MKRISTO UNATAKIWA UFIKIE HATUA AMBAYO HUWEZI KAMWE KUMWACHA YESU KRISTO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Mkristo anatakiwa kufikia hatua ambayo hawezi kamwe kumkana YESU KRISTO.
Mteule wa MUNGU anatakiwa afikie hatua ambayo hawezi  kumkana YESU kwa sababu ya dhambi au ya tamaa za kidunia au kwa vyovyote.
 Mathayo 10:33 '' Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za BABA yangu aliye mbinguni.''

Watu wengi sana wakati mwingine wamejikuta wanamkana YESU kwa tamaa zao au kuupenda ulimwengu.

Mama mmoja siku moja aliniandikia ujumbe uliniacha na maumivu rohoni, Nauleta  ujumbe huo kama ulivyo, alisema hivi:
Shalom mtumishi Mabula,kwa jina naitwa .......(Jina nimeliondoa), uliniombea nikapata kazi mwaka jana ,tatizo nililonalo kwa sasa mimi ni mjamzito na aliyenipa anataka niitoe kwa sababu ya maadili ya kazi mtu huruhusiwi kuwa mjamzito kabla ya mwaka kuisha, mimi sijamaliza mwaka,naomba unishauri Mtumishi sielewi nifanye nini mpaka sasa na kazini wakigundua kuwa mimi ni mjamzito nitasimamishwa kazi, sielewi nifanye nini nina mawazo sana.

Majibu yangu mimi Peter Mabula.
Baada ya kupokea ujumbe wa ndugu huyo moyo wangu uliuma sana, kisha nikamjibu.
Majibu yangu kwa ndugu huyo yalikuwa haya;

Nakuomba Sana Sana Usitoe Mimba Hiyo. Ni Heri Ukasimamishwa Kazi Ukazaa Na Baadae Utapata Kazi Ukiwa Na Mtoto Wako. Usiue Ili Kulinda Kazi. Ukifanya Hivyo Utapata Madhara Makubwa Sana Sana, Naiona Hatari Kubwa Kwako Kama Ukiamua Kutoa Mimba, Utakosa Kazi Na Mtoto Pia, Muogope MUNGU Katika Hilo. Hata Hivyo Uasherati Ni Jambo Baya Sana, Hukutakiwa Kuhusika Na Dhambi Hiyo. Nakuomba Mche MUNGU Utaishi. Sina Maombi Ya Kukuombea Kwa Sasa Ila Ni Ushauri Tu.
Unaweza Ukaishi Maisha Yote Huna Raha Kwa Sababu Tu Damu Ya Mtoto Asiye Na Hatia Inakulilia.Nimepata Maumivu Sana Katika Hili. Nakuomba Tengeneza Kwa YESU Na Anza Kuishi Maisha Matakatifu, Usitoe Mimba Na Kumbuka Kwamba Laana Ya Kutoa Mimba Inaweza Kuzuia Baraka. Heri Ufukuzwe Kazi Kuliko Kutoa Mimba. Mche MUNGU Utaishi. Mtoto Huyo Anaweza Kuja Kuwa Msaada Kwako Mara Mia Kuliko Ambavyo Kazi Ingekusaidia Kwa Miaka Yote. Kama Hutatoa Mimba Naomba Uwe Unanijulisha Ili Nione Nini Cha Kukuombea Kwa MUNGU Akusaidie. Ila Kama Utatoa Mimba Hiyo Mimi Wala Usiwasiliane Na Mimi Kwa Lolote. Unaweza Ukaitoa Hiyo Mimba Kumbe Huyo Ndio Alikuwa Mtoto Wako Wa Mwisho. Tubu Kwa MUNGU Kwa Ajili Ya Dhambi Ya Uasherati, Kisha Zaa Mtoto Huyo Na Yamkini MUNGU Atakupa Kazi Nzuri baadae kama ukikaa kwenye kusudi lake.
Wewe Mche MUNGU Kwanza. MUNGU Anaweza Kukupa Neema Na Kazi Usifukuzwe Na Ukazaa Na Kurudi Kazini.
Baada ya majibu hayo niliyompa sikujua kilichoendelea , ila nilisukumwa rohoni kusema Neno hili.

" Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo ROHO akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza.-Yakobo 4:4-10

Inawezekana ni wewe ndugu unalidhalilisha Kanisa la MUNGU kwa sababu ya maovu yako.
Inawezekana Injili ya KRISTO inatukanwa kwa sababu ya matendo yako ya kishetani.
Inawezekana unawapendeza wanadamu lakini unamchukiza MUNGU na kumkana YESU KRISTO kwa sababu ya matendo yako ya kinafiki na dhambi.
Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.
Unatakiwa ufikie hatua ya kiimani ambayo hata iweje huwezi kumwacha Mwokozi YESU wala kumkana.



2 Kor 4:2 ''lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU.'

Leo kumekuwa na baadhi ya wakristo wa ajabu Sana.
Mtu yuko tayari kumwacha YESU ili apate mke au mume.
Mtu yuko tayari kumwacha YESU ili apate kazi.

Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO. 
 Mtu yuko tayari kumkana YESU ili aupendeze ulimwengu.


1 Yohana 2:22-23, ''Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa YESU ni KRISTO? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye BABA na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye BABA; amkiriye Mwana anaye BABA pia.'' 

Dada mmoja aliniandikia ujumbe akiomba nimuombee ili apate mume, nikamwambia anipigie muda fulani ili nimuombee lakini hakupiga, baada ya siku kadhaa akasema alisahau. Nikampa muda tena ili anipigie hakupiga, baada ya miezi kadhaa akaniandikia ujumbe akisema anakaribia kwenda kwa mganga ili apate mume, nilimwambia kwamba huko kwa mganga wake anaenda kupata majini tu, vifungo vya kipepo na maagano ya kishetani ambayo yatamtesa miaka mingi.
Mtu wa namna hii ni mfano hao wa watu wanaotaka kumkana YESU KRISTO ili waifuate miungu.
Leo ni rahisi tu kumwona mtu ameacha kumtumikia YESU KRISTO na sasa anamtumikia shetani kwa tamaa zake za kijinga.

Wapo watumishi leo wanahubiri watu kwamba hakuna jehanamu na hakuna mwisho wa dunia, wanafundisha hivyo ili wasikimbiwe na washirika maana dunia ya sasa imechafuka kwa dhambi.
Kuna watu wanafundisha leo kwa juhudi ya kwamba YESU hana Wokovu kwa wanadamu na bado watu hao wanajiita Kanisa, huo ni wenu wa kiroho.
Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.
Hawa  wanasababisha kazi ya MUNGU ya kweli inatukanwa.

2 Petro 2:1-2 '' Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata BWANA aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. ''

 Dada mwingine akanipigia simu siku moja akisema kila akipata mchumba baada ya muda mchumba wake anamwacha. Akasema " Kwanini Mtumishi kila nikipata mchumba baada ya muda mchumba huyo ananiona kama takataka na kuniacha?". Nikamuuliza maswali kadhaa na kati ya hayo maswali ni kwamba je alikuwa anafanya nao uasherati? Akajibu ni ndio tena wote. Nikamuuliza unajua madhara ya uasherati? Akasema hajui. Nikamwambia kwamba wanaume wale wanamuona takataka kwa sababu ni kweli yeye ni takataka kwa sababu ya kukubali kuwa takataka kwa Sababu ya yeye kukubali kutembea nao.
Hawa wote ni watu wa Kanisa na wanadai wanamjua YESU.

Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO. 
 Ndugu ambaye unasoma ujumbe huu nakushauri kwamba hakikisha kwamba ukiwa ndani ya Wokovu wa KRISTO unaifikia "A point of no return".
Hakikisha unafikia hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU wala kumkana.

Wagalatia 2:20 '' Nimesulibiwa pamoja na KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali KRISTO yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa MUNGU, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. ''
Andiko hilo hapo juu ndio sifa ya mtu ambaye hamkani YESU bali anamtii kama BWANA na MKOMBOZI wake. 

Wewe unayemwacha YESU kwa sababu ya kwenda kwa waganga wa kienyeji hakika wewe hukumjua YESU kamwe.
Wewe unayemwacha YESU kwa kufanya uzinzi au uasherati hakika wewe hukumjua YESU.
Wewe unayeisaliti imani ya Wokovu ili upate mambo ya kidunia, wewe hakika hukumjua YESU.
Wewe mtu wa Kanisa unayesilimishwa, wewe hakika tangu mwanzo hukuwa na mpango wa kwenda uzima wa milele.
Wewe mtumishi mwaminifu wa shetani ila umejificha Kanisani, hakika wewe hukumjua kamwe YESU KRISTO Mwokozi, humjua MUNGU Muumbaji na humjui ROHO MTAKATIFU.

Biblia takatifu inashuhudia kuhusu wewe ikisema ''Wanakiri ya kwamba wanamjua MUNGU, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.-Tito 1:16  ''
 
Wako watu ni kama pandikizi la shetani kwa Kanisa la MUNGU.
Ndugu nikushauri tu kwamba mtii KRISTO na Neno lake utaishi.
Hakikisha unafikia hatua ambayo huwezi kumwacha YESU wala kumkana.

Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.  
Nasema tena  Ndugu Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO. 
 2 Timotheo 2:11-13'' Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. ''

 Nakuonya wewe unayemwacha YESU kwa kutoa mimba, nakuonya wewe unayemwacha YESU kwa kuiba au kutoa rushwa, nakuonya wewe unayemwacha YESU kwa kuchukua mke au mume wa mtu.
Nakuonya wewe unayemwacha YESU kwa kuoa mke wa pili n.k
Kumbuka baada ya kifo chako kitakachofuata ni hukumu tu na sio vinginevyo

 Waebrania 9:27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; ''
 
Wewe unayemwacha YESU kwa kwenda kwa waganga au kuacha Wokovu hakika wewe hukumjua MUNGU wala YESU wala ROHO MTAKATIFU, Bali uliishia tu kujua dhehebu lako au uliishia tu kumjua mchungaji wako au nabii wako.

Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.  
Waefeso 5:11-12 " Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena."
Mteule uwe macho maana hizi ni siku za mwisho.
Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.
Ndugu, sasa ni wakati wa kujikana mwenyewe.
Kama kuna rafiki anakushawishi mkazini ni heri kukataa na kuvunja naye urafiki.
Kama Mchumba wako anakushawishi mzini hakikisha unamshtaki kwa Mchugaji na vunja uchumba naye, usiruhusu muwe chumbani wawili tu wakati nyie sio mke na mume.
Ni wakati wa kujikana mwenyewe ili tu usimkose KRISTO YESU.
Kama ni ndugu yako nataka kukupeleka kwa waganga wa kienyeji kataa na kimbilia kanisani.
Kama unaiba kazini kwako acha kuiba, kama unaisaliti ndoa yako acha kuanzia leo, kama wewe ni mnywa pombe acha kuanzia leo, kama wewe ni mchawi au tapeli acha kuanzia leo.
Ni wakati wa kujikana mwenyewe ili tu umapte KRISTO.
Kumbuka wanadamu mwisho wa urafiki na wewe ni kaburini tu siku ukifa hivyo mtafute YESU KRISTO rafiki mwaminifu ambaye ukimtii yeye na Neno lake hakika utakuwa na yeye milele katika uzima wa milele.
Ndugu, ni wakati wa kujikana mwenyewe ili umpate YESU KRISTO.
Kama mke wako au mume wako ndio anataka kukukosesha uzima wa milele usikubali ndugu.
Ni wakati wa kujikana mwenyewe ili uupate uzima wa milele katika KRISTO YESU.
 Mathayo 16:24-27 ''Wakati huo YESU aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa BABA yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.''

Ndugu usikubali kinywa chako kikakukosesha uzima wa milele kwa uongo, acha dhambi hiyo na anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu.
Kama sehemu zako za siri ndizo zinataka kukukosesha uzima wa milele, ndugu usikubali na jitenge na dhambi hiyo.
Kama ukoo wako au familia yako ndio wanataka kukukosesha hakikisha hukubali.
Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.
 Wakolosai 3:5 ''Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;''.
Ndugu okoka na kataa dhambi zote na kuziacha kama kweli unamhitaji YESU KRISTO kuwa Mwokozi wako kwa ajili ya uzima wa milele.
 Kumbuka huu ni wakati wa neema hivyo usiichezee neema ya MUNGU kwako.
Tito 2:11-13 '' Maana neema ya MUNGU iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu;''
 Ndugu tengeneza maisha yako maana YESU KRISTO yu karibu sana kurudi.
Ndugu, Mkristo unatakiwa ufikie hatua ambayo huwezi kamwe kumwacha YESU KRISTO.
 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa.-Ufunuo 3:22 ''
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu. Ukiweza pia toa copy na kuwasambazia watu wengi zaidi.

Comments