MATOKEO MAZURI YA MAOMBI HUTOKANA NA MAMBO HAYA MANNE(4).

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

◼️Maombi ni jambo la Muhimu sana kwa kila Mteule wa KRISTO katika KRISTO YESU.
Ukizuiliwa kufanya Maombi umezuiliwa mambo mengi sana.

Waefeso 6:18" kwa sala zote na maombi mkisali KILA WAKATI katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;"

➡️Maombi ni kama kupumua, usipopumua unakufa, Na usipokuwa mtu wa maombi unakufa kiroho.

✔️✔️Maombi kwa mteule wa KRISTO yana maana nyingi sana.

Luka 21:36 "Basi, kesheni ninyi KILA WAKATI, MKIOMBA, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu."

◼️Maombi ni njia ya kumtumikia MUNGU na kumtii.

Wakolosai 3:24 "mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana KRISTO."

Kumtumikia MUNGU ni  kufanya kazi ya MUNGU katika KRISTO YESU.
Kumtii MUNGU ni kutimiza maagizo yake.

◼️Maombi ni ni njia ya kukuonyesha kwamba unamhitaji MUNGU katika maisha yako.
Muombaji anayehitaji matokeo sahihi jifunze hapa.

Wafilipi 4:6-7 " Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na MUNGU. Na amani ya MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISTO YESU."

◼️Unayehitaji matokeo mazuri ya maombi yako kulingana na Wafilipi 4:6-7 zingatia haya;

1. Hakikisha unakuwa mtu wa kusali.

Warumi 12:12 "kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;"

◼️Kusali ni Muhimu sana Ukitaka matokeo mazuri ya Maombi Yako, watu wengi huomba Kisha wanaendelea na mambo yao, wakati Mwingine Malaika anayeleta majibu akikukuta unafanya mabaya anaweza asikupe majibu ya Maombi Yako hivyo kudumu katika kusali ni kitu Cha Muhimu sana Ili kukusaidia ubaki katika Utakatifu na itakuwa rahisi kwako kupokea majibu ya Maombi Yako.
Mfano ni Wewe Mzazi Mtoto wako amekuomba umletew Zawadi, wakati anaomba alikuwa msafi lakini wakati unamletea Zawadi unakuta Mtoto huyo amejisaidia Kisha akajipaka kinyesi Nina hakika hutampatia zawadi kwanza hadi aoshwe awe safi,na Kwa MUNGU ipo hivyo.
Biblia hapo juu inakumbusha unapodumu katika Maombi dumu pia katika kusali, Hakikisha unakuwa Mtu wa Ibada.

◼️Mtu wa kusali ni mtu wa ibada.

2. Hakikisha unaomba.

◼️Ili upate matokeo mazuri ya Maisha Yako Hakikisha hulalamiki tu Bali Hakikisha unaomba.
Usitamani jambo bila kuomba, ukitamani bila kuomba jambo hilo halitakuja, MUNGU anataka uombe utapewa unachoomba kilicho katika mapenzi yake.

1 Yohana 5:14-15 " Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba."

◼️Kwa kila kitu tanguliza maombi.

3. Hakikisha unakuwa ni mtu wa shukrani kwa MUNGU.

◼️Watu wengi sana hawaishi Maisha ya Shukrani, Ukitaka Matokeo makubwa ya Maombi Yako uwe Mtu wa kutanguliza Shukrani kwa MUNGU.
Biblia inakumbusha kwamba unapodumu katika Maombi Kumbuka na kumshukuru MUNGU pia.

Wakolosai 4:2 "Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;"

◼️Hakikisha unakuwa Mtu wa Shukrani ya Maombi, siku Moja Bwana YESU aliomba Maombi ya Shukrani tu na Muujiza ukatendeka, hiyo inatufundisha umuhimu wa kumshukuru MUNGU ulivyo na matokeo mengi.

Mathayo 15:36-37 " akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa."

◼️Na Shukrani ya Sadaka ya Shukrani.

Zaburi 50:23 "Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa MUNGU."

◼️Ni wenye Imani kubwa tu ndio wana uwezo kutoa Sadaka ya Shukrani kwa MUNGU baada tu ya Maombi hata kabla hawajapokea mahitaji yao.

4. Hakikisha mahitaji yako MUNGU anayajua.

Isaya 43:26 "Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako."

◼️Usiseme tu MUNGU anaona Bali omba kwa MUNGU katika KRISTO YESU ukitaja Maombi Yako.

◼️MUNGU atayajua mahitaji yako kupitia maombi yako.
Wako watu walikuwa na matatizo na MUNGU aliona matatizo yao ili aliyaondoa kwao walipotamka kwa vivywa vyao wakiomba awaondolee.

✔️✔️Mfano ni Bartimayo kipofu.

Luka 18:41 "Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwana, nipate kuona."

◼️YESU alikuwa anajua Bartimayo ni kipofu ila alimuondolea upofu alipoomba kuondolewa upofu, asingeomba kuondolewa upofu angebaki kipofu, Ndugu Hakikisha unakuwa na muda wa kuomba kwa MUNGU katika KRISTO YESU.
Mweleze MUNGU Kwa Kinywa chako kwamba unahitaji Nini.

✔️✔️Kuna watu wengine wawili YESU alikuwa anajua wanahitaji Nini ila hadi walipomweleza ndipo akawatendea wanachohitaji.

Mathayo 20:30-34 " Na tazama, vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba YESU anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi! Mkutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi! YESU akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini? Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe. YESU akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata."

➡️Hata kwako ni hivyo hivyo YESU KRISTO anasubiri utamke kwa Kinywa chako unahitaji Nini.

Usiishie tu kusema Mchungaji wangu anajua hitaji langu, na Mtumishi Fulani anajua hitaji langu, Inawezekana hao hata walisahau kukuombea, Hebu tubu Kisha mweleze YESU KRISTO Wewe mwenyewe kwa Kinywa chako atakutendea.

◼️Inawezekana hitaji lako ni Kufunga Ndoa, kuzaa, kupata kazi, kujenga Nyumba, kupata mtaji n.k

◼️Ndugu omba katika Jina la YESU KRISTO huku ukizingatia na mambo mengine 4 hapo juu utafanikiwa haraka.

◼️Omba katika Jina la YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Mbinguni.
Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments