SHUHUDA BAADA YA KUFUNDISHA KUHUSU MADHARA YA PUNYETO NA USAGAJI.

USHUHUDA BAADA YA KUFUNGULIWA KUTOKA KIFUNGO CHA PUNYETO.
Shalom mtumishi wa Mungu
Sikuweza kukupa ushuhuda kuhusu dhambi ya punyeto
Nakumbuka niliianza kama utani mwaka 2009 nikiwa nchini Sudan nikiwa sijui kama ndio punyeto na niliufurahia huo mchezo huku nikiamini kuwa sio dhambi kwa sababu hakuna mwanamke anayehusika na ukizingatia nilikuwa simjui mwanamke
Kipindi hicho nilikuwa karibu sana na Mungu naweza kusema kuliko wakati wowote ule na bado nilikuwa nikiendelea na huo mchezo bila wasiwasi wowote
Kuna wakati nilisikia watu wakiongelea kuwa ni mbaya hivyo nikaadhimia kuacha lakini haifiki hata wiki narudi tena kule kule
Nakumbuka niliwahi kuacha kwa mwezi mmoja lakini nikarudia tena.
Nilikuwa nina uwezo wa kufanya hata mara nne kwa siku.
Na kama unavyojua kuwa ni Jambo la aibu hivyo inakuwa vigumu sana kumshirikisha mtu
Mwaka 2015 nilifunga ndoa lakini bado mke wangu akiwa period niliendelea na huo mchezo
Mwezi wa saba nilisafiri kwenda Congo na bado niliendelea na huo mchezo
Nakumbuka Mtumishi Mabula niliwasiliana na wewe mwishoni mwa mwaka 2015 nikakushirikisha hii shida yangu na ukaniahidi kuomba na mimi na ndio ulikuwa mwanzo kupona huu ugonjwa
Kwa kweli sikuamini kama ningeweza kuja kuacha kabisa huu mchezo
Lakini leo imebaki historia
Mbaya zaidi kuna kipindi hata ufanisi wangu kwenye tendo la ndoa ulipungua sana kwa sababu tu mke wangu hakuwahi kumjua mwanaume yeyote zaidi yangu hivyo kwake haikuwa shida na nilimweleza ukweli wangu.
Kwa neema ya Mungu tu nilikuja kurudi kwenye hali yangu ya kawaida.

Mungu akubariki Sana


USHUHUDA BAADA YA KUZUNGUMZIA KUHUSU PUNYETO.
Bwana Yesu apewe sifa mtumishi Mabula.
Mungu akubariki sana kwa somo la punyeto Mimi nipo mkoa wa Pwani nimesumbuka sana na punyeto kuanzia 2011-2018 mwanzoni, nimeombewa sana ikawa ngumu kuacha, nimefunga mwenyewe na kuomba pia ikawa ngumu, kilichofanyika nikatoa sadaka ya kuondoa vifungo vyote vilivyonifunga na nikaamini Mungu atatenda japo niliendelea kupiga lakini nilikuja kushangaa wiki 1 imepita, mara mwezi, miezi nikajua Mungu ametenda, na sasa hivi nimeokolewa kwa damu ya Yesu, pia Mungu akubariki kwani naamini kwa mafundisho yako Mungu atawafungua vijana wengi ambao hawakupata mwongozo.



USHUHUDA KUTOKA AMERICA.
Jana usiku nilifundisha kidogo kuhusu ubaya wa punyeto.
Rafiki yangu mmoja raia wa Marekani mwenye Asili ya Burundi akaniandikia hivi.

" ubarikiwe sana mtumishi Mabula for a good messege.
Namshukuru sana Mungu wa Isreal atupaye kushinda katika Kristo Yesu.
Hujakosea mtumishi kufundisha madhara ya punyeto yaani upo sahihi kabisa, vijana wengi wapo busy na punyeto kuoa hawataki.
Utakuta kijana ana miaka thelathini hadi thelathini na tano, ana mchumba lakini hana wazo la kuoa sio kwamba hana pesa ya kutoa mahari; pesa anayo.
Punyeto ni mchezo hatari sana.
Wengi wanaopiga punyeto/kujichua hufundishwa na marafiki zao wa karibu.
Mimi pia nilifundishwa na mtoto wa shangazi yangu, nakumba aliniambia kuwa “bora kujichua kuliko kulala na mwanamke.” Before hajaniambia nilikuwa sijui kabisa kupiga punyeto na sikuwa najua kuwa punyeto ni dhambi.
Sasa nikaanza kucheza mchuzo huo bila mimi kujua kuwa nafanya mchezo hatari sana.
Nilipohamia huku Marekani, nikakutana na kaka mmoja mkarimu sana na ni mwimbaji wa kwaya. akaniambia kujichua ni kwa kila kijana aliye duniani, kwa kuwa alikuwa mkubwa kwangu nikamsikiliza na kuendelea kufanya ule uchafu.
Nilipogundua kuwa kupiga punyeto ni dhambi na ina madhara, aisee nilianza kuuchukia mchezo huo na nikawachukia walionifundisha kucheza mchezo huo hatari.
ilikuwa ngumu sana sana kuacha kupiga punyeto. Kuna wakati mwingine hadi kufunga nilikuwa nafunga ili niache kujichua, lakini sikufanikiwa hata kidogo. Kila nikijaribu kujinasua najikuta nikifanya mchezo uleule bila hata mimi kupenda.
Ilifikia hatua hadi nikasihi huenda sitaacha kupiga punyeto maana nishazoea na kila nikijaribu kujinasua najikuta nikiisha kushindwa.
Sasa ilibidi niombe msaada kwa watumishi wa Mungu na kwa marafiki zangu. Licha ya kwenda kwa watumishi lakini sikufanikiwa kabisa.
Baada ya kuona kwamba kila njia ninayotumia haifanikiwi, ilibdi nichukue maamzi magumu ya kuacha dhambi hiyo.
Hiyo dhambi haihitaji maombi bali maamuzi magumu na kujiepusha na maeneo yanayomsababisha mtu apige punyeto.

Lakini pia nikuulize swali Mchungaji Mabula.
Sasa Mchungaji, kwanini wachungaji wengi hawafundishi kanisani kuwa punyeto ni dhambi?
Mimi najua vijana wanaopiga punyeto, wengi wao hawajua kuwa ni dhambi kwani hawafundishiwi.
Kwa huku American hawafundishagi jambo hilo, me sijawahi kuona wala kusikia mchungaji akifundisha jambo hilo kanisani au akiwaonya vijana wanaojichua waache kujichua. Kwenye media nishasikia lakini sio kwa wachungaji wa huku. Me nakwambia wazi bila kificho, hizi media zimenisaidia kwa sehemu kubwa kujua mambo mengi ya Mungu. Sio kwamba kanisani sifundishwi hapana, nafundishwa na ninapewa mafundisho sahihi, lakin mambo mengi nimeyajua kwenye media na kusoma vitabu vya kiroho na masomo pia.
Ubarikiwe

Comments