![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Leo tunaangalia Kazi za manabii wa uongo, Lengo tujitenge mbali na manabii wa uongo maana wao wako kinyume na YESU KRISTO Mwokozi wetu mwenye uzima wetu wa milele.
Biblia ipo wazi ikisema Watatokea manabii wa uongo.
Mathayo 24:11 "Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi."
◼️Kazi za manabii wa uongo ni kudanganya watu na kuwapoteza wasimfuate KRISTO.
Mathayo 24:24 "Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
➡️Narudia tena kazi ya manabii wa uongo ni kudanganya, hivyo ukikaa kwao utadanganywa na ukifanyia kazi huo uongo utakosa mbingu.
◼️Manabii wa uongo wanaweza hata kuapa kwamba MUNGU amewaambia kumbe wala hawahusiki na MUNGU.
Yeremia 5:2 "Na wajaposema, Kama BWANA aishivyo, hakika waapa kwa uongo."
➡️Manabii wa uongo sio lazima waitwe jina "nabii", Bali wengine wanajiita nabii na wengine wanaitwa kwa vyeo vingine vya kiroho kama Mchungaji, Mtume n.k
➡️Manabii wa uongo watafanya uongo wote lakini lengo kuu watu wasifike uzima wa milele.
➡️Lengo la manabii wa uongo ni kuwakosanisha watu na YESU Mwokozi ili wasipate uzima wa milele.
◼️Manabii wa uongo wakati mwingine husema maneno laini na ya heshima ili usishituke.
Ezekieli 13:6 "Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, BWANA asema; lakini BWANA hakuwatuma; nao wamewatumainisha watu ya kuwa neno lile litatimizwa."
➡️Lengo lao ni usiishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
➡️Manabii wa uongo wametumwa na shetani ili kuupoteza ulimwengu kwamba watu wa ulimwengu wasiokolewe na YESU KRISTO hata wakapata uzima wa milele.
Mathayo 7:15-16 " Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. ....."
◼️Kazi nyingine ya Manabii wa uongo ni kuipindua Biblia mioyoni mwa watu.
➡️Manabii wote wa kwenye Biblia walikuwa wanatoa unabii wa watu kutubu na kumrudia MUNGU.
➡️Manabii wa Leo wengi zaidi na inawezekana sio wote unabii wao wanaoutoa ni kuhusu tu mafanikio ya kimwili.
➡️Kama ni hivyo hakika kuna pahali hakuko sawa katika Kanisa la MUNGU.
Wagalatia siku moja waliambiwa ni nani aliyewaroga?
Inavyoelekea sana itafikia hatua ya Kanisa la Leo kuambiwa ni nani aliyewaroga?
➡️Leo kuna manabii mfano mtandaoni huku jumbe zao ni za kusema tu " Watu 100 wa kwanza Ku like post hii watapata pesa nyingi mwezi huu" Mara "Andika Amen ili upate upako" andika "Napokea ndio utapata kibali na Mali"
✔️✔️Hii ndio tofauti kubwa sana kati ya Manabii wa Biblia na manabii wa sasa.
Hebu ona nabii Isaya kama sehemu ya manabii wa Biblia anasema
Isaya 1:16-17 " Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane."
➡️Nabii wa Leo hata unaweza kumfuatilia mwaka mzima na usimuone popote anaongoza watu sala ya toba au anakemea dhambi au anamhubiri YESU anayeokoa.
➡️Hebu ndugu niambie kwa Mara ya mwisho ulimsikia lini nabii katika Kanisa la Leo analionya Kanisa juu ya uzinzi na uasherati au analionya Kanisa juu ya dhambi?
Hakika kama ni hivi hakuko sawa katika Kanisa la MUNGU.
Hadi nakuletea ujumbe huu mfupi nimepitia Biblia na kuona manabii karibia wote na ujumbe wao ulikuwa na lengo la kutaka watu watubu na wamgeukie MUNGU huku wakiwa wakamilifu.
➡️Nabii wa Leo anakuambia tu "pokea gari" hata kama wewe ni mzinzi na unaisaliti ndoa yako.
Hakika hakuko sawa katika Kanisa wakati huu kama watu wako busy tu na kutabiriwa uongo.
◼️◼️Ndugu, YESU KRISTO anaokoa, ukimwamini Leo na kutubu dhambi na kuziacha, hakika unaokoka.
◼️Sio kwamba manabii wa kweli hawapo bali wapo ila ni wachache sana, wengi ni manabii wa uongo.
➡️Manabii wa uongo wako katika vitengo vingi walivyopewa na shetani, wanaweza hata kupingana wao kwa wao kwa sababu ya vitengo vyao japokuwa wote wanafanyia kazi ufalme wa giza.
Ngoja nikupe mifano hai mikubwa ya uongo wa baadhi ya manabii wa uongo.
1. Wapo manabii wa uongo hukataza watu kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi.
◼️Hapo wanadanganya watu maana Biblia inasema
Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;"
2. Wapo manabii wa uongo husema kwamba hakuna hukumu na wala MUNGU hatawapeleka waovu jehanamu.
◼️Hapo wanadanganya maana Biblia iko wazi sana inasema.
Mathayo 13:49-51 "Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. YESU aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam."
3. Wapo manabii wa uongo wanazuia watu kuoa na wengine wanawazuia watu kula baadhi ya vyakula alivyoumba MUNGU na ambavyo ni safi na havina madhara.
◼️Biblia inaonyesha hao ya kwamba ni waongo na wanafundisha uongo.
1 Timotheo 4:3-5 ''wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo MUNGU aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Kwa maana kila kiumbe cha MUNGU ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la MUNGU na kwa kuomba. ''
4. Wapo manabii wa uongo huwafundisha watu kutumainia vitu wao wanaita vya upako na sio MUNGU.
◼️Ni waongo hao kwa sababu Biblia inasema kwamba MUNGU hawezi kuchangia utukufu na kitu chochote kile.
Isaya 42:8 ''Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. ''
✔️✔️Maana moja wapo ya neno kuabudu ni kupenda kitu kupita kiasi na kufikia hatua ya kukiheshimu sana kiibada.
◼️Hivyo kutumainia mafuta ya upako, maji ya upako, chumvi ya upako n.k ni kumkosea sana MUNGU.
◼️Hivyo kuiheshimu sanamu, mawe, miti n.k ni kumkosea MUNGU.
Hizo ni baadhi tu ya mifano hai ya manabii wa uongo wanavyofanya kazi.
Ndugu, kama uko kwa manabii wa uongo basi hama haraka.
Nakushauru haya;
1. Okoka kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Warumia 10:13 ''kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. ''
2. Jiunge na Kanisa safi ya kiroho wanaohubiri Wokovu wa KRISTO.
1 Kor 2:4-5 '' Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za ROHO na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za MUNGU.''
◼️Kanisa la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO lazima lifundishe kwa pamoja utakatifu, maombi, kufunguliwa na kujitenga na dunia ya uovu.
3. Jiunge na Kanisa ambalo wanampa ROHO MTAKATIFU nafasi kwao.
Yohana 14:26 '' Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU , ambaye Baba(MUNGU) atampeleka kwa jina langu(YESU KRISTO), atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote
niliyowaambia. ''
4. Jiunge na Kanisa wanaofundisha Neno la MUNGU kwa usahihi bila kushikiliwa na taratibu chafu za dhehebu, kama zipo.
1 Petro 2:2-3 '' Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ikiwa mmeonja ya kwamba BWANA ni mwenye fadhili.''
5. Ukiwa katika Kanisa hakikisha unakuwa mtu wa ibada, maombi na anza pia kumtumikia Bwana YESU.
Waebrania 10:25 '' wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. ''Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments