MAOMBI YA KUFUTA MANENO YA WATABIRI WABAYA WA MAISHA YAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.


MAOMBI YA KUFUTA MANENO YA WATABIRI WABAYA WA MAISHA YAKO.


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU kisha tuombe maombi ya ushindi.
Ulimi wa mtu unaweza kutoa baraka au laana, unaweza kutoa mambo mazuri au mabaya na watu wengi zaidi hutumia ndimi zao kutabiri mabaya kwa ajili ya wengine.
Wako watu wamekuwa watabiri wabaya wa maisha ya wengine.
Hiyo yote ni kazi ya ulimi, wanautumia vibaya ulimi na kuwafunga watu kwa maneno mabaya.
Yakobo 3:5 '' Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.'' 

Leo nataka tufute maneno ya watabiri wabaya wa maisha yetu.
Nini maana ya kutabiri?
Kutabiri ni kueleza habari za mambo yatakayotokea baadae.
Kutabiri ni kutoa habari za mambo yanayokuja.
Je watu wanatabiri mambo gani kuhusu wewe?

Watabiri wengine husema ni MUNGU amewaambia na kumbe sio.
Wako watu kila siku huuliza mipango ya wengine  kwamba wanaendeleaje, wanafanya nini kisha wao husema utabiri mbaya juu ya watu hao wa MUNGU.
Inawezekana unapanga kujenga nyumba lakini watabiri wako wabaya wanasema ''haiwezekani huyu kujenga nyumba kamwe.''
Wako watu wakisikia una mchumba maneno yao yanabadilika, kila siku wanakutamkia kwamba hutaingia kamwe kwenye ndoa.
Wako watu mtoto wako anapofaulu tu chuo utawasikia wakisema 'hatapata kazi kamwe''
Inawezekana unaumwa lakini watu wanakutabiria kufa.
Watabiri wabaya wa maisha ya wengine wamekuwa wengi sana kwa baadhi ya watu.
Wako watu Biblia inasema juu yao kwamba ''Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.   ''Warumi 3:13-14 ''
Inawezekana ndoa yako sasa ina amani lakini kuna mtu kila siku anakutabiria ndoa yako kuwa na migogoro.
Watu wanaokutabiria mabaya kuna mengine usipoomba yanaweza kukupata hayo waliyoyatabiri.
Kinywa kina nguvu sana, watu wanaweza kukutamkia mambo ambayo yatakushika miaka mingi, sasa kama wamekutamkia mabaya kwa sababu hawakupendi ujue hata hayo yanaweza kukutesa.
Nuhu siku moja alimlaani kwa kinywa Mjukuu wake aitwaye Kaanani  na ikawa kama alivyotamka Nuhu
 Mwanzo 9:25 ''Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.''
Ajabu ni kwamba Kaanani alilaaniwa akiwa bado ni mtoto mdogo asiyejitambua tena akiwa hana kosa, alilaaniwa kwa kosa la Baba yake mzazi aitwaye Hamu.
 Yaani alikosea Hamu lakini akalaaniwa mtoto wa Hamu na uzao wake wote.
Unakumbuka Isaka alimbariki Yakobo kwa kinywa na ikawa vilevile?
Kinywa kina nguvu sana japokuwa watesi wako hutumia kinywa kukulaani au kukutamkia mabaya.
Mwanamke mmoja siku moja alinipigia simu akiomba nimuombee apate Mume na aolewe. Katika maelezo yake akaniambia kwamba kila mara huwa anamuona ndotoni mwanaume mmoja ambaye utotoni walikuwa wanakaa kijiji kimoja eneo moja wakiwa watoto wadogo na walikuwa wanacheza pamoja michezo ya kitoto. Sasa wakati wakiwa watoto wadogo kulikuwa na wamama majirani mara kwa mara walikuwa wanapenda kusema ''Nyie watoto mtakuja kuwa mume na mke baadae, mnaendana sana'' 
Maneno hayo yalimaanisha kwamba Mwanamke huyu na Yule Mwanaume wangekuja kuwa mke na mume halisi ukubwani. Sasa baadae wakawa watu wazima na michezo ya kitoto ya baba na mama haikuwepo tena, kila mmoja akaendelea na maisha yake na baadae yule Mwanaume akafunga ndoa. Tangu utotoni hawakuwahi kuwa na mahusiano yeyote na walikuwa marafiki tu na urafiki wao ulikoma wakiwa watoto wadogo maana kila mtu alisoma shule eneo lake. Sasa Mwanamke huyu baadae sana akiwa mtu mzima kupata mchumba ikawa vigumu sana, sasa alipoanza kuomba ili apate Mume akashangaa kila mara anaota ndoto akifunga ndoa na rafiki yake wa utotoni ambaye kwa sasa alishaoa na ana watoto. Sasa jambo hilo lilimchanganya kwa muda mrefu maana haiwezekani yeye aolewe na mume wa mtu, kumbe maneno waliyotamkiwa utotoni yalikuwa bado yanamshikilia kwamba yeye angekuja kuwa mke wa Mwanaume yule, anapomuona ndotoni ilikuwa na maana amefungwa agano lisilosahihi na mwanaume huyo hivyo alikuwa anajulishwa  alifute agano hilo baya ndipo atapata Mwenzi, agano hilo lilitengenezwa kwa maneno ya watu ya kila mara waliokuwa wanawatamkia wakiwa watoto wadogo. Naamini sasa unaona nguvu ya kinywa kwamba inaweza kuumba jambo ambalo linaweza kuja kumtesa mtu.
Inawezekana wewe watu walikutamkia kwamba utakufa kwa ajali au kwa ugonjwa fulani mbaya, ndugu maneno mengine yanaumba hivyo hakikisha kwenye maombi yako unafuta kwa damu ya YESU KRISTO kila neno baya ulilotamkiwa na wanadamu wasiokutakia mema.
Je wewe unateseka sasa kwa sababu ya maneno mabaya ya utabiri mbaya wa nani?
Kumbuka sio watu wote wanakupenda au wanakutakia mema, wengine inawezekana kabisa wamekuendea kwa waganga na huko umetamkiwa maneno ya kukufunga yaliyoambatanishwa na agano na sadaka, hiyo ni hatari sana.
Kuna watu ndimi zao zinatunga hila na maneno yao ni kama wembe mkali unaokata hivyo ukitamkiwa maneno na watu hao wabaya unaweza kujikuta umeshikiliwa kwa maneno yao hayo mabaya.
Zaburi  52:2-4 '' Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila. Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli. Umependa maneno yote ya kupoteza watu, Ewe ulimi wenye hila.''

Inawezekana unapanga kumtumikia Bwana YESU lakini watabiri wako wabaya wanasema haitawezekana.
Inawezekana kuna watu wanaomba maombi mabaya kuhusu wewe kila siku, maombi yao hayo hayajibiwi na MUNGU ila nguvu ya kinywa inayafanya mengine yatimie kwako.
Mithali 18:21 ''Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. ''

Wewe kama Mteule wa YESU KRISTO wakati mwingine maneno ya watabiri wabaya yanaweza kukusimamisha kupitia maneno yao mabaya waliyokutamkia.
Wako watu kila siku asubuhi, mchana na jioni ni kutabiri tu mabaya kwa wengine, ndugu leo futa maneno yao yote mabaya waliyokutabiria.
Inawezekana majirani zako ndio wanakutabiria mabaya.
Inawezekana wafanya kazi wenzako ndio wanakutabia mabaya.
Inawezekana baadhi ya ndugu zako ndio wanakutabiria mabaya.
Inawezekana wasiokupenda ndio wanakutabiria mabaya.
Inawezekana wenye wivu na wewe ndio wanakutabiria mabaya.
Inawezekana hawakutamkii mabaya wewe ila walimtamkia Babu yako na uzao wake hivyo mabaya hayo umeyarithi kwa Baba yako na yeye aliyarithi kutoka kwa Baba yake.
Inawekana uzao wa tumbo la mama yako ulilaaniwa hivyo na wewe kwa sababu umetokana na mama yako basi na wewe uko chini ya laana ya zamani.
Leo katika jina la YESU KRISTO futa kila maneno ya watabiri wabaya waliyoyatamka kukuhusisha  wewe.
Wako watu walitamkiwa kwamba watafukuzwa kazi na ikawa vilevile.
Wako watu walitamkiwa kwamba ''Atakayekuoa wewe labda awe taahira'' na kweli umekuja kuolewa na mtu mkatili na anakunyanyasa na kukutendea mabaya sana na kukusaliti, na utabiri umetimia maana mume wako ni zaidi ya taahira.
Inawezekana wako waliokutamkia kwamba ''Wewe utaona mwanamke mapepe'' na imekuwa vilevile umejikuta umepata mwanamke mapepe nusu mapepo.
Najisikia nguvu sana kukuambia kwamba leo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO utabiri mbaya wote kuhusu maisha yako, afya yako, kazi yako, ndoa yako, uchumba wako, uchumi wako na kila baraka yako, huo utabiri mbaya unaenda kufutika wote na kuanzia leo hautashikiliwa tena na maneno ya watabiri wabaya waliokutabiria tangu hujazaliwa na hata sasa.
Bwana YESU mwenyewe Mwokozi wako anakupa kibali leo akisema kwamba ''Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.-Yohana 14:14'' Tena Neno la MUNGU liko wazi sana leo kwamba kama YESU KRISTO atakuweka huru leo hakika utakuwa sio huru tu bali utakuwa huru kweli kweli.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana(YESU KRISTO) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.''
Hakikisha tu YESU KRISTO ni Mwokozi wako, kama hujaokoka hakikisha unaokoka leo leo na utapata kibali cha MUNGU kinachoruhusu damu ya YESU KRISTO kufuta laana za vinywa zote ulizotamkiwa na watu wabaya wa kila aina.
Je watu walikutabiria mabaya gani hata yanakutesa sasa?
Mtumishi mmoja wa siku siku moja alipata ufunuo wa kuyakamata maneno mabaya yote aliyotamkiwa na mawakala wa shetani kisha maneno hayo akayachoma moto kwa damu ya YESU ndipo baada ya muda wale walimtabiria mabaya walibaki wakishangaa, hayakumpata kamwe hata kama walihusisha hadi na uganga na uchawi.
Ndugu, Kwa YESU KRISTO kuna ushindi wa ajabu sana kama ukijitambua, ukajipambanua kiroho na ukamtambua YESU KRISTO kama ndio Mwokozi wako.

Ni akina nani wanaweza kukutabiria mabaya na mabaya hayo yakakupata kama hukujua kuomba?

1. Wewe mwenyewe.

Inawezekana  ni wewe mwenyewe ulijitabiria mabaya au unajitabiria mabaya.
Kama ni hivyo tubu na acha kujitabiria mabaya.
Mithali 6:2 ''Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako, ''
Kuna njia nyingi mawakala wa shetani wanaweza kutumia ili kukufanya ujitamkie mabaya ambayo yanaweza kukushikilia usipojua jinsi ya kujinasua.
Moja ya silaha za shetani ni kukufanya ukate tamaa au uwe na hasira hivyo kujikuta unajitamkia mambo mabaya ambayo yatakutesa mwenyewe baadae.
Mfano inawezekana ni binti umekosana na mchumba wako na marafiki zako wakajua kwamba umeachwa, sasa kwa hasira unasema ''Kwani nini, hata nisipoolewa haina shida, kwanza mimi sio mwanamke wa kwanza kuishi duniani miaka yote bila kuolewa''
Maneno hayo ukiyachunguza unagundua kwamba ndugu huyu amekubali kuishi bila kuolewa miaka yake yote ya kuishi duniani, sasa aliyasema hayo kwa sababu ya hasira lakini hasira ikiisha na miezi kadhaa ikapita atarudi katika hali ya kawaida ndipo ataanza tena kuomba au kutamani kuolewa, amesahau kwamba maneno yake hajayafuta hivyo bado majini wanafuatilia kuhakikisha maisha yake yote haolewi, kwanini majini wamfuatilia? ni kwa sababu amefungua mlango maana amesema kwamba maisha yake yote hata asipoolewa ni sawa tu.
Sasa mtu anaweza kuteswa na maneno aliyojitamkia mwenyewe hasa kipindi alipokuwa na hasira au amekata tamaa.
 Hata ahadi unazojisemea mbele za MUNGU hakikisha unatimiza, hata nadhiri unazowaahidi watumishi waaminifu wa MUNGU hakikisha unatimiza maana maneno hayo tu yanaweza kukushikilia na kukutesa au kugeuka kifungo baadae.
Mhubiri 5:2 '' Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za MUNGU; kwa maana, MUNGU yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.'' maana yake hakikisha unasema maneno ya kweli mbele za MUNGU.
Ngoja nikupe mfano hai, mimi katika kuombea watu walio mataifa mbalimbali na maeneo mbalimbali baadhi ya watu waliwahi kuahidi kwamba watanunua vyombo vya kuhubiria injili, wengine wakasema wanahitaji mahubiri yangu ya video hivyo watanunua kamera na laptop ili kuwezesha mahuburi ya video, wengine walisema wanahitaji mahubiri ya audio hivyo watawezesha vifaa vinavyoweza kurekodi sauti vizuri na mahubiri hayo wayapate, ni ahadi nyingi sana.  Sasa kwa mfano kama MUNGU ameamua kutokufungua mlango mwingine kwa sababu wapo aliowapa agizo hilo ndio hao walioahidi maana waliahidi mbele zake. Sasa kama watu wale watasahau au wataghairi na kumbe wanatakiwa kuwezesha hayo waliyoahidi basi miaka inaweza ikaenda na mtu baadae akajikuta anaadhibiwa na MUNGU na sio nguvu za giza, Hata mimi walioniahidi wala sikumbuki  na nilishasahau zamani sana hivyo wakati huu nakuwa sijui chochote, kumbe yuko mtu aliahidi mbele za MUNGU na sio kwangu.
Inawezekana wewe uliahidi kufanya jambo fulani kanisani lakini baadae ukasahau na hata watu wa Kanisa wakasahau lakini MUNGU huwa hasahau hivyo unaweza kujikuta unapitia magumu sana na ni MUNGU ameyaagiza kwa sababu tu uliahidi mbele zake na hukutimiza.
Kumbuka Yona ndiye alitakiwa kuhubiri Ninawi, hivyo kuchelewa kwa Yona kwenda Ninawi haikuwa na maana kwamba MUNGU atafute mtu mwingine wa kwenda kuhubiri Ninawi, Yona aliendelea kusubiriwa Ninawi hadi alipofika na kukamilisha jukumu alilopewa na MUNGU lakini mapigo hakuyaepuka Baharini.
Ndugu, unaweza ukashikwa kwa maneno ya kinywa chako na jambo hilo likageuka tatizo kwako baadae.
Kuna namna nyingi sana unaweza ukajifunga mwenyewe kwa kinywa chako.
Yako mengi unaweza kujitamkia mwenyewe kumbe ni wewe unajitabiria mabaya ambayo yanaweza kukutesa sana.
Hata mimi kuna kipindi niliumizwa sana na nikaanza kujitamkia kwamba ''MUNGU naomba unichukue mbinguni, uniue ili nije tu mbinguni maana ya dunia yamenichosha'' Sasa hata siku mbili hazikupita nilianza kuona roho ya mauti ikinifuatilia kwa speed kali sana, nusura nigongwe na gari yaani ilibaki sekunde chini ya mbili nigongwe, nusura nigongwe na bajaji ila ikamgonga mtu aliyetokea ghafla nyuma yangu na sijui kama mtu yule alipona maana alichukuliwa akiwa hawezi chochote, niligundua kwamba kwa sababu nilitamani kufa basi majeshi ya pepo wabaya walitaka kutimiza hilo haraka kabla sijagundua kwamba nimekosea. Namshukuru MUNGU maana nilipata ufunuo hivyo nikaanza kuomba maombi ya kutubu kwa sababu ya maneno hayo niliyojitamkia, Namshukuru Bwana YESU maana nilisamehewa na roho za mauti hazikunifuatilia tena. 
Unajifunza nini?
Unaweza kujitamkia mabaya na ukashangaa maneno hayo yamefungulia uharibifu kutoka ulimwengu wa roho wa giza.
Kumbuka Biblia inasema ''Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.-Mathayo 12:37 ''

2. Watu wengine.

Zaburi 41:5 ''Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea?  ''
Inawezekana sio wewe umejitabiria mabaya ila kuna watu ndio wamekutamkia mabaya yanayoweza kukutesa.
Watu hao inawezekana uliwahi kuishi nao mkoa fulani au eneo fulani, inawezekana ni wazazi wako au ndugu zako, marafiki, wanafunzi wenzako n.k

3. Maajenti wa kuzimu.

Maajenti wa kuzimu ndio mawakala wa shetani, hao hata huhitaji kusikia kama wamekutamkia mabaya bali ndio kazi yao, hao ni pamoja na  ni falme za giza, huko kuna wahusika na hao wanaweza kukutabiria mabaya, mamlaka za kipepo,wachawi, mizimu, wakuu wa giza na kila majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Hao siku zote wako ili tu kuhakikisha hufanikiwi katika maisha yako.
Mawakala hao wa kuzimu wanaweza kukukosesha kama hutajua kujinasua na utabiri wao wa kishetani.
Yeremia 23:13 '' Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli.''

Nini ufanye kutokana na utabiri mbaya kukuhusu?

1. Tubu kwa ajili ya chanzo cha tatizo lililosababisha ukashikiliwa na maneno ya watabiri wabaya.
 Ayubu 42:6 ''6 Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu. ''

2. Ifute  nguvu ya maneno mabaya waliyokutabiria.
Hesabu 13:30-31 '' Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.''
Kalebu alikuwa anaifuta nguvu ya wana wa Anaki japokuwa  wenzake walikuwa wanawaona wanefili kuwa hakuna wa kuwapiga, MUNGU aliwapiga hao wanefili na Israeli wakapita salama.
Hata wewe kwa damu ya YESU KRISTO ifute nguvu ya maneno ya waliokutabiria mabaya, hata kama wana nguvu sana hao waliokutabiria mabaya.

3. Futa maneno yote ya utabiri mbaya kukuhusu wewe.
Yeremia 14:14 '' Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao. ''
MUNGU hakuwatuma hao ili wakutabirie mabaya hayo hivyo yafute kwa damu ya YESU KRISTO yatafutika.

4. Jitabirie mema kwa jina la YESU KRISTO.
Yoeli 2:28 '' Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; ''
Wewe uliye Kanisa umepewa kibali na MUNGU cha kutabiri mema, hivyo anza kujitabiria mema kwa maneno au kwa maombi yako.

5. Mche MUNGU na epuka kijitamkia mabaya pia amua kuishi katika kusudi lake la Wokovu wa KRISTO YESU.
Zaburi 34:13 '' Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila. ''

6. Usivunjike moyo kutokana na utabiri wao bali ongeza juhudi na kaa katika kusudi la MUNGU na maombi.
Zaburi 64:3-8 '' Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu, Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.  Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona?  Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa.  Kwa hiyo MUNGU atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa. Ndivyo watakavyokwazwa, Ulimi wao wenyewe ukishindana nao. Wote wawaonao watatikisa kichwa. ''

7. Omba ROHO MTAKATIFU akufundishe na kukuongoza.
Zaburi 32:8 '' Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.   ''

8. Endelea na kuliweka Neno la MUNGU moyoni(Wakolosai 3:16) huku ukiendelea pia na maombi.
1 Thesalonike 5:17 ''  ombeni bila kukoma; ''


Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa na somo hili  nitalifafanua zaidi ndani ya kitabu.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane na nitakujulisha jinsi ya kukipata na Naamini kitakusaidia sana.
Hapa chini ni
MAOMBI YA KUFUTA MANENO YA WATABIRI WABAYA WA MAISHA YAKO.
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea. Kumbuka pia fundisho ni muhimu kuliko maombi hivyo wewe ambaye huwa unahusika na maombi tu hakikisha unajifunza kwanza somo lote ndipo utapata nguvu za kuomba na kushinda.

MAOMBI YA KUFUTA MANENO YA WATABIRI WABAYA WA MAISHA YAKO.

 MUNGU Baba wa mbinguni ninakuabudu na ninaungana na maserafi na makerubi kukuabudu wewe.
Ninakushuru MUNGU wangu maana umenilinda na kunipa afya njema na uzima.
Ninaomba BWANA unisamehe dhambi zangu zote, makosa yangu yote na maovu yangu yote.
Wewe MUNGU Baba unasema  '' Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.-Isaya 43:25 ''  Hivyo ninaomba unisamehe Bwana YESU.
Ninaomba damu ya agano ya YESU KRISTO Mwokozi wangu inifutie hatia zote zinazonikabili zilizo katika ulimwengu wa roho.
Ninatubu kwa ajili ya kila chanzo cha kifungo kilichotokana na kinywa cha mtu yeyote, majini, mizimu na kila majeshi ya pepo wabaya.
Ninatubu BWANA kwa ajili ya kila chanzo kilicholeta mateso kwangu na vifungo, ninaomba MUNGU BABA unisamehe mimi na mlango uliokuwa umefunguliwa ili niendelee kuteseka kwa sababu ya maneno hayo, sasa kwa jina la YESU KRISTO mlango huo ujifunge na asiwepo wa kuufungua.
Kwa mamlaka iliyomo ndani ya jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu ninafuta kila nguvu ya maneno mabaya ya kila watabiri wabaya wa maisha yangu, ninaifuta hiyo nguvu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Sasa ninafuta kila maneno ya utabiri mbaya yaliyotamkwa ili kunifunga mimi. ninafuta maneno hayo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno ya kipepo yaliyonifunga yaliyotamkwa kipindi sijazaliwa, hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno mabaya niliyotamkiwa utotoni, hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno mabaya niliyotamkiwa na wachawi na majini,hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno mabaya yaliyotamkwa kwenye madhabahu za giza popote, hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno mabaya niliyotamkiwa kwa waganga wa kienyeji,hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno mabaya yaliyotamkwa kazini kwangu, hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila maneno mabaya niliyotakiwa na ndugu zangu au watu wangu wa karibu ili kunifunga mimi, hayo maneno mabaya nayafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Niko kinyume na kila mchawi, mshirikina, mwanga,msoma nyota na mnajimu wa kina aina, niko kinyume na kila wakala wa shetani aliyenitabiria mabaya.
Katika jina la YESU KRISTO sasa ninafuta kila neno la siri au lililotamkwa kwa wazi ila linanifunga mimi, Neno hilo nalifuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya ambalo ni mimi mwenyewe nilijitamkia, Eee MUNGU Baba naomba unisamehe kwa makosa yangu hayo na ninaomba maneno hayo niliyojitamkia mimi mwenyewe yafutike sasa, kwa damu ya YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Enyi mawakala wa shetani sasa hamtaniweza kamwe, imeandikwa katika Zaburi 118:13-14 kwamba  '' Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini BWANA akanisaidia. BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.'' 
Ni kweli mlinisukuma kwa maneno yenu ili niangamie, ni kweli mlinitamkia mabaya ili nidhurike lakini leo MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi ndiye MUNGU wangu na sasa namwita yeye ili anisaidie, hivyo kwa jina la YESU KRISTO natangaza kuangamia kwao mawakala wa shetani wote waliokuwa wamenishikia maisha yangu kwa laana zao za kichawi.
Mmenitesa muda mrefu sana, mmetesa familia yangu muda mrefu sana, mmenisukuma muda mrefu sana lakini MUNGU wangu sasa ananishindia na hamtanipata tena.
MUNGU wangu katika KRISTO YESU ndiye Mweza yote.
MUNGU wangu anasema sasa '' Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.-Isaya 43:11 ''
Nimemkimbilia Mwokozi wa maisha yangu hivyo kuanzia sasa zitadhulika na nguvu za giza kamwe.
Leo ndio mwisho wa kila neno la laana nililotamkiwa na wakuu wa giza.
Katika jina la YESU KRISTO ninafuta kila laana zilizotoka katika ulimwengu wa roho wa gza, nazifuta kwa damu ya YESU KRISTO Mwokozi wangu.
Kila neno baya lililotamkiwa afya yangu au mwili wangu, hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya llilotamkiwa ndoa yangu au uchumba wangu, hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila Neno baya nililotamkiwa uchumi wangu au kazi yangu,hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa uzao wangu au familia yangu,
hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa kibali changu au huduma yangu,
hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa pesa yangu au malengo yangu, hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa biashara yangu au kipato changu, hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa ili niugue au nife, hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa  ili nifilisike au nikose kazi, hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila neno baya lililotamkiwa kuhusu chochote cha kwangu,
hilo  neno baya nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Katika jina la YESU KRISTO ninayakamata maneno yote mabaya niliyonenewa kutokea popote, nayakamata na ninayachoma moto kwa damu ya YESU KRISTO.
Kuanzia sasa hakuna neno la wakala wa shetani au la mwanadamu yeyote litakalonishikilia.
Imeandikwa  katika Isaya 54:14 kwamba  ''Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.-'' Hivyo kuanzia leo hakuna neno la wakala wa shetani yeyote litakalonishikilia, hakuna adui anatayenionea.
Ninakushukuru MUNGU Baba maana katika wewe nimeshinda na zaidi ya kushinda.
Ni Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
 Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen.
Hakika umeshinda. Ukiweza kufunga unaweza kufunga hata siku 1 au 3 au 4 au hata 5 au zile ambazo wewe utaona unaweza ukihusika kila siku na kipengele kuombea na kumbuka baada ya maombi ya kufunga au hata maombi ya bila kufunga fanya tendo la imani kwa MUNGU kwa kutoa sadaka nzuri itakayoambatana na maombi juu ya ukomo wa kuteswa na maadui zako katika ulimwengu wa roho
Nawaonya pia wanaotumia masomo yangu vibaya na kwa manufaa yao waache tabia hiyo.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsap).


Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments