![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◾Leo tunaangalia kazi 3 za Maombi.
Najua Kuna kazi zaidi za 7 za Maombi, na Mimi Peter Mabula Nimewahi kufundisha kazi nyingi za Maombi lakini Leo ni Ufunuo mpya juu ya kazi za Maombi.
◼️Maombi kwa ufupi yanamuunganisha mwanadamu na Muumba wake.
◼️Maombi ni njia mojawapo ya kumwabudu MUNGU.
◼️Maombi ni njia ya kupokea baraka kwa MUNGU.
◼️Ukijua kazi za Maombi hutaacha kuomba.
➡️Wengi sababu yao ya kufanya maombi ni ili tu wapokee baraka, wakipokea hawaombi tena kwa sababu hawajui kazi zingine za maombi.
Ndugu yajue hayo Leo ili hiyo ikupe nguvu za kuomba kila siku na ili hiyo ikupe kuomba zaidi sana baada ya kupokea hitai lako.
◼️ Na katika Maombi Yako usisahau kuwaombea na wengi.
➡️Ulishawahi kuomba nusu saa nzima, ukipeleka tu mahitaji ya wengine kwa MUNGU ili MUNGU awatendee mema?
Kama hujawahi kufanya hivyo basi siku nyingine uwe unafanya hivyo.
Unaweza ukaomba masaa mengi ukiombea mahitaji yako binafsi, ni sawa lakini wakati mwingine tenga muda wa kuwaombea wengine kwa uzito ule ule kama unajiombea wewe mwenyewe.
◾Kazi 3 za Maombi.
1. Maombi ni njia kuu ya kupokea majibu yako.
Luka 11:10 "Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
◼️Maombi ni njia kuu ya kupata suluhisho la chochote kwenye maisha yako ndio maana Biblia inasema Kila aombaye hupokea.
◼️Maombi ni njia kuu ya kuwashinda maadui zako na watesi wako, unaweza kuomba ukapewa kuwashinda adui zako.
➡️Maadui zako wanaweza kupanga kukushusha cheo ili wao wapande cheo.
➡️Lakini kwa muombaji makini hakika mashauri ya watu wabaya yanaweza kutanguka na wewe ukawa juu huku maadui zako wakishushwa chini.
Ayubu 5:12 " Yeye(MUNGU) huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao."
Unahitaji tu kuomba na kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.
◼️Maombi ni muhimu sana katika maisha ya mteule wa KRISTO.
◼️Unapofanya maamuzi baada ya maombi hakika utaamua vyema.
Maombi hukufanya uamue vyema.
◼️Unapofanya jambo jema baada ya maombi utafanikiwa sana.
◼️Maombi ni ufunguo wa kufungua ushindi wako.
◼️Maombi kwa kutumia Neno la MUNGU husambaratisha nguvu zote za giza.
◼️Maombi yanaondoa vikwazo na vizuizi vyote.
Maombi pekee ninayoyazungumzia ni maombi katika jina la YESU KRISTO.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
2. Maombi huifanya ahadi ya MUNGU kwako Uijue, Uipokee na Uifanyie kazi.
Mfano hai ni huu.
Matendo 13:2 "Basi hawa walipokuwa wakimfanyia BWANA ibada na kufunga, ROHO MTAKATIFU akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia."
➡️Hawa Maombi yao yalisanabisha wajue kusudi la MUNGU, mapokee majukumu ya ki MUNGU na wafanyie kazi kusudi la MUNGU.
◼️Hakikisha unakuwa mtu wa maombi.
➡️Mapenzi ya MUNGU Huwezi kuyajua kwa usahihi kama wewe sio muombaji.
◼️Mapenzi ya MUNGU ni watu waijue kweli.
◼️Mapenzi ya MUNGU ni watu Waokolewe na kwenda uzima wa milele.
Maombi ni muhimu sana kwa mteule wa KRISTO.
Mathayo 21:22 "Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea."
◼️Hatuwezi kupokea majibu yetu hadi tuombe.
Huwezi kupokea bila kuomba.
Huwezi kujibiwa bila kuomba.
Ndugu inakupasa sana kuwa muombaji.
◼️Maombi yenye nguvu ni maombi ya kuomba kwa Neno la MUNGU.
➡️Kuomba kwa Neno la MUNGU sio kukariri tu maandiko Bali ni kuomba sawasawa na Neno la MUNGU na huku ukilitumia Neno la MUNGU.
◼️Kumbuka Neno la MUNGU ndio linaloweza kukupa uhakika wa ulichoomba.
◼️Neno la MUNGU ndilo hukuongezea imani ya kupokea ulichoomba.
◼️Neno la MUNGU ndio huonyesha miiko na mipaka ya muombaji.
◼️Neno la MUNGU humpa nguvu muombaji.
◼️Kama huna Neno l MUNGU ni vigumu sana kuwa na nguvu za maombi.
Waebrania 4:12" Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."
◼️Ndugu hakikisha unaomba sawasawa na Neno la MUNGU na omba kwa Neno la MUNGU.
➡️Mawakala wa shetani wanaweza wakakuletea ugonjwa ili tu kubadili ratiba yako ya mafanikio uliyopangiwa na MUNGU.
MUNGU amekupa mamalaka hivyo uwe muombaji ukifuta kila mipango ya shetani dhidi yako.
◼️Maisha yako hayawezi kuinuka kama hujui kuomba. Ndugu maombi ni muhimu sana sana.
◼️Unaweza kusalitiwa na wanadamu lakini muujiza wa MUNGU kwako uko pale pale.
Simama imara ndugu kwa maombi na songa mbele na KRISTO
3. Maombi yanatiisha mwili.
1 Wathesalonike 4:4 "kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;"
◼️Kuutiisha mwili ni kuufanya usikutawale.
Wagalatia 5:13 "Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo."
◼️Katika Maombi utakuwa busy na mambo ya MUNGU kiasi hutakuwa na Nafasi ya kuwaza mabaya, kutenda mabaya Wala kiu ya mabaya haitakuwa ndani Yako, huko ndiko kuutiisha mwili.
Warumi 8:8" Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza MUNGU."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments