USIKUBALI KUDANGANYWA NA WAPINGA KRISTO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.Kuna maunganiko mawili ya kudumu na ya muhimu sana katika maisha ya wateule wa MUNGU.
1. Unganiko la kindoa kati ya Mume na Mke waliofunga ndoa takatifu.
Marko 10:7 "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja."


2. Unganiko kati ya Mwanadamu na YESU KRISTO.

1 Wakorintho 6:17 " Lakini yeye aliyeungwa na Bwana(YESU KRISTO) ni roho moja naye.''

Maunganiko haya ni muhimu sana.
Unganiko kati ya mume na mke walio wanandoa ni unganiko ambalo wahusika hawatakiwi kuruhusu unganiko hivyo kuvunjika.
Unganiko hilo linawahusu walio katika ndoa sasa na litaanza kukuhusu pia na wewe utakapoingia katika ndoa.

Unganiko kati ya Bwana YESU na wewe mteule wake ni unganiko la kiroho baada ya wewe kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako, Biblia inasema kwamba wewe uliyeokolewa na Bwana YESU ni roho moja na Bwana YESU maana yake YESU kupitia ROHO MTAKATIFU anaingia ndani yako na kufanya makazi, kukuongoza na kukufundisha utakatifu. Tena unapompokea YESU ujue umempokea na MUNGU Mwenyezi
Ufunuo 3:20 " Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami."

Maunganiko haya yanatakiwa kuwa ya kudumu.
Sasa ninachotaka kukueleza Leo ni hiki.
Marko 10:9 "Basi alichokiunganisha MUNGU, mwanadamu asikitenganishe."

Alichokiunganisha MUNGU mwanadamu asikitenganishe.
MUNGU alikuunganisha wewe na Mwanaye wa pekee YESU KRISTO ili wewe uwe wa KRISTO milele katika ufalme wa MUNGU.
Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

 
Ndugu, alichokiunganisha MUNGU hakikisha mwanadamu hakitenganishi.
Kanisa la KRISTO limeungwa na KRISTO hivyo wewe uliye Kanisa hai uliyeokoka na kuungwa na KRISTO hakikisha wanadamu hawakutenganishi na YESU KRISTO Mwokozi wako.
Mteule hakikisha shetani na mawakala zake wote hawakutenganishi wewe na YESU Mwokozi.
Alichokiunganisha MUNGU cha Wokovu mwanadamu asikitenganishe.
Usikubali kumwacha YESU Mwokozi kwa kudanganywa na wanadamu.
Wewe unayebadili imani kwa kumwacha YESU Mwokozi ujue unajipeleka jehanamu kimya kimya.
Wewe unayedanganywa kwamba MUNGU ni mmoja hivyo hamia tu hata imani ya mashetani kumbuka kwamba hata shetani ni mmoja na huyo shetani wengi sana humwabudu wakimwita mwenyezi Mungu na kumbe sio MUNGU wa mbinguni bali ni shetani mwenye malaika zake majini, mizimu na wakuu wa Giza, ndugu ukimwacha YESU ujue umemwacha MUNGU wa mbinguni, ukimwacha YESU ujue umeiacha njia pekee ya uzima wa milele.
Hakikisha Alichokiunganisha MUNGU cha Wokovu, mwanadamu hakitenganishe.


  Siku moja usiku Bwana YESU Alinitokea Na Kuniambia Maneno Haya "NITAKUJA KUTENGANISHA WATU WALIO KONDOO NA WALIO MBUZI KAMA NENO LANGU LINAVYOSEMA KATIKA MATHAYO 25:31-34"
Muda Huo Huo Nilianza Kujiombea roho Yangu Maana Kondoo Ni Watakaoingia Uzima Wa Milele Na Mbuzi Ni Watu Watakaokwenda Jehanamu. Kisha Nilikuwa Tayari Kuupeleka Ujumbe Huo Kwa Kila Rafiki Yangu Na Ndugu Yangu. Kibinadamu Mimi Nisingekuwa Na Ujasiri Wa Kukuambia Wewe Ila Aliyesema Ni YESU KRISTO. Kondoo Ni Watu Watakatifu Katika KRISTO, Waliobaki Wote Ndio Mbuzi. Mimi Sijui Kama Wewe Ni Kondoo Au Ni Mbuzi. Yu Karibu Hakika.
Ndugu nakuomba sana sana mpokee YESU kama hujampokea.
Nakuomba sana sana wewe uliyempokea YESU basi ishi maisha matakatifu.
Bwana YESU kwa sauti yake amesema Hawahitaji wanafiki yaani walioko kanisani ili hawayatendi yaliyo ya MUNGU.
Ndugu yangu, Mimi najua ni Neema ya MUNGU Mimi kukuletea ujumbe huu kama ilivyokuwa Neema ya MUNGU kwangu kwa Mwokozi YESU kunitokea na kuniambia haya, kwa ajili yangu na kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki zangu wote.
Hiyo Mathayo 25:31-34 inasema hivi " Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;"

Ndugu yangu, kama una masikio ya kusikia basi basi lisikie Neno hili la Bwana analokuambia, okoka na acha dhambi zote, anza kuishi maisha matakatifu.
Na hata ukisoma
Mathayo 25:41 Biblia inasema " Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto(yaani walio mbuzi), Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;"

Mwenye sikio la kusikia na asikie Leo kile ambacho Bwana YESU anamwambia.
Angalieni mtu asiwadanganye kwa lolote maana wengi watakuja wakisema wao  nao watadanganya wengi.
Bwana YESU alipoyasema hayo kilikuwa kipindi ambavyo hakuna dini nyingine ya Leo iliyokuwepo nje na Wokovu wake.
Aliyasema hayo kipindi ambacho hakukukuwa na dhehebu lolote la Leo ambalo linalohubiri watu kumkataa YESU na Wokovu wake.
Bwana YESU aliposema kwamba watakuja wakijiita Kristo maana yake, Kwanza KRISTO maana yake masihi au mpakwa mafuta wa MUNGU yaani aliyeteuliwa na MUNGU. Mtu huyo anaweza kujiita masihi au asijiite masihi lakini atakuja na kuwafundisha watu njia nyingine kwa ajili ya uzima wa milele, wakati ukweli ni kwamba hakuna njia nyingine nje na Wokovu wa KRISTO(Matendo 4:12)
Watu hawa Lengo lao ni moja tu kuwafanya watu wasimtii MUNGU katika KRISTO YESU.

2 Yohana 1:7-11 '' Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa YESU KRISTO  yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.  Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya KRISTO, yeye hana MUNGU. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba(MUNGU) na Mwana(YESU KRISTO) pia. Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu. ''
 
Ndugu inawezekana ni wewe sasa uko katika dini au dhehebu wanaomkataa YESU KRISTO kama Mwokozi, wewe uko kwa makristo na sio kwa KRISTO, undoka huko na uokoke Leo.
Inawezekana wewe uko dhehebu ambalo viongozi huko wanasema hakuna jehanamu, ndugu hao wanakufariji uongo maana labda ni wao wameichagua hiyo jehanamu hivyo wanataka wakurubuni na wewe ili usimche MUNGU Baba katika KRISTO YESU Mwokozi, nakuomba Ndugu mpokee YESU Leo kama Mwokozi wako, acha dhambi zako zote na anza sasa kuishi maisha matakatifu ya Wokovu.
Mathayo 24:4-14 " YESU akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni KRISTO; nao watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja."

Mwenye sikio la kusikia na asikie Leo na kumpokea YESU kama Mwokozi wake, na kuanza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu.

Wewe ni nafsi iliyo hai kiroho au ni nafsi iliyokufa kiroho?
Nafsi iliyokufa kiroho haisikii injili, haielewi sauti ya MUNGU ya ndani ya Neno la MUNGU, haiachi dhambi, haina utii wala unyenyekevu kwa MUNGU, imejaa kiburi na majivuno.
Ndugu kumbuka kwamba MUNGU sio wa vitu vilivyokufa, MUNGU sio wa nafsi zilizokufa kiroho, hivyo inakupasa kufufuka Leo kutoka hiyo mauti ya kiroho ya dhambi na maovu.
Ezekieli 18:20-22 "Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi."

Mama, Baba, kaka, Dada, ndugu, rafiki, mwanamke au mwanaume naamini umeelewa sasa Neno la MUNGU linalokukataza dhambi.
Kijana au mzee naamini sasa umeelewa nini MUNGU anataka ufanye.
YESU KRISTO anakungoja utubu na kumpokea kisha uache dhambi zako zote ndipo uhusike na uzima wa milele.

'' Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. -Ufunuo 2:11''

Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments