najibu meseji za watu 100 kwa siku moja maana ni watu wengi mno wanahitaji msaada.
Sasa naomba nikupe njia ya kulipata somo langu lolote ulitakalo wakati wowote.
Unachotakiwa kufanya ni kwenda ggogle au opera min au mtandao wowote ambao wewe huwa unautumia ku-search vitu kisha andika jina la somo ulitakalo kisha weka alama ya '', '' kisha jjna langu Peter Mabula au Peter M mabula na utaona masomo yanayohusiana na kitu ukitakacho.
Mfano unaweza kuandika MAISHA YA WOKOVU, PETER MABULA. au unaweza ukandika MAOMBI YA KUHARIBIBU MADHABAHU ZA GIZA, PETER MABULA au MAOMBI YA KUFUTA AGANO LA KIPEPO, PETER MABULA. au UCHUMBA NA NDOA, PETER MABULA.

Na kuna watu huyaweka masomo yangu katika blog zao au page zao huku wameyabadili kidogo hivyo sehemu salama kabisa ambazo uki-search somo langu na kusoma penda kusoma somo hilo likiwa katika link hizi.
1. Maisha ya ushindi, ni blog kwa link hii
https://maishaushindi.blogspot.com
2. Page ya facebook ya blog yangu iitwayo Maisha ya ushindi.
link yake ni hii
https://facebook.com/MaishaYaUshindi
3. Page yangu binafsi ya facebook iitwayo Mwinjilisti Peter Mabula.
link yake ni https://facebook.com/Mabulapm

MUNGU akubariki sana na endelea kujifunza Neno la MUNGU.
Nisamehe pia kama nimekukwaza.
Na nakuomba share kwa mtu mwingine ambaye huwa anafuatilia masomo yangu.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com

Comments