![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Ujumbe huu naomba umsaidie kila anayeshiriki uovu huu, na wewe ambaye hauhusiki na uovu huu basi ujumbe huu ukupe maarifa ya kiroho ya kuwasaidia wengine watakaokushirikisha juu ya kitendo hicho kiovu wafanyacho.
✓✓Kwa kuanza ni kwamba punyeto kwa wanaume na usagaji au kujisaga kwa wanawake Matendo haya ni dhambi na chanzo chake ni roho za Shetani za uchafu wa kiroho.
Ufunuo 16:13 "Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo."
roho za uchafu za shetani utendaji wake upo maeneo mengi baadhi ni pamoja na punyeto na usagaji.
Biblia mahali pengine uchafu huu inauita uchafu wa kutamani.
Waefeso 5:3 " Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;"
Uchafu huu huanza kwa Mtu kushawishiwa kwa kutazama au kuambiwa na watu.
Kitendo hicho kina madhara makubwa kiroho, kimwili, kihisia na kimaisha.
Lakini kwa Wewe uliyekamatwa na roho hizo za shetani za usagaji na punyeto, ukiamua YESU KRISTO anaweza akakuondolea roho hizo chafu.
Ni ahadi kwenye Neno lake kwamba atafukuza roho za uchafu wa kiroho ambazo mojawapo ni usagaji na punyeto.
Zekaria 13:2 "Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia NITAWAFUKUZA manabii, na roho YA UCHAFU, watoke katika nchi."
Kupiga punyeto kwa mwanaume au kujichua/kujisaga kwa mwanamke ina maana sawa, ni kitendo cha mtu kujichezea sehemu zake za siri kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.
Kwa Mwanamke pia ni kitendo Cha Mwanamke mmoja kujifanya Mwanaume kimahaba ili kumlidhisha Mwanamke mwenzake kingono kwa kutumia mwili au vidole au vifaa vya kutengenezwa.
Mama mmoja ambaye ni mtumishi Kanisani kwao aliniandikia ujumbe huu ambao ulipelekea somo hili.
Aliandika hivi;
" Habari za uzima Mtumishi Mabula.
Nimekuwa wa kuchezea sehemu zangu za siri kwenye eneo linaloitwa kinena na kunipelekea kusikia raha na kufika kileleni kana kwamba nimetenda tendo la ndoa na mume wangu, na mara nyingi nikishiriki na mume wangu huwa sifikii hii hali. Sasa moyo wangu unauma sana maana ni dhambi na dhambi hii sitaki ikanifanya nikakosa mbingu, isitoshe mimi ni mtumishi.
Na nimekuwa kwenye dhambi hii kwa muda mrefu sana.
Naomba msaada wako na ushauri pia"
Baada ya mama Huyo kuniandikia hivyo nilimjibu kama nilivyojaliwa lakini sio yeye tu ambaye amewahi kuniuliza juu ya punyeto au kujichua, wapo watu wengi na nataka nitumie nafasi hii kuwasaidia kiroho.
Biblia kwa Kanisa la MUNGU inasema "jitengeni na ubaya wa kila namna. MUNGU wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu YESU KRISTO.-1 Thesalonike 5:22-23"
Ubaya wa kila namna tunaopaswa kujitenga nao ni pamoja na punyeto na kujichua au Usagaji.
Yako madhara mengi ya punyeto na kujichua, baadhi ya madhara kwa anayeshiriki kitendo hiki kichafu ni;
1. Ni ishara ya kwamba mtu huyo ana mapepo na vifungo vya giza Vingi.
2. Hicho ni kifungo cha kumzuilia mtu kuolewa au kuoa, au akiwa ndani ya ndoa ni kitendo ambacho kitamfanya asiifurahie ndoa yake.
3. Kitendo hicho ni dhambi mbele za MUNGU.
4. Kama hujaingia katika ndoa ujue huwezi kumuomba MUNGU akupe Mume/Mke mwema na akakupa hadi uache hiyo tabia chafu.
5. Hiyo ni ishara kwamba wewe ni wa shetani na unamilikiwa na malikia wa kuzimu.
Biblia inasema katika Waefeso 5:3 kwamba " Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;"
✓✓Kumbe punyeto na kujichua ni uchafua unaoendana na kutamani.
Biblia inasema Watakatifu haiwapasi kuhusika na uzinifu wala uchafu unaotokana na kutamani.
Bila kutamani haiwezekani mtu kupiga punyeto wala kujisaga.
Biblia pia inasema katika
Wakolosai 3:5 kwamba " Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;"
✓✓Kama unashiriki punyeto au usagaji ujue jambo ufanyalo ni dhambi.
Jambo hilo chanzo chake ni majini mahaba na imeshafikia hatua ya kukuathiri kisaiklojia ndio maana kuacha imekuwa ngumu.
Nini ufanye ili kuachana na punyeto au usagaji?
1. Tubu kwa ajili ya chanzo cha tatizo hilo.
Isaya 59:1-2 " Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."
Ndugu usikubali kufarakana na MUNGU kwa sababu ya uovu wako uitwao punyeto au kujichua.
Tubu na kuacha dhambi hiyo.
2. Futa muunganiko(connection) kati yako na ulimwengu wa roho wa giza na futa connection na majini mahaba.
1 Wakorintho 6:16 "Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja."
Majini mahaba ndio kiini cha ukahaba, hivyo kama kuna muunganiko kati yako na majini hata unatenda dhambi hiyo basi baada ya kutubu omba maombi ya kufuta muunganiko kati yako na majini, futa connection na akina Jezebel spirit wote.
3. Ziharibu nguvu za giza ulizowekewa na mawakala wa shetani zinazokutumikisha kufanya dhambi hiyo.
Nguvu hizo za giza ni mapepo na vitu vyenye mapepo unavyotumia kwenye dhambi hiyo, ni YESU KRISTO pekee anayeweza kuyaondoa mapepo ndani yako, mkimbilie YESU KRISTO kwa maombi utafunguliwa.
Neno lake linathibitisha hilo katika
Mathayo 8:16 kwamba " Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,"
4. Maeneo haya yanahusika na nguvu za giza kwako ili utende dhambi hiyo.
Dawa ni damu ya YESU KRISTO kukutakasa, omba Maombi ya kujitakasa kwa damu ya YESU KRISTO.
1 Yohana 1:7 "bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."
A. Mikono.
Takasa mikono yako kwa damu ya YESU KRISTO.
B. Sehemu za siri
Takasa sehemu zako za siri kwa damu ya YESU KRISTO.
C. Nafsi, akili na ufahamu.
Takasa maeneo hayo kwa damu ya YESU KRISTO.
5. Vunja agano la kipepo linalokutumikisha kipepo.
Hosea 10:4 ''Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.''
✓✓Maagano ya kishetani ni mabaya sana na ni muhimu kujitenga nayo kwa kumkimbilia Bwana YESU KRISTO na nguvu zake.
6. Tabia hiyo najua hukuanza mwenyewe bali inawezekana kuna mtu alikufundisha au alikusimulia, uliona kwenye TV n.k Sasa jitenge mbali na kila vitu au watu waliosababisha uingie katika uovu huo.
1 Wakorintho 15:33-34 " Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui MUNGU. ......."
7. Chukulia kitendo hicho kama sumu kali inayoua roho yako kiroho, naamini ukiambiwa kuacha kula chakula fulani chenye sumu hakika utaacha. Kama ni hivyo basi hata jambo hilo acha maana linaweza.
A. Kukukosesha mbingu.
B. Kufungulia milango zaidi ya dhambi kwako.
C. Kuvuruga ndoa yako maana shetani atakutengenezea mazingira ili ujifurahie mwenyewe kipepo na sio kufurahi na Mwenzi wako.
D. Kuharibu huduma yako hivyo unaweza kubaki Mtumishi vuguvugu tu kwa sababu ya dhambi hiyo Kama Wewe ni Mtumishi wa MUNGU.
Waefeso 4:17-23 " Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika BWANA, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa MUNGU, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao; ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani. Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza KRISTO; ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika YESU, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya MUNGU katika haki na utakatifu wa kweli."
8. Kama uko ndani ya ndoa na unafanya punyeto au usagaji muombee Mume/Mke wako na msaidie kiroho na kimwili ili akutosheleze maana ni huyo tu ndio MUNGU amekupa.
Yakobo 5:16 "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. ......."
9. Tembea kwenye Kanuni za Ki MUNGU ili shetani asipate nafasi ya kukutumia.
Kumbu 28:1 "Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;"
✓✓Ziko kanuni nyingi za ki MUNGU unazotakiwa kutembea nazo, baadhi ni maombi, kuukomboa wakati, ibada, kusoma neno na kulitafakari, kuandaa mafundisho na n.k
Ukitembea kwenye kanuni hizo kwa ukamilifu utashinda dhambi hizo.
10. Omba MUNGU akupe neema ya kuachana na tabia hiyo chafu sana.
Waefeso 1:7 "Katika yeye huyo(YESU), kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake."
Ndugu kuanzia Leo usikubali kamwe kuwa msagaji wala mtu wa punyeto.
Ishinde dhambi hiyo kwa kufuata neno la MUNGU na kulitii.
"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. -Ufunuo 2:11''
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292( whatsapp).
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments