NENO LA MUNGU NI MUHIMU KATIKA KUPOKEA MAHITAJI YAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
MUNGU akikusudia jambo hakuna wa kulibatili wala hakuna atakayeuzuia mkono wa MUNGU kutenda chochote.
Isaya 14:27 " Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?"
MUNGU akikusudia ufunge ndoa, ndivyo ahadi yake ilivyo katika Neno lake, ndugu baki tu kwenye kusudi la MUNGU huku ukiishi maisha matakatifu.
MUNGU amekusudia upone, ndugu muombe MUNGU katika jina la YESU KRISTO utapona.
MUNGU amekusudia usiteswe tena na nguvu za Giza, mtii MUNGU na mtegemee kwa maombi na maombezi hakika utafunguliwa vifungo vyote.
MUNGU amekusudia kuwaabisha mawakala wa shetani wote wanaofuatilia maisha yako, wewe mtii KRISTO YESU, nyenyekea kwenye mkono wa MUNGU, mche MUNGU na husika na maombi hakika kusudi la MUNGU hilo litatimia.
Inawezekana walisema hutazaa au hutapata mchumba, ndugu kama MUNGU amekusudia ufanikiwe hakika utafanikiwa, ila baki tu katika kusudi la MUNGU ambalo ni utakatifu, utoaji na maombi.
Walipanga ufilisike, ndugu MUNGU akisema hutafilisika hakika itakuwa.
Walipanga mabaya yakupate, MUNGU akisema mabaya hayatupata wewe(Zaburi 91:10) hakika itakuwa.

Hilo andiko la Zaburi 91:10 linasema hivi '' Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.''
 
Mimi  nakushauri kwamba hakikisha MUNGU anasema neno kukuhusu.
Hakikisha ROHO MTAKATIFU anakuhakikisha ushindi, amini na baki kwenye kusudi la MUNGU.

Dawa ya moyo ni Neno la MUNGU.
Ndugu utibu moyo wako kwa Neno la MUNGU.
Zaburi 107:20 '' Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.''
Usilipokee Neno la MUNGU kama neno la mwanadamu.
Neno la MUNGU ni la MUNGU, litii hilo na lifanyie kazi katika maisha yako.

Wakolosai 3:16-17 '' Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye.  ''
Neno la MUNGU likae ndani yako.
Neno la MUNGU lijae ndani yako.
Neno la MUNGU litengeneze maisha yako.
YESU KRISTO ni Neno juu ya Neno la MUNGU hivyo litii Neno la MUNGU na liishi hilo tu.
Zingatia hayo katika maisha yako yote na utastawi sana kiroho na kimwili.

Hakikisha tu unamjua MUNGU na kusudi lake na mpango wake kwako, kwa kukusaidia kidogo iko hivi;
MUNGU ni Muumbaji wetu
Mwanzo 1:27 '' Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. ''
 
MUNGU ni Mwokozi wetu.

Tito 2:13-14 ''tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.''
 
MUNGU anaweza yote na hakuna aliye kama yeye 

Zaburi 83:18 '' Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote. ''
 
MUNGU wetu ni ROHO na anaabudiwa katika kweli 

Yohana 4:24 '' MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. ''
 
Hakuna aliye kama MUNGU wetu 

Yeremia 10:6 '' Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.''
 
MUNGU wetu anapatikana ndani ya Wokovu wa KRISTO 

Yohana 3:16-18 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''
 
MUNGU wetu anataka utakatifu

Zaburi 34:14 '' Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.''
Ndugu hii ni muhimu sana pia.
Isaya 55:6-7 "Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa."


Ukishajifunza ndani ya Neno la MUNGU kuhusu MUNGU na kanuni zake hakika utaomba katika Kusudi la MUNGU na kupokea mahitaji yako.
Kama kuna Binadamu anadhani ana akili sana, naomba atambue, Kama ni akili basi za MUNGU hazichunguziki. 
Isaya 40:28 '' Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye MUNGU wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.''

 Nataka pia ujue jambo hili, Kila Mkristo amewekwa na MUNGU ili kuujenga mwili wa KRISTO.
Ajabu ni kwamba sio Wakristo wote wanaujua Mwili wa KRISTO kwamba ni kanisa.
Na sio kila mkristo analijua jukumu lake hii la kuujenga mwili wa KRISTO.
Hii ni takakari kwako mpendwa wangu katika KRISTO YESU.
BWANA yuaja na atamlipa kila mtu sawasawa na kazi na matendo yake.

Maamuzi yako ya haraka haraka yasiyo sahihi, wakati mwingine yanaweza kukuweka hatarini. Uwe makini sana
Hakikisha unatembea katika Neno kwa utakatifu na kumtii ROHO MTAKATIFU.
Neno la MUNGU lina mchango mkubwa sana wa wewe kupokea mahitaji baada ya maombi.
Biblia inasema
Zaburi 23:4 "Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji."
Gongo la MUNGU ni Neno lake yaani Biblia takatifu.
Fimbo ya MUNGU ni kuongozwa au maongozo ya MUNGU kwako.
Fimbo ya MUNGU kwako inaweza kuwa Neno la ufunuo ambalo ROHO MTAKATIFU anakupa kutoka katika Biblia kwa kusudi maalum.
Fimbo ya MUNGU hubeba;
1. Mamlaka ya KRISTO kwenye maisha yako.

2. Uongozi wa ROHO MTAKATIFU kwako.
3. Matumaini mapya ya ushindi kwa maana wewe u mteule wa MUNGU uliyepokea Wokovu wa YESU
.
4. Neno lake la ufunuo ambao hakika litatimia.

Yeremia 1:11-12 "Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi.
Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize."

Ufito ni fimbo, hivyo ni Neno analokupa MUNGU ili litimie.
MUNGU akubariki sana kama gombo lake na fimbo yake vinakufariji kwa kukuhakikishia ushindi wa jina la YESU KRISTO kwako.

 Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
0714252292(Hadi whatsapp).
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments