KILA MTU NA AITII MAMLAKA ILIYO KUU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibu katika somo hili fupi ili tujifunze Neno la MUNGU.
Warumi 13:1 '' Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na MUNGU.''
Kila mtu aitii mamlaka iliyo kuu, ziko mamlaka zilizo kuu nazo ni hizi.

1. Mamlaka ya MUNGU.
 
Hii ni mamlaka kuu kuliko zote, mamlaka hii ina YESU KRISTO pekee.
Mathayo 28:18 ''YESU akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. ''
 
YESU ana mamlaka yote mbinguni na duniani hivyo mamlaka zote za duniani zinapaswa kumtii.
YESU anatawala mbinguni na duniani, hivyo mamlaka ya MUNGU iko na MUNGU kupitia YESU KRISTO, hiyo ndiyo mamlaka kuu ya kwanza ambayo kila mwanadamu anatakiwa kutii. Akitawala YESU KRISTO maana yake ametawala MUNGU mwenyewe, akitawala MUNGU ujue ni YESU KRISTO pia anatawala.

2. Mamlaka ya Kiroho ya kiroho ya watumishi wa MUNGU.
 
Kanisa lina mamlaka kuu sana kiroho ila kama tu Kanisa likikaa katika kweli ya MUNGU kupitia YESU KRISTO.
Mamlaka ya viongozi wa Kanisa inatakiwa itokane na MUNGU tu na sio vinginevyo.
Viongozi wa kiroho wa Kanisa wana Mamlaka kubwa sana ambayo wamepewa na MUNGU kupitia YESU KRISTO.
Bwana YESU mwenye mamlaka yote mbinguni na duniani ndiye aliywwapa mamlaka pia watumishi wake, na yeye Bwana YESU anasema ''Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.- Mathayo 10:40 ''
Maana yake anayepokea ujumbe wa MUNGU unaoletwa na watumishi wa KRISTO basi mtu huyo anakuwa amepokea kutoka kwenye mamlaka iliyo kuu sana.
Mamlaka ya kiroho ya Kanisa la MUNGU duniani itakiwa iheshimiwe na watu wote.
Biblia inasema anayemwasi mwenye Mamlaka anakuwa anapishana na kusudi la MUNGU.
Warumi 13:2 ''Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU; nao washindanao watajipatia hukumu.''
Wako watu walipingana na watumishi wa MUNGU wakaishia kufa.
Wapo watu waliwaonea watumishi wa MUNGU na watu hao kuishi kufa.
Mamlaka ya kiroho ya watumishi wa MUNGU ina nguvu sana japokuwa katika hali ya kimwili inaweza isionekane sana.
Unaweza ukamdharau mchungaji wako na ukamtukana au kumpinga kwa sababu tu wewe una kazi nzuri au wewe unaheshimika katika jamii kuliko yeye lakini huyu mtumishi mwaminifu wa MUNGU ana mamlaka kuu sana katika ulimwengu wa roho, anaweza akakutamkia Neno likakuvaa siku zote za maisha yako.
Watumishi wa MUNGU wana mamlaka sana kwa sababu wakati mwingine wanakuwa wanaleta ujumbe wa MUNGU mwenye mamlaka yote, hivyo unaweza ukaletewa ujumbe ambao huupendi lakini kwa sababu ni ujumbe wa MUNGU fanyia kazi na sio kuidharau hiyo mamlaka ya kiroho.
Wengine walibisha na kujikuta wanajiinua na kumkufuru MUNGU hivyo wakapata uharibifu mkuu.
Ona mfano huu ambapo nabii feki aitwaye Hanania alipishana na agizo la MUNGU.
Hanania aliwaambia watu uongo kwa lengo kwamba Yeremia nabii aonekane sio kitu kwa jamii na taifa, Ukisoma sura ya 28 ya Yeremia utaona hayo lakini kwa sababu alimdharau mtumishi halisi wa MUNGU na kujiona yeye ni bora kuliko watumishi halisi wa MUNGU hakika alikufa mwaka huo huo kwa sababu amepishana tu na mtumshi halisi wa MUNGU, Mstari wa 15 hadi 17 wa hiyo Yeremia 28 inasema hivi ''Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; BWANA hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo. Basi BWANA asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya BWANA. Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba.''
Kwenye kinyume na mamlaka ya MUNGU iliyo katika watumishi wake waaminifu ni hatari sana.

3. Mamlaka ya kiserikali iliyokubaliwa na MUNGU.
Serikali ni mamlaka iliyo kuu hivyo moja ya mamlaka iliyo kuu anayotakiwa kuitii mtu ni mamlaka ya kiserikali, anayetakiwa kuitii mamlaka hii ni mtu yeyote yule awe serikalini au nje ya serikali.
Mamlaka ya kiserikali inaweza kujumuisha Rais, wateuliwa wa raisi, bunge mahakama, jeshi n.k

Kwanini uitii mamlaka iliyon kuu?
Kwa sababu kama kuna kusudi la MUNGU basi unapomwasi mwenye mamlaka uakuwa kinyume na agizo la MUNGU na watu wa jinsi hiyo Biblia inasema watakuwa wanajipatia hukumu.
Warumi 13:2-8 ''Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa MUNGU kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa MUNGU, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa MUNGU, wakidumu katika kazi iyo hiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. ''
 
Ndugu, kumpinga YESU KRISTO ni kumpinga MUNGU.
Kuidharau mamlaka ya Kanisa la MUNGU ni kumdharau mwenye Kanisa ambaye ni MUNGU.
Mwenye mamlaka ni Mtumishi wa MUNGU kwa ajili ya mema.
Unapoitii pia mamlaka ya Kibinadamu kumbuka pia kwamba usiifanye mamlaka hiyo kuwa ndio tegemeo lako pekee, ukifanya hivyo utapata laana.
Yeremia 17:5 '' BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. ''
 
Tii mamlaka kabisa lakini mtegemee MUNGU aliyeziweka hizo mamlaka.
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu. Ukiweza pia toa copy na kuwasambazia watu wengi zaidi.

Comments