ZAWADI TATU ALIZOPEWA BWANA YESU

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Bwana YESU alipoamua kuja duniani kuwaokoa wanadamu aliamua kuchagua tumbo la bikra Mariamu. 
YESU alipozaliwa sio kwamba ndio alikuwa anaanza kuishi bali hiyo ilikuwa ni njia tu ya kupitia ili kuja kutupa uzima wa milele.
Biblia inasema YESU alikuwepo mbinguni tangu milele.
Mika 5:2 '' Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.''
 
Sasa siku anazaliwa kuna mambo yaliyokea, moja ya mambo hayo ni zawadi alizopewa YESU siku hiyo.
Ngoja niseme machache kwa ajili ya zawadi tatu ambazo Bwana YESI alipewa siku anazaliwa.


Mathayo 2:11 '' Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.'' 
 
Zawadi alizopewa ni Dhabahu, Uvumba na Manemane.

 
1. DHAHABU iliwakilisha Ufalme, hivyo YESU angekuwa Mfalme na yeye sio Mfalme tu bali ni Mfalme wa wafalme wote milele, ndivyo Biblia inasema kwamba YESU KRISTO ni Mfalme wa wafalme.


Ufunuo 1:5-6 '' tena zitokazo kwa YESU KRISTO, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina. ''

2. UVUMBA uliwakilisha ukuhani, maana ni makuhani tu waliotumia uvumba katika shughuli za ibada, Zawadi ya uvumba ilijulisha kwamba YESU ni kuhani. Na Biblia inasema YESU ni Kuhani mkuu 

Waebrania 8:1 ''Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,''

3. MANEMANE iliwakilisha kifo, hivyo zawadi hiyo ilijulisha kwamba siku moja YESU atakufa, ni ukweli kwamba Bwana YESU alikufa mara moja tu ili atukamilishie Wokovu wetu

 1 Kor 15:3-4''Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;  na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; ''
 
Hata Yeye Bwana YESU alithibitisha hilo baadae akisema 


'' Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu.-Luka 24:7''

Ndugu uliyeokolewa na Bwana YESU, ni kweli hauko chini ya sheria, ni kweli kabisa, lakini uko chini ya mamlaka ya KRISTO YESU Mwokozi ambaye ana mamlaka yote mbinguni na duniani.
Mathayo 28:18 " YESU akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani."


Kazi yako kama Mteule wa MUNGU ni kuhakikisha una mtii KRISTO na Neno lake ili umpendeze MUNGU.

2 Yohana 1:9-11 " Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya KRISTO, yeye hana MUNGU. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba(MUNGU) na Mwana(YESU) pia. Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu."

Ndugu hakikisha unamtii YESU KRISTO, na njia ya kumtii ni kulitii Neno lake, ndipo utakuwa chini ya mamlaka yake na kwa njia
utampendeza MUNGU Baba Hakikisha unadumu sana katika fundisho la KRISTO. Hakikisha unampendeza MUNGU Baba kwa wewe kuzingatia injili ya Wokovu wake.

 Sisi tuliookoka tuko hai kwa sababu YESU KRISTO Mwokozi wetu yu hai milele. Uzima tulio nao sasa ni katika YESU KRISTO Mwokozi aliyetuokoa.
Si mimi tena bali ni KRISTO yu hai ndani yangu, sio sisi tena bali ni KRISTO YESU yu hai ndani yetu.
Uhai tulionao sasa tumeupata katika Mwana wa MUNGU aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu tunaomtii.


Wagalatia 2:20 '' Nimesulibiwa pamoja na KRISTO; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali KRISTO yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa MUNGU, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.''

 
Ni hai sasa, maisha yangu yatakuwa hai, ndoa yangu itakuwa hai, baraka zangu zitakuwa hai huduma yangu itakuwa hai siku zote kwa sababu YESU KRISTO ndiye Mwokozi wangu na Mwokozi wangu siku zote milele yuko hai.
Mimi niko hai sasa kwa sababu ROHO MTAKATIFI yuko ndani yangu na ndiye kiongozi wangu.
Mimi ni hai sasa kwa sababu ninamwabudu MUNGU Baba Mwenyezi , ni hai sasa kwa sababu Mwokozi wangu ni YESU KRISTO aliye hai.
Ni hai ni hai hai haiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Namtukuza sana MUNGU Baba.
Najua YESU alikonitoa ndio maana leo namtukuza.
Ndugu ikiwa YESU KRISTO ni Mwokozi wako na unaishi maisha matakatifu katika yeye hakika una kila sababu ya kumtukuza MUNGU wa mbinguni.
Kama hujaokoka basi hakikisha unaokoka leo.

Kumbuka  '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.- Yohana 3:16-21  ''
 Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments