SHUHUDA KUTOKANA NA MASOMO YANGU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Namshukuru MUNGU katika KRISTO kwa jinsi anavyojibu maombi.
Nikipata shuhuda huwa napost ili angalau Mimi na wewe tupate kumtukuza MUNGU pamoja.
Biblia iko wazi sana kwamba inatupasa kushuhudia Matendo ambayo MUNGU wetu ametutendea.
1 Nyakati 16:8-11 " Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote."

Ninazo shuhuda ili tujifunze juu ya Matendo ya MUNGU na ili tupate kumtafuta na kumtukuza.
SHUHUDA.
1. Mtumishi Mabula, nashukuru sana kwa maombi yako, niliwahi kukushirikisha ili unisaidie kuomba, juu ya kaka yangu ambaye alianguka chini ghafla na hali yake ikawa kama kichaa. Sasa amepona. NAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA PIA NAKUSHUKURU KWA KUMWOMBEA. MUNGU YEHOVA WA MBINGUNI AENDELEE KUKUTIA NGUVU.
2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu, hakika nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyonifanyia, nilikupigia simu siku ya tarehe 5 nikakuomba unifanyie maombi kwa ajili kujifungua, ulinifanyia maombi na hatimaye Mungu ametenda muujiza nimejifungua salama siku ya jumapili tarehe 8, nimejifungua salama bila hata operation napenda kumshukuru Mungu sana kwa Neema yake aliyonijaalia na nakushukuru na wewe. Yaani uchungu haukuwepo ila baada ya maombi uliyoniombea Mungu alitenda muujiza.
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu, habari za siku, samahani sana kwa kutokuwasiliana na wewe kwa muda kidogo, ila napenda kukutaarifu kwamba Mungu amenitendea muujiza hivi sasa nina ujauzito. nikipata muda wa maongezi ntakupigia tuongee kiundani zaidi. Yaani miaka mingi bila mimba lakini baada ya maombi yako Mungu amenitendea muujiza, Ila dhidi kunikumbuka katika suala la ajira.
Ubarikiwe Sana na namshukuru sana Mungu kwa muujiza huu.


USHUHUDA MFUPI WA MTU ANAYESUMBULIWA NA WACHAWI.
Habari za asubuhi Mtumishi Mabula. Mtumishi wa Mungu
Sina budi kumshukuru Mungu kwa yote yanayoendelea kuonekana kwangu dhidi MAOMBI yako na mafundisHo yako.
Usiku wa Leo nimeanza kusoma kitabu chako kwa moyo na kwa nguvu zote ktk sura ya 4 sala ya kuharibu mitego ya wawindaji ikiwa saa sita usiku nikasikia nyayo za MTU akitembea sebureni kitu kikanijia rohoni nenda ukaone roho nyingine ikasema sali kwa nguvu muda huo huo MTU akatua pembeni yangu pembeni ya meza mwili ukatokewa na uwoga roho wa Mungu akaniambia sali kwa nguvu nikatamka maneno haya Adui zangu ni adui za Mungu, moto wa Yesu uwateketeze mpaka muwe majivu maneno hayo mtu Huyo sikujua ametowekaje. ikiwa SAA saba sasa na DK 13 kishindo kikubwa kilisikika huko nje nikampigia jirani Simu nikamuuliza kuna mini ananiambia Niko nje hii ni Mara ya pili sioni kitu.
Baada ya MAOMBI nikalala nikiwa nimelala nikasikia sauti ikiita jina Langu
Ila sikuitika.
MAOMBI yako juu yangu endelea kuniombea.



USHUHUDA.
Mungu azidi kukubariki Mtumishi Peter Mabula Kwani Mungu anazidi kutenda Kupitia Maombi yako kwani nimetambua kuwa Mungu ameweka Kusudi Kubwa ndani yangu ambalo shetani alijaribu kulizuia kwa Kupandikiza magonjwa na nguvu za giza kwenye maisha yangu nimeamini hilo kwani baada ya maombi yako wakati nikiwa nasoma Bibilia naona utofauti Mkubwa Sana kwa Jinsi navyopokea na Ninajiona kuwa Mungu ananianda kuwa Mtumish Mkubwa Sana na ndio maana shetani alifanya njama za kutaka kunizuia. Nakuomba uzidi Kuniweka Kwenye Maombi wala usiache kwani Najua unaniombea Mara nyingi dhidi ya uonevu wa shetani. siku hizi naona nguvu kubwa sana hata ya Mimi kujiombea na pamoja na Maombi yako naamini Kitu kikubwa sana katika Ulimwengu wa Kiroho Kinafanyika hivyo tuwezidi kuwapamoja katika Maombi kwani Mimi na Wewe ni wabeba kazi kubwa kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo
Na ninakuomba Mtumishi wa Bwana unisaidie nijue ni kitabu gani hasa cha kwenye Bible kinachonifaa Zaidi kukisoma kulingana na Wakati nilionao?

Majibu yangu kwa rafiki huyu yalikuwa ni haya;
MUNGU akubariki Sana.
Vitabu vyote vya Biblia ni Vitabu sahihi vya kusoma. Soma Biblia nzima lakini isome kwa jinsi ya KRISTO.
MUNGU akubariki



USHUHUDA.
Shalom!
Asante sana mtenda kazi katika shamba la Bwana hakika namuona Mungu tangu ile siku umeniombea niwe na nguvu za Roho mtakatfu
Najikuta nina mamlaka tofauti na zamani siku ile umeniombea usiku nikaota namfukuza mchawi wa kiume ila sura sikuiona kwa jina la Yesu na akakimbia. nyumbani kulikuwa na mapaka yanalia kama watoto usiku kucha lakini ni tangu siku ile nimekuwa na nguvu za Roho mtakatfu nilikemea na hawaji tena. namuona Mungu mtumishi maelewano na mume wangu yalikuwa hafifu sana lakin tangu uniombee tunaaman na kufurahi namshukuru Mungu sana kwa ajili yako hakika ipo siku nitayasimulia matendo makuu ya Mungu ubarkiwe
Nguvu za maombi ya usiku zimerudi upya asante sana



Bwana YESU Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.
Baada ya kufundisha somo la kuharibu madawa ya kiganga na kichawi nilipata shuhuda kadhaa.
Mtu mmoja aliniambia kwamba alipoomba maombi Yale alitetemeka na kuona vitu vikitoka mwilini mwake.
Mtu mwingine akasema kwamba baada ya kujifunza somo hilo na kuomba alipata amani ya ajabu na usiku alilala kwa amani baada ya muda mrefu kupita.
Mtu mwingine amenijulisha Leo juu ya ndoto yake, hiyo nimesukumwa kukuletea kama ilivyo na uone majibu yangu ili kama na wewe uko mbali na MUNGU kwenye fahamu zako basi uanze na YESU KRISTO ili shetani asikuhusu tena.
Mtu huyo aliniandikia hivi:

"Bwana asifiwe mtumishi! Jana nlikuwa nafanya maombi yale uliyotuma kwenye group kuhusu waganga na uchawi. basi usiku nimelala nikaota nipo kwenye foleni ya watu wengi sana wanaoenda kwa mganga maarufu kaja, nami nikaaamua kumfuata ili akanitatulie shida zangu, na kiuhalisia nina shida mpaka nakata tamaa lakin nilipokaribia kufikiwa zamu yangu moyo ukaanza kuniuma sana, nikasema ngoja nikatafute Mchungaji nitubu kwa hicho kitendo, basi nikaondoka kwenda kutafuta Mchungaji ili nitubu.
Ila sijaelewa nini maana yake ndoto hiyo.

MAJIBU YA MTUMISHI PETER MABULA YALIKUWA HAYA.
Maana yake hiyo ndoto ni hii.
1. Usije kamwe ukaenda kwa mganga yeyote maana utapata madhara makubwa.
2. Ulikuwa na nia rohoni mwako ya kwenda kwa mganga ila MUNGU amekuonya maana ni hatari kwako kuliko unavyodhani.
3. Umejulishwa juu ya wakala wa shetani mmoja atatokea kwa gia hiyo ya uganga na atawanasa watu wengi wasio na akili za rohoni.
4. MUNGU amekufunulia msaada wako utatoka kwake kupitia watumishi wake(Unaweza ukaanza na Mimi leo , nipigie saa moja na nusu usiku Leo nitakuombea na MUNGU atakuonekania.) Hivyo anza kuutafuta msaada wa MUNGU na huo uko makanisa waliko watumishi, hivyo okoka kama hujaokoka, husika na watumishi wa kweli wa MUNGU kimaombi na utashinda kiajabu.
5. Mali au pesa uliyotakiwa kuipeleka kwa waganga ipeleke kwenye kazi ya MUNGU.
Ubarikiwe


USHUHUDA Mzuri.
Mtumishi tokea uliponiombea juzi kupiga upofu wachawi yaani nalala usiku vizuri, hakika wamepigwa upofu maana walikuwa wananisumbua sana na kunifuatilia hadi nikawa naamka saa saba usiku nawasha taa. Ila shetani ameaibika na jeshi lake. Namshukuru Mungu sana kwa kunishindia pia namshukuru Mungu sana kwa kukupa kibali na wewe mtumishi wake kutumika shambani mwake. sifa na utukufu mamrudishia Mungu kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.


USHUHUDA Mzuri.
Bwana Yesu apewe sifa saaana 👋🏽👋🏽 mtumishi wa Mungu Peter Mabula
Mafundisho yako hua yananibariki sana, na wewe ni mmoja kati ya watu walionikuza kiroho, kabla sijaokoka nilikutafuta wewe kwanza na ukanipa njia za kufanya ili nimuone Yesu wa msalaba hakika nimemuona na namuona na mafundisho yako yamenibariki sana, pamoja na walimu wengne kwenye group la NENO LA MUNGU ORIGINAL, kwa kweli MUNGU akuinue sana katika viwango vya juu zaidi
Kwa sasa natumia namba hii mpka nitakaporudi Tanzania,
Nipo Uganda kwa sasa



USHUHUDA
Bwana Yesu asifiwe mtumishi hata mimi pia namshukuru Mungu maana ulipofundisha lile somo la Malaika pamoja na kazi zao, na mimi pia nilichukua jukumu la kuomba Yale maombi ya kazi za Malaika. Niliomba kuhusiana na suala Zima la kazi nilipomaliza kuomba ilikuwa asubuhi niliona moyo wangu mwepesi nina furaha na amani isiyo ya kawaida na isiyoelezeka. Basi jioni nikapigiwa simu sehemu moja wapo Kati ya zile nlizokuwa nimetuma maombi, nikaambiwa lini utakuwa na muda uje ofisini kwetu? Nikawaambia Ijumaa wakaniambia sawa njoo. Nilipokwenda waliniuliza maswali machache wakaanza kunielekeza taratibu za kazi, wakaniambia kazi nmepata wananipa wiki moja kwa ajili ya maandalizi.


USHUHUDA.
Bwana Yesu asifiwe Mtumishi Peter Mabula nashukuru Mungu kwa maombi yako kuhusu kuota ndoto nafanya mapenzi na watu nisiowajua, nashukuru toka umeniombea zile ndoto azijanirudia tena wala kuota kuwa nafukuzana na wachawi tangu tumefanya maombi Mungu kanijibu kwakweli nashukuru kwa maombi yako bado tu suala Ka kupata kazi ndo nashuhulikia katika hilo nawatafuta watu wenye ofisi ili waweze kunisaidia kupata kazi kama nilivyokuambia kuwa sina MTU wa kunisomesha ndo nikipata hiyo kazi niweze kujiendeleza kimaisha na kimasomo.
Natumaini hata hili nalo litapita tu na huu mwezi wa saba hautaisha bila ya kujibiwa ombi langu la kupata ofisi Mungu atakayopenda
Ila Mtumishi Mimi nilikuwa naombi, nausikia kweli moyo wangu ukihitaji kutoa fungu la kumi lakini sina ufahamu nalo sana na nimeshangaa umetuma hilo neno kwenye group nikahisi Kama ulikuwa moyoni mwangu sasa naomba kujua tofauti ya zaka na fungu LA kumi.



USHUHUDA.
Shalom Mtumishi, juzi baada ya kufundisha somo kuhusu malaika niliingia kwenye maombi na baada ya maombi nililala nikaota ninapanda mlima halafu nikashindwa kupanda ile nilishakata tamaa ya kupanda wakaja watu wawili mmoja nyuma yangu na mwingine mbele, wa mbele akanishika mikono na wanyuma akanishika miguu na nikapandishwa ule mlima .
Jana pia nilisoma somo uliyofundisha jinsi ya kupigana vita ya kiroho, na nikaona yale maombi uliyoandika katikati ya somo kuhusu maadui kuwekea alama na kisha Malaika akiwaona wawapige. Baada ya kuomba niliota ndoto niko sehemu ninapita kwenye ukuta mrefu sana na nikajikuta kuna kitu kimenipaisha juu sana nikawa ninatembea juu juu tu hadi nikamaliza ule ukuta nikatua sehemu safi.

Comments