![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Mtumishi wa MUNGU ni Mteule yule aliyeokoka na anaipeleka mbele Injili ya Bwana YESU KRISTO.
Marko 16:15 "Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe."
◼️Mtumishi wa MUNGU ni mtu yule aliyeamua kumfuata YESU KRISTO kama Bwana na Mwokozi wake.
Marko 1:17" YESU akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu."
◼️Mtumishi wa MUNGU ni mtu yule anayeamua kuyatoa maisha yake ili kumtumikia YESU KRISTO.
Mathayo 19:29 "Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele."
➡️Mtumishi wa MUNGU sio mpaka yule tu aliyewekewa mikono bali mtumishi wa MUNGU ni yule aliyeamua kumfuata YESU KRISTO siku zote.
◼️Mtumishi wa MUNGU ni yule aliye mwanafunzi wa Neno la MUNGU.
◼️◼️Mwanafunzi wa YESU ni yule anayejifunza Neno la MUNGU, ni yule anayekubali kushughulishwa na maelekezo ya Mwalimu wake yaani YESU KRISTO kwa njia ya ROHO MTAKATIFU.
◼️◼️Ni vyema sana kufanyika Mtumishi wa MUNGU uliye mwaminifu.
2 Timotheo 2:15 ''Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. ''
Katika Utumishi kuna;
1. Watu kufunguliwa vifungo vya giza na kuponywa magonjwa ya kiroho na kimwili.
Luka 10:9 "waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa MUNGU umewakaribia."
2. Watu kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao.
Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;"
3. Watu kutubu na kuacha dhambi.
Luka 5:32 "Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu."
4. Watu kuwa na msingi mzuri wa imani katika KRISTO.
Waebrania 12:2 "tukimtazama YESU, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha MUNGU."
5. Watu kusamehewa dhambi na kusameheana.
Luka 1:77 "Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao."
6. Watu kuwa na moyo wa kulijenga Kanisa la MUNGU.
Mathayo 16:18 "Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."
◼️Moyo wa kulijenga Kanisa uko ndani ya walio na YESU KRISTO.
7. Watu kumwabudu MUNGU Baba katika roho na kweli.
Yohana 4:23 "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu."
◼️Mtumishi wa MUNGU hakikisha una ujumbe wa msingi wa Neno la MUNGU ili kuwafundisha wale ambao MUNGU amewakusudia.
➡️Ujumbe wa msingi unaotakiwa kuwa nao ni ule uliopewa na ROHO MTAKATIFU.
➡️Ni Ujumbe usiopendelea watu.
➡️Ni ujumbe unaotimiza kusudi la MUNGU.
◼️Hakikisha una ujumbe wa kumbadilisha Mtu kutoka gizani an aende nuruni.
◼️Hakikisha una Ujumbe wa kumbadilisha mtu kutoka dhambini na sasa aende uzimani.
◼️◼️Hakikisha una ujumbe unaombadilisha Mtu kutoka kwa shetani na sasa awe kwa YESU KRISTO, huo ndio Ujumbe wa msingi.
◼️Kama ujumbe huo unawafundisha watu waliookoka na wanaishi maisha matakatifu basi ujumbe wako utawapa maarifa na utawapa tahadhari ili wasirudi nyuma.
◼️◼️Simamia Neno na MUNGU na tembea kwenye Neno la KRISTO.
◼️◼️Litumie Neno la MUNGU kwa haki.
Sema yakupasayo kusema, na yale yasiyokupasa kusema basi usiyaseme.
2 Timotheo 2:15-16 " Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,"
◼️Ili umtumikie MUNGU vyema zingatia haya;
1. Omba MUNGU akupe kibali kwa watu unaotakiwa kuwapelekea Neno la MUNGU.
Isaya 50:4" Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao."
2. Hakikisha ROHO MTAKATIFU anakupa ujumbe wa Neno la MUNGU.
Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."
3. Ishi maisha matakatifu kama YESU aliyekuita anavyotaka.
1 Petro 1:15" bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
4. Omba MUNGU akupe roho ya hekima na ufunuo katika kumfahamu yeye na Neno lake ili utembee kwenye kusudi lake.
Waefeso 1:17 '' MUNGU wa Bwana wetu YESU KRISTO, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;"
5". Kwa msaada wa ROHO MTAKATIFU uwe mtu wa kuchunguza maandiko, ujue vyema na utazame kama MUNGU atazamavyo.
Matendo 17:11 "Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo."
◼️Ni vizuri kuchunguza maandiko na omba ROHO MTAKATIFU akupe kuelewa maandiko.
Luka 24:45 "Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko."
➡️Uwe kama Danieli aliyechunguza maandiko akapata Ufahamu wa ni Nini na wakati gani Kutatokea Nini.
Danieli 9:2" katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini."
◼️◼️Ndugu hakikisha umeokolewa na YESU KRISTO na kisha anza kumtumikia MUNGU.
1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."
Nitafafanua somo hili siku moja.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments