PETER MABULA;KUTOKA KWA MARAFIKI ZANGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Hizi ni meseji za facebook, Whatsapp na email nilizotumiwa na baadhi ya marafiki zangu ambao hufuatilia masomo yangu mitandaoni.
Namshukuru MUNGU maana mpaka leo nimeshaandika masomo 860 na namshukuru Bwana YESU pia maana maelfu wamefunguliwa na yeye kupitia huduma hii.
Namshukuru sana ROHO MTAKATIFU ambye ndiye  analiongoza Kanisa la KRISTO duniani.
Bwana YESU anasema  '' Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. -Yohana 14:26-27 '' 

Hizi hapa baadhi ya meseji kutoka kwa baadhi ya marafiki zangu.

Mtu wa kwanza:
 
Bwana asifiwe Mtumishi Mabula!
Leo nimesoma lile somo ulilotuma kuhusu majini mahaba muda naomba yale maombi nikasikia maumivu makali yanakatiza kifuani nikaendelea kuomba ghafla kikaja kizungu zungu ambacho kinanifanya nisione vizuri nikasema nijitahidi kuendelea kusali ile hali ikapotea yakabaki maumivu upande wa kulia ila sasa yameenda yanaisha naamini Mungu kanifungua, kwani nilikuwa nateseka Sana kuota ndoto za kufanya mapenzi na watu ninao wajua na nisio wajua nazani hili ndio lilikuwa tatizo kubwa linalopelekea mie kuwa na ugomvi kwenye mahusiano yangu. MUNGU AKUBARIKI UENDELEE KUFUNULIWA MAANA UNATUSAIDIA SANA


Mtu wa pili
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Bwana
Mimi nakaa Arusha,nimepitia page yako ya maisha ya ushindi nimekutana na artcle ya majini mahaba
Nimekuwa nikisumbuliwa na haya majini kwa muda marefu sana, nimezisoma na kuelewa mambo ya kufanya na maombi ili kuvunja hizo ndoa
Mtumishi wa Bwana maombi nimefanya na ninaendelea kufanya na deliverence nimefanyiwa na watumishi wa Mungu mara nyingi zikiambatana na sadaka
Lakini bado nimekuwa nikisumbuliwa na hizi ndoto
Mtumishi wa Mungu naomba unisaidie kuomba Bwana Mungu afunue ni kitu gani kinawapa uhalali kwangu mpaka kungangania na kutoyachilia maisha yangu nimeteseka kwa muda mrefu sana na mimi niwe huru katika Kristo Yesu
Mimi nimeokoka na nimemkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu
Naomba nisaidie mtumishi wa Bwana

Mtu wa tatu:
Haujambo Mtumishi Katika Jina Tukufu La Bwana Na Mwokozi Wetu Yesu
Kristo, Shukurani Zangu Kwako Nilipokuwa Nazoezi Yakusoma Soma Mambo
Fulani Fulani Kwenye Mtandao, Nimebahatika Kusoma Fundisho Katika
Maisha Ya Ushindi Lisema: Je Wewe Ni Mtauwa? Somo Ambalo
Limenifurahisha Na Nimelielewa Zaidi Kuhusu Utauwa Na Mtauwa,
Ninachokuomba Ni Kwamba Uzidi Kunitumia Masomo Mengine Mengi Na Anwani
Yenu Kwa Mawasiliano Zaidi. Asante Jbarikiwe.


Mtu wa Nne:
Bwana Yesu asifiwe! Mimi natokea Congo. Mimi nina tatizo, tatizo langu huwa Naoto ndoto ambazo hazieleweki, huwa sielewi ndoto hizo. Kila siku nikiwa nimelala naota ndoto za ajabu ajabu tu. Nashindwa kuelewa kwanini hata huwa sipendi usiku ufike maana naota ndoto mbaya sana. Mara nafukuzwa na watu amabo siwajui mara nalishwa vitu [chakula]. Mimi nampenda sana Yesu nataka kuokoka nakuishi maisha matakatifu ila nina tatizo pia, hapa nilipo kila kanisa ninaloenda naona kuna vitu vibaya, amabvyo havimpendezi Mungu, na bado sijabatizwa. Na pia naumwa, nilienda kwa doctor lakini doctor kakosa ugojwa naambiwa sina ugojwa lakini nateseka. Kichwa kinaniuma sana na mwili unakua kama nimeungua mgongo unauma miguu inawaka moto na mgongo pia. Nina kama miezi 8 au 9 nahuo ugojwa. Naomba lakini sioni mabadiliko yoyote. Hayo ndo matatizo yangu, siku hizi huwa sipendi usiku ufike maana mara tu nilalapo, naota ndoto mbaya, na cha ajabu ninapo amka huwa sikumbuki hizo ndoto, huwa nakumbuka kidogo tu, sikumbuki mwanzo mpaka mwisho wa ndoto nilioota. Mungu akubariki sana


Majibu ya Peter Mabula kwa ndugu huyo kutoka Congo:
MUNGU akubariki Sana.
Naomba endelea kujifunza Neno la MUNGU na Maombi.
Jiunge na kanisa la Wokovu lililopo karibu na wewe hakika utafunguliwa, wewe una nguvu za giza ndani yako na uko katika vifungo hivyo ni lazima uwe mshirika kanisani, jitahidi sana kwa hilo. Pia naomba uniandikie ujumbe WhatsApp namba +255714252292 ili nitafute nafasi ya kukuombea na MUNGU atakutendea mema, ila hakikisha unaokoka na watumishi wa MUNGU huko uliko, hiyo ni muhimu sana.
MUNGU akubariki


Mtu wa Tano:
Bwana YESU apewe sifa Mtumishi Peter Mabula,
Asubuhi ya leo nikiwa njiani kuelekea kazini, nikakutana na somo hilo hapo mtandaoni Kuhusu Maonyo, kila lilioelezwa hapo lilinigusa sana, nilihisi kuumia hadi moyoni kabisa.

Nilikuwa na mchumba, nikashindwa kuvumilia na sasa yeye ni mjamzito kabla hata ya ndoa,
kuna wakati inabidi nitumie njia fulani zisizo halali ili kujipatia kipato cha ziada hapa kazini kwa kuwa mshahara ni mdogo na madeni ni mengi,
Lakini Namshukuru MUNGU kwa neema aliyonipa ya kuiona hata siku ya leo na kusoma ujumbe huu, MUNGU anisamehe, nishauri kwa hayo mambo mawili hapo juu Mtumishi.
MUNGU akubariki kwa masomo haya.




Mtu wa sita:
Bwana asifiwe!
mchungaji nina jambo nahitaji unijuze kwa maana bado sijakuwa kiroho kutokana na kutopatikana kwa huduma bora ya MUNGU mahali ninapoishi,siyo kwamba nadharau ila huduma hainijengi kiroho,na ndio maana naitafuta huduma bora mpaka mitandaoni,na ninajengwa na huduma yako,
sasa iko hivi kabla sijampokea YESU Kristo mimi tayari nilisha kuwa "nimeowa" yaani nina mwanamke ananiita mme kutokana na hali fulani ya mazingira ninayoishi,na sisi wote wawili mpaka sasa tumeokoka,ila mke wangu alitangulia kuokoka kabla yangu na aliokoka kabla ya ndoa yetu ya kimila ila mimi niliokoka baada ya ndoa! sasa naomba unifahamishe kuhusu hii ndoa iko vipi katika KRISTO??


MAJIBU YA MTUMISHI PETER MABULA.
Ndoa yako ni ndoa halisi. Unachoweza kufanya ni kuibariki tu hiyo ndoa.

Hizi zote ni ndoa halali.
1. Ndoa ya Kanisani.
2. Ndoa ya kiserikali.
3. Ndoa ya kimila au kitamaduni, ila tu isiwe ndoa ya kuoa mke zaidi ya mmoja. Ila kama mtu ameshamjua MUNGU na anahitaji kuoa basi ni sheria ya kiroho kwake kufunga ndoa Kanisani, Wakolosai 3:17-19 " Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye. Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika BWANA. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao."

  Hivyo kwa mtu ambaye ameshaokoka haimpasi tena kufunga ndoa za kimila Bali afunge ndoa Kanisani. Wewe uwe na amani maana uko katika ndoa sahihi mbele za MUNGU, Mnaweza tu kubariki ndoa yenu. Wale wote ambao walioana kipindi hawajamjua YESU sio kwamba ndoa zao ni feki. MUNGU akubariki na songeni mbele na YESU Mwokozi hadi uzima wa milele. MUNGU akubariki.

Mtu wa saba:
 Salamu mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU KRISTO ahsante sana mtumishi ubarikiwe sana sana maana karibia kila somo utakalotoa linanigusa sana kuhusiana na maisha yangu kwa hakika MUNGU amekuleta hapa kwa kusudi uitie nguvu mioyo minyonge niliteswa sana na vifungo vya kipepo lakini sasa YESU amenifungua ahsante kwa maombi yako UBARIKIWE

Mtu wa nane:
Bwana YESU Kristo asifiwe ndugu Peter M.Mabula? nikiwa mmoja wa wanafunzi wako kutoka kenya,pokea salamu zangu katika mwaka huu.Tangu nianze kusoma masomo yako kupitia mtandao yamenijenga na kunibadilisha katika safari yangu ya wokovu. Najisikia ni mwenye matumaini kwa nafasi ambayo Mungu ananizawadi kila siku nakunionya ile nitengeneze maisha na uhusiano wangu wa wakwake kupitia masomo yako ndugu; Mungu akubariki na akutie nguvu na kukupa maisha marefu ili Huduma ipanuke hataye yale ambayo hatuja yajua na tunastahili kuyajua kupitia wewe tukayafahamu. Wewe ni kati ya walimu wachache ambao hawaligushi Neno la Mungu bali unafundisha njia sahihi ya kumuona Mungu. Mungu akubariki sana.Ni mimi mwanafunzi wako ,kutoka Kenya(Malindi in Kilifi county)
Pia ndugu mabula naomba msaada wako kwa mafundisho haya:-
-wokovu na kukombolewa,na katika kukombolewa;je ni nani anastahili kukombolewa?,na ni nani anakomboa?,je ni kipi Yesu hakumaliza ndio mwanadamu akikomboe? na je nini maana ya sadaka ya ukombozi? ni halali kutoa sadaka ya ukombozi? ahsante na Mungu akubariki unapo liandaa kwa hili somo.


Mtu wa tisa:
Habari zebu Ndugu Yangu. Nina matumaini mazungumzo Kati yetu ni ya siri
Kama naweza kukuamini niweze kuongea Nawe kwani Mahala nimefika ni pagumu na hata ninavyoandika haya nilipata ukurasa wako Katika tovuti nikiwa Katika harakati za Kusaka mganga WA kunisaidia kwani nipo mahali pabaya mno maisha ni hivi
Mambo yangu yalienda mrama nilipotoka kwa mganga. Nimepata ajali mbili za barabarani. Gari sina tena na afya sio nzuri. Niombeeni tafadhali.


MAJIBU YA MTUMISHI PETER MABULA.
Ubarikiwe ndugu na usiende tena kwa mganga yeyote ili usife, ujumbe wa kila mtu ni siri kwa sababu nafuta jina la mtu husika na hata baadhi ya maeneo yafuta ili ujumbe uwe fundisho tu kwa wengi, na sio kumtangaza mtu ili watu wamjue, uwe na amani. Pia Pole kwa hayo ndugu, nakuomba sasa tafuta Kanisa la kiroho uokoke, nasi tutakuombea kwa juhudi na MUNGU atakusaidia. Ni muhimu sana ujiunge na kanisa maana umefungwa na waganga uchawi utakaokutesa sana hadi uende kanisani kuombewa na kufunguliwa. Naamini utashinda, zingatia na ubarikiwe sana


Mtu wa kumi:
Mtumishi nashukuru kwa Masomo yako maana nimejifunza mengi na nimefunguliwa mengi tangu nimeanza kupata masomo yako, pia leo nilikua nataka kukushirikisha jambo linalonisumbua lakin Roho mtakatifu amenikumbusha nisome somo lako linalosema JINSI YA KUTOKA KWENYE Vifungo vya Giza, hivyo nimepata ufumbuzi wa yale yalikua yananitesa, hivyo ubarikiwe Mtumishi maana naona kufunguliwa


Mtu wa kumi na moja:
Mtumishi Bwana Yesu asifiwe mimi nimeokoka na ninampenda Yesu sana.Kuna swali nimekutana nalo kwakeli nimeshindwa kulijibu kwa usahihi swali lenyewe ni hili[nini tofauti ya Roho na Nafsi na zinavyofanya kazi]


MAJIBU YA MTUMISHI PETER MABULA:
Nafsi ni sehemu ya nje ya utu wa ndani wa mwanadamu.

Roho ni sehemu ya ndani ya utu wa ndani wa mwanadamu.

Mtu wa kumi na mbili:
Bwana Yesu asifiwe mchungaji. mimi ndoto zinazonisumbua ni za watu walio kufa.
kuna siku niliota tumekwenda kuzika makaburini gafla maiti akatoka kwenye jeneza na kumkumbatia mke wake gafla akaanza kutukimbza watu walio kuwa wamekusanyika katika mazishi.
je mtumishi wa Mungu kipi ni fanye?
pia wakati mwingine huwa kuna vitu huwa vinanikaba wakati wa usiku. kiukweli ndoto hizi huwa zinanisumbua sana. napia hunifanya ata wakati mwingne kuogopa.


MAJIBU YA MTUMISHI PETER MABULA:
Kukabwa ni kuvamiwa na nguvu za Giza.
kuota aliyekufa maana yake roho ya mauti inafuatilia ili wengine wafe, pia ni roho ya uharibifu inafuatilia.
haribu roho za nyoka maishani mwako.
Nyoka kwenye ndoto huwakilisha
-roho ya uongo.
-huwakilisha pia shetani mwenyewe.
-Huwakilisha mizimu.
-Huwakilisha uchawi
-Huwakilisha uganga wa kienyeji.
-Huwakilisha unajimu pia na machukizo mengine mengi.
Unaweza ukaota nyoka anakukimbiza kumbe maana yake ni kwamba wachawi wanataka kukuangamiza na maana nyingine ni kwamba uko kwenye eneo ambalo shetani ametawala sana hivyo uwe makini.
Unaweza ukaota nyoka anazunguka sehemu kumbe maana yake kuna uongo mkubwa utanenewa wewe ambao uongo huo unaweza ukaleta madhara makubwa maishani mwako.
Kumezwa na nyoka ndio kabisa kumwezwa au kuzidiwa na nguvu za Giza.

MUNGU akubariki uliyesoma na najua kuna kitu hata kama ni kidogo umejifunza, pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu. Ukiweza pia toa copy na kuwasambazia watu wengi zaidi.

Comments