WATOTO WA MUNGU NISIKILIZENI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
MUNGU ni Baba mzazi wa roho zetu, hii ni kweli kabisa.
Kila mmoja anamuita MUNGU kwamba ni Baba wa mbinguni, ni kweli kabisa maana hata Biblia inasema kwamba MUNGU ni Baba mzazi wa roho zetu aliyezuzaa kwa Neno lake katika KRISTO YESU.


Yakobo 1:18 ''Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.''


YESU alikuja kuurudisha uhusiano wetu na Baba yetu wa mbinguni uliokuwa umevunjika tangu Adamu na Eva walipokosea, ndio maana Biblia inasema kwamba YESU alitupa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU.

Yohana 1:12-13 ''Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''


Hakika tu watoto wa MUNGU na MUNGU ni Baba yetu mzazi wa roho zetu.
Na Biblia iko wazi sana kwamba wateule wa KRISTO tutang'aa kama jua katika ufalme wa BABA yetu wa mbinguni.


Mathayo 13:43 ''Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa BABA yao. Mwenye masikio, na asikie.''


Na katika maisha haya MUNGU Baba mwenyewe anatuambia kwamba tuyaache machukizo ya dunia, tumkatae shetani na kazi zake ndipo MUNGU atakuwa Baba yetu safi na sisi tutakuwa watoto wake.
Tena MUNGU hana ubaguzi kabisa bali wote yaani wanaume na wanawake hakika tukimpokea YESU KRISTO kama Mwokozi tunakuwa watoto wa MUNGU.


2 Kor 6:17-18 ''Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, ''


Sasa nisikilize ewe Mwana wa MUNGU mwenzangu.

Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama humtii kama Baba mzazi wa roho yako?
jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe umemwacha YESU na kufuata miungu tena ni wewe unafanya kampeni sasa ili kuliangusha Kanisa la MUNGU?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe ni kahaba?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe unaisaliti ndoa yako kwa siri?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe huwa unaenda kwa waganga wa kienyeji?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa umeacha Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe unavaa kikahaba?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe ni mwasherati au mzinzi?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama sasa wewe unafanya ibada za wafu na kutambika?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe ni muongo, tapeli, mwizi na mtoa rushwa?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa huhubiri tena injili ya KRISTO bali siku zote unahubiri yasiyo ya MUNGU?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama sasa wewe ni mnywa pombe tena humtaki tena YESU anayeokoa?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama sasa wewe ni mvuta sigara au bangi?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe umetorosha mwanamke au wewe mwanamke umekubali kutoroshwa na mwanaume kwa tamaa zako?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe umeacha kumtumikia KRISTO na umeanza kuimba nyimbo za kidunia?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe umetekwa na mambo ya kidunia yaliyo machukizo?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama kwa sasa wewe umetekwa na roho ya Yezebeli?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama unaabudu shetani?
Jibu ni si kweli.


Je MUNGU abaki kuwa Baba yako hata kama unawachukia watumishi waaminifu wa MUNGU na unawatukana na kuwasema vibaya?
Jibu ni si kweli.


MUNGU Baba leo anasema na wewe maneno haya '' Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa. Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi. Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; je! Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi.- Malaki 1:6-9 ''


Ndugu, kama kweli uko katika KRISTO YESU na MUNGU ni Baba yako basi anza sasa kumcha yeye na tii Neno lake.
Ishi maisha matakatifu, acha dhambi zote na machukizo.


1 Petro 1:17''Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.''

 
"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa.-Ufunuo 3:22 ''
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu. Ukiweza pia toa copy na kuwasambazia watu wengi zaidi.

Comments