SHUHUDA BAADA YA MAOMBI.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Huwa napenda pia kukushirikisha baadhi ya shuhuda zinazotokea kutoka kwa watu wa MUNGU ninaowaombea ambao baadae hutuma shuhuda baada ya MUNGU kutenda muujiza kwao.
Sifa heshima, adhama na utukufu wote ni kwa YAHWEH MUNGU wetu milele.

Shuhuda mbili ni hizi.
1. BWANA YESU asifiwe Sana Mtumishi, nina mshukuru Mungu Sana kwaajili ya maombi ya Jana, Leo asubuhi nikiwa ofisini nilikuwa nimeacha Mlango wa ofisi yangu wazi, Mungu akamtumia mwenzangu kuja kuufunga ule Mlango, na moyoni mwake alikuwa anashuhudiwa asiniache peke yangu, baada ya muda tukasikia makelele kwenye Mlango wa ofisi yangu Kumbe nyoka alikuwa anataka kuingia kwangu bahati nzuri akauawa. Ninamshukuru Mungu Sana kwaajili ya hilo. Ubarikiwe Sana Mtumishi kwa mafunuo yako na maombi.
2. Nashukuru Mwalimu Mabula Kwa Maombi Yako Tangu Uniombee Sijawahi Tena Kuota Nafanya Mapenzi Hata Zile Dalili Hazionekani Namshukur Sana Yesu Kristo Kwa Matendo Yake. Makubwa Sasa Nahitaji Kutembea Katika Kristo Yesu Ili Niwe Mshindi. Mimi Sadiki Kutokea Mkoa Wa Geita
Asante Yesu Hakika Wewe Siyo Mwanadamu Njia Zako Hazichunguziki Sitaishia Kukushukuru Bali Nitakutumikia Pia .

3. Bwana yesu asifiwe! Nakushukuru Mtumishi, uliponifanyia maombi kwa ajili ya tatizo langu la jicho kuuma, kiukweli namshukuru sana MUNGU Wa yasiyowezekana kwa binadamu!!! Hakika nimeona utofaut kabisa na hapo awali jicho linaendelea kurecover!!! Naomba uendeleee kunikumbuka kwenye maombi yako binafsi!!! Nami kwa nafasi yangu naendelea kujiombea!!! Namshukuru MUNGU Wa mbinguni.


USHUHUDA
Shalom Mtumishi wa Mungu na rafiki yangu Peter Mabula.
Hakika maombi uliyoniombea jana ni ufunuo kutoka kwa Mungu maana mimi tangia wiki iliyopita hadi jana nimepitia vita vikali katika ulimwengu wa Roho kiasi ya kwamba nimepigana vya kutosha lakini kila nikiomba maombi ya vita hali inazidi kuwa mbaya kwangu , na cha kushangaza ni kwamba maadui zangu ninaonyeshwa na Mungu lakini kila nikiwapiga kesho wanarudi kwa njia nyingine. basi ikafika mahali nikasema ngoja sasa nimwachie Mungu apigane mwenyewe vita vyangu maana kasema katika 2 Nyakati 20:15 vita ni yake.

Nilipofanya hayo maombi ya kumkabidhi Mungu maadui zangu apigane nao. Nikaota ndoto nimempiga mjusi, hawa wenye mistari nyeusi migongoni na fimbo nikamgawanyisha katikati na nikawa ninasema leo nimekumaliza hurudi tena, lakini cha kushangaza ni kwamba kipande kimoja cha yule mjusi ni kama kikanirukia kichwani mwangu nikajikuta ninachukua kioo ili kujiangalia kama kimetua kichwani ,nilipoona hamna basi nikasema leo nimemmaliza huyu kabisa.
Nikawa ninaendelea kumuomba Mungu aingilia kati maisha yangu anisaidie dhidi ya hizi vita vya kiroho. Na jana niliota ndoto yenye watu wengi akiwemo huyu mke wa mwajiri wangu, na Nabii mmoja wa hapa Tanzania na watu wa ukoo wetu. Nikatambua kabisa kuwa hawa sio watu wazuri ni ishara ya vita vya kiroho maana nikawaangalia wote kwa jinsi ya kimwili sio watu wazuri kabisa wana mambo ya kishirikina wote. Kasoro huyo nabii maana sijawi kumuona akifanya hivyo lakini kwa mambo niliyoona akifanya katika ulimwengu wa roho ni dhahiri kabisa ni nabii wa uongo.
Sasa nikaingia kuomba nikajikuta ninaomba kwa kunena kwa lugha tu. Nimeomba kama dakika 45 kwa kunena kwa lugha na nikawa ninakumbuka kuwa niliona mtu amefungwa mguu na kamba na nikawa ninaongea maneno yaliyoandikwa kwenye Mika 5..12
Nilipomaliza kuomba nikasema ngoja nikanywe chai ili nije nisome, nikaenda kunywa chai niliporudi badala ya kusoma hiyo mika nikasoma Yohana 17 yote. Nilipomaliza nikawa ninaomba kuhusu yale nilisoma hapo lakini nikitaka kuomba kwa kiswahili Roho Mtakatifu anakamata ulimi na ninaanza kunena kwa lugha na nikianza tu kunena ninakumbuka yale maneno yaliyoandikwa kwenye Mika 5;12 ,Nikafungua Biblia nikasoma nilipomaliza nikaanza kuomba na nikaona kitu cha ajabu maana niliomba kwa kawaida tu sijanena kwa lugha,
Hapohapo nikasema kuwa kuna soma la Mtumishi Peter Mabula nilionaga imeandikwa Kufuta uchawi wa nyongeza. Nikasema ngoja leo nitaingia kwenye blog yake nifanye yale maombi. Na nikamwambia Mungu asiniache niangamia anisaidie juu ya haya yote

Sasa nikiwa katika mawazo hayo ndipo ukanipigia simu na kuniambia "ngoja nikuombee" nikasema sawa na maombi uliyoniombea ni ya kuharibu uchawi, kuwapiga washirikina, mizimu na maadui wangu wote katika ulimwengu wa roho, nilishangaa sana, yaani wakati unaniombea nikajikuta ghafula ninacheka moyoni mwangu tu. Hakika Mungu amesikia sauti yangu, amejibu maombi yangu.
Mtumishi Mungu azidi kukubariki sana sana, sina cha kukulipa nasema tu Mungu azidi kukufungua macho ya rohoni
Ubarikiwe sana, nina imani hawa watesi wangu nimekwisha washinda Amen
Ninaomba pia uzidi kuniombea Mungu anifungue macho ya rohoni na masikio ya rohoni na niweze kumsikia Mungu na kufahamu kile anachosema nami. Maana Mungu amekuwa akisema nami juu ya huyo Nabii ila nimeshindwa nifanyaje.




USHUHUDA BAADA YA MAOMBI.
Bwana Yesu asifiwe Mtumishi Mabula.
Namshukuru Mungu naendelea vizuri ila kichwa walikisumbua sana wachawi yaani Mara usikie unapigwa na nyundo,Mara wanakata kichwa kama wanatumia wembe ,mara nywele zote usikie zinahama,yote hayo kichwa kikianza kuuma unafikiri kinataka kutoka
Leo kilianza kama wanakata na wembe baada ya MAOMBI YAKO sijui hali hiyo imeishia wapi
Mtumishi. Yaani unaupako wa hali ya juu sala zako nimwisho kwa wachawi, zimenisaidia saizi wanalalamika eti kwamba ninawaumiza na watakufa, nikiwauliza mmekuwaje hawanijibu kila mtu Analia kivyake .
Mwanzoni niliogopa lakini sasa hivi wakisema mi nazidi kuomba na kufunga na kukesha nimekutana na mambo mengi kupitia sala zako na kitabu chako, shetani anajeshi kubwa hata sana na alidhamiria mabaya sana, yaani hata mtu usiyemtegemea
Mimi ndugu zangu nimeshindwa niwafanyeje wanateseka sasa na wamehusika kunitesa Mimi ila sasa mapigo ni kwao baada ya maombi yako.
Nilikonda sana Mtumishi kila Mtu akawa ananinyooshea mkono Leo wananiomba Dawa eti umeponea wapi.
Yaani maombi yako ya siku chache hizi yamebadilisha pakubwa sana.
Nilikuwa naanza kuuza vitu vya ndani Leo akili imetulia najiuliza sipati majibu
Kweli Mungu ameniokoa amenikomboa Mungu

Endelea kuniombea Mtumishi nani siku moja nisimame na kuomba mwenyewe na roho wa Mungu anionekanie
Ni muda mfupi Peter Mabula umenitoa mbali sana nilikokuwa nimefungwa na wachawi, yaani namshukuru sana Bwana Yesu, nami Leo naamka Niko salama nafanya kazi wala siumwiumwi, Mungu akutie nguvu uendelee kutuombee na kutufundisha neno LA Mungu.
Mungu akubariki sana sana
Endelea kuniombea juu ya pesa ili mwezi ujao niweze kumshukuru Mungu kwa sadaka,zaka,na matoleo mengine mengi.
Hata mshahara ulikuwa mikononi kwa mtu sijui nikwambie nini nimeteseka mengine nashindwa kuelezea sasa, ni ndoto sijui nitakupa nini na nifanye nini kwa Mungu.
Mungu ni mwema hakika mtumishi.
Mungu akubariki na nakutakia siku njema
.

Comments